Nashauri makamu mwenyekiti CHADEMA apumzike tu siasa, yanini kujilazimisha na haiwezekani kamanda?

Mungu ni wa wote gentleman,

na ndie alienifanya mimi nimuonee huruma huyo muungwana, lakini pia aliekupa wewe uwezo wa kujaribu kumpa ujasiri asiejiweza..

Sisi sote ni waja wake, na kwa wakati muafaka apendavyo yeye kila moja atarejea kwake..

hakuna haja kujihesabia haki wala kujipa umuhimu zaidi ya wengine kwa Mungu..

hata hivyo,
ni ukweli usiopingika kwamba muungwana anahitaji kupumzika na nashauri chama kuchukua hatua stahiki kwa mustakabali wa ustawi wake..

wampatie nafasi ashughulikie masuala yake binafsi, ambayo kwasasa kwa kiasi kikubwa anayabeba na anayaasociet na chama, kitu ambacho si sawa na hana uwezo wa kuwakabili inavyostahili πŸ’
 
Kwanini unapenda kuona upinzani dhaifu?
si kweli,
upinzani si dhaifu nchini. udhaifu ni mipango mikakati yao, chuki binafsi baina yao, migawanyiko, uchu wa madaraka na vyeo, tamaa na usaliti miongoni mwao ndiyo hasa changamoto..

hata hivyo,
ushauri wangu kwa chadema ni wa kiutu na kibinadamu zaidi. Nimejawa huruma gentleman πŸ’
 
Unadhani uliyo zungumza kunayoyote angekuzuia kuzungumza. La hasha kwasababu ni wewe mwenyewe umeyabuni kutoka kwenye kichwa chako. Kwakuwa watu wanaupeo tofauti tofauti za kufikiri na kujua mambo, basi niseme kuwa upeo wako siyo mwisho wakufikiri kwa wengine, huo ni mchango wako na mawazo yako si lazima na wengine waweze kuwaza kama uwazavyo wewe. Ndiyo maana maamuzi mengi huwa yanafanywa na jopo la maamuzi.
 
Amekuwa Magufuli aliyekuwa anapumua kwa kutumia moyo unayotumia umeme?wenye umeme wakikata wao umeme hakuna kupumua.
kwani muungwana ana Tatizo la kiafya gentleman?πŸ’
 
Miujiza tena?
 
Kama wewe ndio LISSU yaliomkuta tungalikuwa tushakuzika au unaokota makopo njiani. Kumininiwa risasi kama mvua lkn bado ukawa unacheka, unaimba na unafurahi hata kuliko huyo aliekumiminiya risasi sio jambo la kawaida ktk dunia hii. Tunaona askari tu akibambikiwa kesi kama ya wizi makazini kwa bahati mbaya ,akichomoka tu anarudisha magwanda na anatafuta jembe akalime, anaona isiwe na noma.
 
Jiwe alipiga pushups kwenye majukwaa leo hii yupo wapo boss? Mbona hukumuonea huruma? Usichezee huruma yako kwa wasiokuhusu, itakuwa matumizi mabaya sana ya huruma
Plz plz gentleman tuwage na huruma kwa wenzetu, na hakuna haja kufananisha mambo yasiyo fanana hata kidogo..

kwani muungwana ana Tatizo la kiafya? huruma yangu ni kwamba hali aliyonayo inaweza kuzalisha tatizo la kiafya na hiyo haitakua nzuri..

vilivyomo ndani ya mwili wake nadhani vinahitaji utulivu zaidi ya kashkash na mbilingembilinge za kisiasa..

Nadhani pale chadema wapo wengi sana wa kuchukua wajibu huo na huyu muungwana akapata wasaa wa kutosha kujihudumia na kupumzika πŸ’
 
Wakutumwa wakutumwa.
Ugali noma.
mdogo wake hamza unajulikana vizuri hunaga huruma kama hamza tu kaka yako uliembandika kama avatar yako. Katili sana wew gentleman πŸ’

ugali ndio unamfanya muungwana akomae jukwaani hata kama hawezi, right?
 

Tunza tu huruma yako kiongozi, wapo wengi sana wa kuwahurumia huko vijijini wanabebana kwenye matenga kwenda kutibiwa, wape tu hiyo huruma yako! Achana na Simba baba atakutesa sana. Chawa wote lazima wataje jina lake kutafuta relevance. Mbona yupo juu sana tu? Huoni? Hivyo vilivyomo ndani yake havikuhusu, we mzima angalia yako, mbona dunia ina mambo mengi tu ya kufanya mkubwa?
 
wacha tuchague wenyewe.. kwani wew ni nani hadi utuchagulie... out of 100% .. 80% yote anaongelea yeye kutaka kuuwawa... 20% ndo unaona anatema cheche za kuwanufaisha wadanganyika...

tutachagua kiongozi kwa huruma yetu kwake na sio sera zake..
😁😁😁😁😁😁
 
Vipi kama ukamshauri Menyekiti?
 
Amekusikia ili atulie nyumbani uwe unampikia chakula huku unachelea rungu.
 
umezungumza vizuri sana gentleman,

haya ni maoni, mtazamo na huruma yangu kwa namna nimuonavyo muungwana kwenye majukwaa ya kisiasa..

ni muhimu sana,
ikiwa kuna mawazo mapya na fikra mbdala bora zaidi, sawa au kinyume na hoja yangu wadau wako Free kuyatoa kwa mustakabali mwema wa umoja, amani, utulivu na ustawi wa Demokrasia ndani ya vyama vya siasa nchini πŸ’
 
Wewe unaita malalamiko binafsi lakini hayo malalamiko ndio wanayotendewa watanzania wengi ila tatizo wanakosa sehemu ya kusema na wengi wanaogopa mkono wa dola kuwarudia kwa mara ya pili.
Mleta uzi Lissu ni asset kwenye nchi hii,uwezo wake na kuponea tundu la sindano kwenye shambulio la mvua ya risasi ni uthibitisho tosha kuwa Mungu ana kazi naye hapa duniani.
Kama wewe binafsi unamuonea huruma na kutaka aache siasa ni ngumu kukuelewa.
Kupigwa kwake risasi kulitokana na yeye kuwa mwanasiasa.Sasa inakuwaje leo amenusurika kifo aache siasa na ulemavu alioupata kwenye siasa??

Nakushauri onea huruma familia yako na wazazi wako mbona nao wana hali mbaya ya umaskini??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…