Nashauri msafara wa Rais Samia nchini Marekani, uwe ndio msafara wake hapa nchini ili tupunguze magwanda na mitutu

Wenzetu wana technology ya hali ya juu unaona magari machache lakini pembeni huko kuna walinzi na vifaa vya ulinzi kibao na vya gharama kubwa.
 
Kwahiyo Magufuli alikuwa anakwepa kukaa karibu na raia maana hajafanya kitu?
Ulinzi wake ulikua kwa ajili ya wasiofurahishwa na aliyokuwa akiyafanya kwa manufaa ya Taifa.
 
Sasa mbwembwe za chama tawala unataka wazipigie Lumumba? Kinachoonekana sasa hakikuwahi kufanyika hata wakati wa ukoloni, gavana alitembea huru bila kulindwa na mabunduki na makombora ya kwenye helikopta, kura zetu zimetujengea uadui na tuliowachagua.
 
Sisi tuna mbwembwe nyingi sana na ushamba mwingi tu.
Yaani tumepitiliza. Kuanzia ya eti wanausalama kukaa nyuma ya rais. Mpaka polisi, jeshi, magereza, waziri mkuu na spika, mpaka vyama vya upinzani!😅😂🤣. Vituko mpaka unahisi kweli yawezekana wabongo wana IQ ndogo sana. Ndiyo! Tunajali upuuzi kama huo wakati kuna ya maana ya kufanya. Bado miundombinu hovyo, huduma za afya, ustawi wa jamii, elimu, uwajibikaji nk.
Twapenda kujionyesha tuko juu kumbe bado sana. Umaskini twautaka wenyewe. Tuna rasilimali na maliasili zisizoisha. Ila uwajibikaji na ubunifu. Hata mama azunguke mpaka north pole kama hatuwezi simamia hela na mali zetu tutabaki maskini tu huku wachache wakiishi kama malikia na wafalme😡🤬
 
CCM ukiwaambia Kuna wakuu wa nchi wanakwenda ofisini na baiskeli watasema ni uzushi. Ukimwambia Idugunde kwamba Angela wa ujerumani alikua anakaa kwenye flat na wapangaji wenzake na alikua anapika chakula chake na kufua nguo zake atasema ni propaganda ya TLP ya Mrema
 
Rais akiwa ugenini,nchi mwenyeji hubeba dhamana ya ulinzi,usione hakuna watu ukadhani hakuna ulinzi,angalia msafara wa Waziri mkuu wa uingereza..hutoona walinzi,si kwamba hawapo
 
Wewe ndio muongo.
 
Rais akiwa ugenini,nchi mwenyeji hubeba dhamana ya ulinzi,usione hakuna watu ukadhani hakuna ulinzi,angalia msafara wa Waziri mkuu wa uingereza..hutoona walinzi,si kwamba hawapo

Huku inashindikana nini ulinzi kuwa wa hivyo maana huku ndio amepigiwa kura?
 
Kila idara ya usalama Ina namna yake inayoona inafaa kuweka usalama

Hakuna cha zaidi ya uwezo mdogo wa kufikiri na kutengeneza mazingira ya upigaji. Ule ujinga eti rais anapita wananchi wanasimamushwa hadi masaa mawili huko hakuna ndio maana wana maendeleo. Huku rais anaingia madarakani kwa kupora uchaguzi, halafu eti anageuka muheshimiwa na kusujudiwa juu!
 
Tena masokwe kabisa
 
Mtu akiwa nchini kwake ndio tishio linakua kubwa , akiwa kwa mzungu yuko na amani ya bwana.
 
Ni woga au kukosekana kwa amani nchini kunasababisha hii misururu mirefu?
 
Ingekuwa viongozi wetu wakisafiri nje wanajifunza mambo mazuri wanayoyaona (kama huwa wanayaona) tungekuwa mbali sana. Hata boda boda hawangehatarisha usalama wa waenda kwa miguu unaouona hapa Bongo!
 
Kule anaonekana kama diwani
 
matumizi mabaya ya fedha za umma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…