Unaweza ukaliweka hivyo na ukaeleweka na baadhi ya watu ila lengo langu ni kumpa muda wa kuwa na maamuzi binafsi yasiyotokana na influence nyingine hasa wakati huu anapoanza kufanya kazi.
Huko mbeleni haina shida ila kwa sasa itamfanya asiwe na misimamo yake binafsi na watu watashindwa kuielewa misimamo yake yeye mwenyewe.
Mimi sidhani kama anaweza kusoma kitu mtandaoni halafu akakibeba hivyo hivyo.
Lazima atafanya uchunguzi wake kujiridhisha.
Na sio kwamba ndio anategemea mtandao as a main source.Naamini hii ni mojawapo tu kati ya njia zake nyingi kupata taarifa na kushauriwa.
Inawezekana pia haya ni maamuzi ya system yake na wanamsaidia kuhakikisha anapata anachotaka na sio kwamba ni yeye mwenyewe yuko mtandaoni full time au kwamba yeye personally ndio anaendesha zile accounts zake.
Inawezekana pia uwepo wake mitandaoni unaleta mtazamo fulani kwa jamii ambao in turn unaipa system feedback fulani wanayoitaka kirahisi tofauti na kama wangejificha na kutokuwa public.
Pia pre emptying ni mojawapo ya faida inayoweza kupata system ya mama kwa wao kuzoeleka mitandaoni kama hivi.(kama una idea ya intelijensia utanielewa hapo).
System inabadilisha mbinu kila wakati kulingana na mahitaji ya wakati kwa namna wao wanavyotaka kuendesha nchi.
Hivyo hata baadhi ya tabia kiongozi anafundishwa kuziadopt ili awe na taswira fulani katika jamii kwa wakati fulani na sababu fulani.
Nikudokeze tu kwamba sio mama pekee aliyeingia mtandaoni,viongozi wa serikali ya awamu ya sita wengi wameanza kuwa very active mitandaoni.
So nadhani this is planned na system iko aware na huenda ndio architecture wa hili kwa sababu wajuazo wao.