Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Mama anawachukulia poa hawa jamaa zetu kina Polepole, anawachukulia kidiplomasia hawa kina Ndugai. Ni mwanafunzi wa JK na atakuwa ni mshauri wake mkubwa japo ni wa kisiri.Ndugu zangu wa JF
Nitoe maoni yangu kama Mtanzania Mzalendo kufuatia kauli ya Ndugai kubeza kitendo cha Rais Samia kuendelea na Sera ya kukopa Fedha nje ya Nchi kugharamia miradi ya Maendeleo
Kauli ya Mheshimiwa Ndugai sio tu inabeza na kudharau mamlaka ya Rais bali inalenga kuhujumu jitihada za makusudi za Rais Samia kukamilisha miradi mikubwa ya maendeleo inayohitaji Fedha nyingi sana kuikamilisha
Mheshimiwa Ndugai akiwa Kiongozi wa Bunge ameshindwa kuonyesha uwajibikaji wa pamoja wa kidola na ameamua kwa makusudi kutumia nafasi yake vibaya kwa maslahi binafsi
Ieleweke Rais Samia anakopa fedha kwa maslahi ya Nchi yetu na amekuwa muwazi kwenye suala hili
Ieleweke kuwa Fedha za Tozo haziwezi kugharamia miradi yote mikubwa ya kimkakati na haiwezi kuwa mbadala wa kukopa Fedha
Mheshimiwa Ndugai angeliweza kuomba kuonana na Rais Samia na kumshauri aonavyo badala ya njia aliyoitumia ya kuropoka HADHARANI!
Kwa maoni yangu kauli ya Mheshimiwa Ndugai likusudia kukwamisha juhudi za Rais wetu kukamilisha miradi mbalimbali ya Maendeleo kama ilivyoelekezwa kwenye Ilani ya CCM
Nashauri Mheshimiwa JOB NDUGAI ajiuzulu mara moja wadhifa wake wa Uspika na akishindwa kufanya hivyo mamlaka husika zimchukulie hatua za kumvua uanachama wa CCM kwani kwa sasa sio Mwenzetu tena
Tumpe ushirikiano Rais Samia
KaziIendelee
JK anazijua sana hizi fitina, ni mtu anayeamini katika busara ya kuupa muda nafasi ili uamue. Ni kama vile Bashiru alivyowatukana wapumbavu wazee wa CCM halafu alipokufa bosi kila kitu kikaharibika. Akapewa ubunge wa viti maalum kwa kumlindia tu heshima yake.