Nashauri tubadili jina la nchi na tuitwe Kilimanjaro, badala ya Tanzania

Nashauri tubadili jina la nchi na tuitwe Kilimanjaro, badala ya Tanzania

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,850
Reaction score
6,030
Nimesafiri na kuishi nchi mbalimbali duniani, ila nchi yetu si maarufu sana, yaani Zanzibar na Mountain Kilimanjaro ndio watu wanavijua, Tanzania hawaijui.

Nahisi makosa yalifanyika katika kulichagua jina la nchi enzi hizo, japo nasikia toka awali huko ilishapendekezwa nchi iitwe Kilimanjaro, sema labda bado ukanda wa kule ungeonekana kupendelewa.

Kilimanjaro ni jina zuri, na linajulikana, kuliko Tanzania, hata mdomoni ni tamu, inaweza kuwakilisha jina la nchi vizuri, ikatusaidia kuongeza watalii, na pia itasababisha Kenya waache kusingizia mlima ni wao.

Chonde chonde, huko majuu watu hawaijui Tanzania, jina la nchi ila si zuri sana, naogopa labda navunja sheria kwa kusema hivi ili najaribu kuwakilisha mawazo yangu.

Hata Serengeti sio baya ni zuri kuliko lililopo, mbona wenzetu Zanzibar nchi yao ni maarufu kwa maana hata jina tu ni tamu jamani.

I love my country Kilimanjaro/Serengeti, nadhani hili litaenda sambamba na katiba mpya huko mbeleni.
 
I love my Country Kilimanjaro/Serengeti, nadhani hili litaenda sambamba na katiba mpya huko mbeleni

Mkuu naona unajikanyaga sasa. Tanzania unasema haifahamiki, hapo chini ukesema "mbona wenzetu Zanzibar nchi yao ni maarufu kwa maana hata jina tu ni tamu jamani".Sasa najiuliza kama umekubali Zanzibar ni nchi hiki unachotaka kiitwe Kilimanjaro/Serengeti ni Tanzania yote au ni Tanzania bara a.k.a Tanganyika? Ukumbuke tu kuiita Tanzania yote Kilimanjaro wazanzibari hawata kuacha salama kabisa na waliokuwa na allergy na Kilimanjaro sijui watakufanya nini. Tafadhali fafanua.
 
Ni jina tu, vingine vyote vinabaki kama vilivyo
 
Mtazaomo mzuri..
Inawezekana na ishatokea japo itahitaji process ndefu...
Congo, Mynmar, burkina faso, benini, Swizland n.k wote walifanikiwa ktk hilo
 
Swali langu ni jina badala ya Tanzania au badala ya Tanzania bara a.k.a Tanganyika?
Km zanzibar itabaki km ilivyo..
Inabidi iwe badala ya tanganyika(duu ila hili jina nalooo, yani sisi hata majina ya ajabu ajabu....)
Lkn tukumbuke sasa hapa tutakua tumeua jina la muungano.......
 
Huna point ya hata ya kutu-convince kufikiria kufanya hivyo
Zunguka nchi za nje ndo utanielewa, nilikaa na jamaa wa pakistani akaniambia unatoka wapi, nikasema tanzania africa, akaguna nikakolezea east africa, nilivosema east africa akadakia is it close to ethiopia, dah nikachoka kabisa
 
Km zanzibar itabaki km ilivyo..
Inabidi iwe badala ya tanganyika(duu ila hili jina nalooo, yani sisi hata majina ya ajabu ajabu....)
Lkn tukumbuke sasa hapa tutakua tumeua jina la muungano.......
Huko nyuma tulianza na Jamhuri ya Muungano ya Tanganyika na Zanzibar. Tukianzia hapo basi tunaweza kwenda Jamhuri ya Muungano wa Kilimandjaro na Zanzibar. Serngeti iko neutral zaidi lakini Kilimandjaro inapendeza na inafahamika zaidi. Na ule mwenge wetu na bendera vilisimikwa huko. Tanganyika ni kurudi nyuma ingawa ni better kuliko huu unafiki wa Tanzania Bara.
 
Zunguka nchi za nje ndo utanielewa, nilikaa na jamaa wa pakistani akaniambia unatoka wapi, nikasema tanzania africa, akaguna nikakolezea east africa, nilivosema east africa akadakia is it close to ethiopia, dah nikachoka kabisa
Nimekaa nchi za nje nusu ya Maisha yangu. Ila hoja yako sikubaliani nayo kwa kuwa Kilimanjaro inapata umaarufu kwa sababu ya mlima sasa unataka kila nchi ipewe jina kutokana na umaarufu wa vitu?mfano Egypt tuiite Pyramid South Africa tuiite Table Mountain na Kenya tuiite Maasai Mara? Kuna jina la nchi na vitu nchi itabaki kuwa nchi na vitu vitabaki na majina yake
 
Kwahiyo nchi zote maarufu zimekua maarufu coz majina yake ni matamu kama unavyodai? umaarufu unatengenezwa kwa vitendo na sio jina,vitendo ndio vinatengeneza jina/Brand,

Mfano Brazil ni maarufu kutokana na usakataji wao wa Football sio eti coz jina Brazil ni tamu!
 
Tanzania jina zuri pia maana ukisema uite kilimanjaro utaonekana kama watu wakaskazini unawapa upendeleo ila nchi ya Tanzania kwa Sasa ni maarufu sana tokea aingiie jiwe imeweka headlines kwenye television zakitaifa mfano CNN BBC aljazeera so we should stick with Tanzania
 
Mangi buana[emoji28][emoji28]... Janja janja nyingi sana nyie ndo mana mkiingia ikulu mtataka makao makuu yaende marangu.
 
Back
Top Bottom