Nashauri tubadili jina la nchi na tuitwe Kilimanjaro, badala ya Tanzania

Nashauri tubadili jina la nchi na tuitwe Kilimanjaro, badala ya Tanzania

Louis II, Kuna movie ya James Bond imetengenezwa mwaka 1969 niliona anaitaja Nairobi nikasema hawa wajomba walianza kujulikana kitambo sana.
 
Inawezekana ukawa kijana kimwili,lakini kikongwe akilini
 
Zunguka nchi za nje ndo utanielewa, nilikaa na jamaa wa pakistani akaniambia unatoka wapi, nikasema tanzania africa, akaguna nikakolezea east africa, nilivosema east africa akadakia is it close to ethiopia, dah nikachoka kabisa
Alafu hao wasioijua Tanzania ni wale wananchi wa kawaida sana but watu wasomi na viongozi wakubwa huko huko kwa wakoloni wanaifaham sana ma ndiyo maana hata media zote kubwa duniani hazijawahi kukosea kwa kuandika au kutamka...

Eti "...Rais wa Tanganyika, Tasmania au nchi iliyopo karibu na Ethiopia ..."

Kaonane na viongozi hawa Shevshenko au Itlamandar waulize kuhusu Tanzania.
 
Je, na Tanzanite siyo maarufu kweli huko duniani? Kama ndivyo, basi na Kilimanjaro iwe Mombasa; "a equation balanced".
 
Louis II,

Mkuu kama hatujulikani inamaana hawa watalii tunaopokea kila mwaka huwa hawajui wanakoenda? Halafu Kutofahamika si aibu. Hata ww humu JF watu hawakufahamu ww ni nani. Tena ingekuwa vizuri ukiulizwa unakotoka usitaje nchi utaje kijiji, wakiuliza ni wapi taja wilaya, wakiuliza waambie mkoa halafu wakiuliza ndo waambie nchi halafu uwape na notes za huku tuna nini ili wasiulize ulize tena na wawape wenzao waje kutalii. Halafu bombadier zitasaidia pia kufahamika, mzipromote.
 
ubarinolutu, Mnaanzaga taratibu hivyo hivyo kutafuta jinsi ya kuharibu historia ya nchi hii ili kumtukuza mtu.. hapo shida si jina Tanzania Wala si kuwa mnamapenzi sana na jina kilimanjaro maana mngeweza kuhamisha pia mngejaribu..... Ila ukweli ni kuwa mwataka mtu fulani aonekane enzi yake aliweza badili jina la nchi kama Congo Mobutu(Zaire)&Kabila Senior(DRC) Rhodesia(Zimbabwe) Upper Volta (Bukinafaso)
Ni wakati wenu huu na nchi ni maliyenu hata mkiamua kuiita Jamuhuri ya Kajidemokrasia ka Chato ni sawa tu.. hatutakuwa na uwezo wa kuwazuia.
 
Kama ni kujulikana tu,nchi iliyokuwa inakubalika ni TANGANYIKA.Tanzania imekuja baada ya muungano.
Nadhan kule kutangatanga ndo kumeleteleza haya yote.
Laiti ingebaki tanganyika
 
Sioni sababu yenye mashiko kufanya maamuzi haya kubadili Jina zuri na Tamu lenye ladha ya Nchi yenye matumaini makuu Siku Za baadae.
 
Ukishaijua kilimanjaro na Zanzibar utatafuta muelekeo na kuijua Tanzania
 
Itakuwa marufu polepole usiwe na haraka kama cha kwanza,

Ndo maana saivi kuna mondi, samatta, wanaanza kujulikana duniani na hivyo hivyo Tanzania inajulikana
 
 
Wazungu wanatutesa sana.

Enzi za JK waziri wa mambo ya nje Membe alisema uwanja wa ndege pale dar umebadilishwa kutoka JKIA to JNIA sababu lile neno Kambarage wazungu wanashindwa kulitamka,daah nilitafakari nikasema tu hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
Mh! Mbona Nyerere ndiyo jina linawapa taabu sana kulitamka.
 
Back
Top Bottom