Nashauri tubadili jina la nchi na tuitwe Kilimanjaro, badala ya Tanzania

Nashauri tubadili jina la nchi na tuitwe Kilimanjaro, badala ya Tanzania

Zunguka nchi za nje ndo utanielewa, nilikaa na jamaa wa pakistani akaniambia unatoka wapi, nikasema tanzania africa, akaguna nikakolezea east africa, nilivosema east africa akadakia is it close to ethiopia, dah nikachoka kabisa
Ungesema iko pembeni ya Kenya. Maana ukisema tu iko next to Kenya na kwa vile Kenya inajulikana basi wanakuelewa mko pande zipi za Africa. Sisi tunako feli ni kwenye kujitangaza. Kenya is far far ahead of us.
 
Uhamiaji desk; Umetokea Tanzania?
Msafiri; Ndio bwana, baba yangu alikuwa
mwalimu wa kiingereza kule
Zanzibari.

Niliiona hii katika movie moja hivi ya mwaka 2018 sikumbuki jina.
 
Mnaposema Tanzania haijulikani huko nje mnataka kusemaje, hawa watalii wanaomiminika kila uchwao kuingia wanaandika taarifa gani huko watokako..?

Sababu sio tu jina gumu kutamkika, tangazeni nchi yenu kimataifa kwa kufanya vitu muhimu mtajulikana tu.... hivyo ‘vivutio’ vya asili vimesaidia hadi hapo sasa sio vema kuishia hapo.

Umenikumbusha hii ya kuwaita watoto wetu eti ‘majina mazuri’ yanayotamkwa vizuri, kwani jina ni kitu gani zaidi ya utambulisho tu.... wazo lako halina sababu yenye mashiko.
 
Ili nchi ijulikane lazima iwe ina umaarufu furan kma utajiri, nguvu za kijeshi, wagunduzi wa technologia, na vingne vingi
Kwa africa mashariki kenya n maarufu kuliko tanzania... Kutokana na kunyakua medali za kidunia katka michezo ya marathon olymbiki, na sababu nyingine

Kwa hyo mnaoshangaa serikali kununua ndege akili kumkichwa...
Watu hawawez kuijua kama tunaishi kama kijiji lazma tuwe na international standard.. Asa nchi ata ndege moja hamna.. Nani aijue? Haina hata international media
Ukiangalia mfano china.. Tangu kuanza kukua kwa kasi kumeifanya ifungue cgtn ambayo inapatikana dunia nzima ivi leo n nani asiijue?
Qatar kiinchi kidogo lakin kinajulikana na nchi zote dunian... Kwa influence ya aljazeera

Ni sawa tu hapa tanzania wengi wanamjua diamond n alikiba had wazee kwann wanafanya mambo makubwa sana!!

Heshima ya nchi ndyo inayofanya nchi iheshimike
Na nchi inaheshimika kwa mambo makubwa!!
Ndo biadam tulivoumbwa kuheshimu vitu vilivyo extra ordinary na vikubwa mfano tembo, simba, nguvu, ujasiri hamna ataeheshimu sisimizi, au udhaifu
 
Back
Top Bottom