GE2025 Nashauri viongozi waache kusema watu walioko nje ya nchi ndio wanachochea ya ndani. Kana kwamba huku ndani mambo ni shwari

GE2025 Nashauri viongozi waache kusema watu walioko nje ya nchi ndio wanachochea ya ndani. Kana kwamba huku ndani mambo ni shwari

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Hamjambo!

Nimemsikia viongozi kadhaa wakisema na kulaumu watu walioko nje kama kina Mange Kimambi na wengineo wao ndio wanachochea vurugu na amani ndani ya nchi. Kauli hiyo inatolewa ni kana kwamba huku ndani watu wako sawa na hakuna tatizo.

Kauli kama hizo zinatufanya tukimbie ukweli na uhalisia na matokeo yake kuchukua hatua stahiki kwa yanayoendelea.

Pakiwa na ufa ambao hauzibwi ndani ya nyumba ufa huohuo ndio hutumika kuingiza mijusi, ng'e, panya, nyoka na hata wadudu wasiodhuru.

Ni muhimu kuziba ufa ili kuepuka kujenga ukuta na kuzuia wadudu hatari kuingia ndani ya nyuma.

Lakini kutokuziba ufa na kuishia kulalamika kwa nini wadudu wanaingia kw kweli hiyo sio suluhisho.

Wakati huu wakati nchi inaendelea na mambo mengine ya maendeleo ni muhimu wawepo watu maalum wenye ujuzi na maarifa wasioendeshwa na mihemko ili kuziba ufa tulionao.

Ufa huu hautazibwa na machawa, ufa huu hautazibwa na walioumizwa na wenye visasi, ufa huu hautazibwa na walioumiza, kutesa, kuteka na kuua watu. Ufa huu hautazibwa na viongozi wa dini machawa walioshindwa kuwa wakweli, jasiri wa kusema nyeupe ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi.

Ufa huu hautazibwa na watu wenye maslahi ya Kisiasa kwa vyama vya kisiasa.
Ufa huu utazibwa na kundi moja tuu. Naam WATIBELI.

Watu ambao ukweli kwao ni ukweli hata kama hauna maslahi na unawaumiza hata wao.

Watu ambao wanapenda haki sio zao tuu hata haki za maadui zao kumaanisha hataonewa mtu.

Watu ambao wana upendo kwa watu wote hata wale wanaowaudhi.

Watu ambao wanapenda maarifa na ufahamu kwa sababu wanamcha Mungu.

Watu ambao hawataki kuwa upande wa yeyote zaidi wanataka upatanishi na liwepo kundi moja ndani ya familia za watu na taifa kwa ujumla.

Ndugu zangu, kila mtu anatamani kufurahi. Kila mtu anahitaji kuhisi heshima. Kila mtu anashauku ya tuishi duniani kama hadithi za peponi.

Sisi watibeli tunaamini na kujua Pepo ya mwanadamu ipo Duniani hapahapa. Na atakayeileta hiyo pepo ni sisi wenyewe wanadamu.
Ikiwa tutakuwa na UPENDO, HAKI, UKWELI NA AKILI/MAARIFA.

Mungu awabariki

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Viongozi wanasahau mtaani kumejaa graduates wa vyuo vikuu sio kama miaka ile wasomi walikuwa wenyewe tu
 
9 December 2025 Kuna party tutakula na kunywa Kila mmoja na kikombe chake.
 
Warioba alionya sana tunapoelekea lakini alipuuzwa, wakadhani kizazi hiki nisawa na kile cha miaka 40 iliyopita.
 
Kwa mfano huyu bwana mdogo hapa mama yake kapigwa risasi akiwa mlangoni nyumbani kwao.

Unafikiri huyu kijana serikali na familia ya Samia ataichukuliaje miaka 20 mbele?

Mimi hadi sasa nimeelewa kwanini rebels hutokea.

Pale mtu anapokosa haki katika vyombo vyote vya kisheria ambavyo vimetekwa na mafisadi na vibaka wachache ndio rebela hutokea.

Tusidanganyane hakuna kiasi chochote cha pesa au maridhiano yatafuta kumbukumbu la tukio hili kwa huyu kijana na ndugu zake kuhusu utawala wa Samia.


View: https://x.com/mangekimambi/status/1985782281261449293?t=uav7Qjn-zdTsBOTjROlsrQ&s=19
 
Mbinu lazima zibadilike.

Mpaka kazi ya bodaboda nayo iko full
Hawajui tunawafundisha mambo makubwa Hadi wadogo zetu na wajomba zetu huwa nakaa standby kuwaambia kinaachoonyeshwe kwenye taarifa ya habari huu ni uongo na huu ni robo ya ukweli
 
Back
Top Bottom