Kama wataweza kufunika mapengo yote watapiga hela sana! Ipo hivi kutafsiri kunamapana yake humohumo na ubunifu n.k Kuna swala la usikikaji wa sauti na muonekano wa picha pia,watafsiri wengi wamekuwa wakiharibu ubora wa picha na sauti na unakuta anachotafsiri ni uongo mtupu japo si wote.
Kama watatokea wenye kuziba mapungufu basi wataheshimisha kazi husika!, let's say mtafsiri anatoka na ubunifu huu mfano kwenye muvi anaonekana mtu anatumia bunduki Aina ya AK47 hapa mtafsiri anaweza akaweka pozi movie kidogo halafu kwa maelezo mafupi na yaliyoshiba anaweza akaielezea aina hiyo ya bunduki na uwezo wake na hata ikibidi ka historia kidogo! Hii inakuwa ni burudani na pia sehemu ya elimu. Yapo mengi wanaweza kuyafanya na Kama mtu anaweza basi awe specific kwenye aina fulani ya muvi labda za kipelelezi anakuwa anatumia muda mwingi kuziangalia kuzifatilia na kujua kwanini hapa palitumika mbinu hii au kwanini hapa palifanywa hivi n.k
Movie sometimes hazina maelezo zinahitaji uelewa Sasa waangaliaji wengi Kuna vitu huwa vinawapita kwa maana wao huwa wanaangalia tu hawana la kujiuliza!.. so no vyema wawameng'enyee wateja wao ili wazipende kazi zao. Muvi nyengine mtu hawezi zipenda kwasababu hajajua undani wake ila akijua basi humnyang'anyi remote!.
Huo ndo mchango wangu.