vibertz
JF-Expert Member
- Mar 15, 2022
- 2,474
- 4,726
Kuna sakata kama tatu zimejitokeza kuhusu mikataba, Morrison, Fei toto, na sasa ni sportpesa. Sitaki kuchimbua sana lakini ukiangalia kwa umakini unaona kabisa mtu anayesimama kwenye kusainiana mikataba ni mtu asiye na maono, asiyekuwa na uwezo wa kufikiria na asiyejua kusimamia mikataba yenye maslahi ya klabu.
Hapa natoa mifano miwili ya makosa niliyoyaona
1) Ishu ya Feisali, ni kosa kubwa sana kuweka wazi kipengele cha kuweka kiasi fulani cha pesa ili kujinasua na kifungo cha mkataba. Kuvunja mkataba kupo ila ikifikia upande mmoja unataka kuuvunja basi ni swala la kuwekana mezani na kufikiana muafaka kuwa toa kiasi kadhaa ili uwe huru na sio kutanabaisha kwa maandishi wazi wazi.
Pesa unayoiona leo nyingi kesho utaiona ndogo. Huyu mwanasheria hana maono ya mbali na hafatilii hata mikataba ya timu za ulaya wanawezaje kulinda maslahi ya klabu.
2) Ishu ya pili ni hili la sportpesa
Unapoingia mkataba na mdhamini mkuu, lazima muweke vipengele vyote na lazima ujue vipengele vikae sawa kulingana na mashindano ambayo timu inaenda kushiriki.
Inatambulika kabisa kuwa sportpesa ni kampuni ya kamari na huwa haziruhusiwi kampuni za kamari kuwepo kwenye jezi pindi timu ikifuzu hatua ya makundi kwenye mashindano ya interclub. Lazima kuwekana sawa na mdhamini mkuu kuhusu ukomo wao au nini kitakachoweza kufanyika endapo timu itafuzu hatua hiyo na kila kitu kuanishwa katika mkataba husika.
Kinachoendelea kwasasa ni either mkataba una mapungufu au pengine Yanga wamekiuka masharti ya mkataba lakini kwa hayo yote wa kwanza kuwajibika ni mtu wa sheria wa timu kwa kushindwa kuuelewa/kuufata mkataba ama kushindwa kuufanya mkataba ueleze kila kitu ili kulinda maslahi ya klabu.
Ni wakati sasa, uongozi wa Yanga kutafuta mwasheria anayejielewa mwenye akili ya kuchanganua mambo, upeo mkubwa na pia mwenye maono ya mbali ili aweze kusimamia vyema maslahi ya timu.
Huyu mwanasheria wa sasa ni mweupe sana kichwani, anakula mshahara wa bure.