Nashindwa kuelewa, hapa kuna upendo kweli au napotezewa muda?

Achana nae tuu wanaume wamaana wamejaa jf ushindwe mwenyewe tuu
 
Binadamu bwana mnazitafuta stress wenyewe🤣🤣🤣 wacha mpigwe tuu
 
Ushauri wangu we mgande huyo huyo tena anzisha utaratibu wa kwenda huko mkoani kwake kila weekend kumsalimia na kukaa nae mpaka jumatatu.

Kwa sasa hivi wanaume wamebaki wachache sana na pisi kali ni nyingi mno mitaani kwahiyo uwezekano wa kupata mwanaume wa maana ni mdogo. Komaa hapo hapo
 
Sasa si anataka ushauri kila mtu na mawazo yake hayo ndio yangu 😆😆
Mkuu mimi nimesoma "between ze lines" kwenye post ya huyu dada nimegundua yafuatayo;
1. Ana miaka zaidi ya 30 (anajiita Mama ndege. Hakuna binti wa 20's anajiita mama fulani)
2. Yuko na mwanaume aliemzidi 15 years. Hii inamaanisha:
a) Yuko nae ki maslahi (hakuna mapenzi)
b) Dada yetu soko lake gumu (kwa umri huo hana mtu/mahusiano)

Nahisi hata huyo jamaa anamchukulia huyu dada kama kipoozeo tu wakati akihitaji huduma achape esepe zake, sema dada yetu ndio anataka mambo mengi.

Ndio maana nimemshauri dada yetu yeye akomae hapo hapo maana hana jinsi. Competition imekua kali sana kwa sasa.
 
Unatarajia hapa utasaidiwa unachotaka? Hapa utatongozwa upya,utapewa maneno na watu waliokata tamaa ya mahusiano ya kukukatisha na wewe,wengine watakushauri vizuri lakini kwa maoni yao, ushauri mzuri uko kwenye sauti yako ya ndani maana sauti ya ndani ndiyo MUNGU huwa anaongea na mtu,siku nyingine mambo kama haya jitafakarishe wewe mwenyewe.
 
Asante mkuu
 
Mh! Hapo ndiyo atazidi kunishusha thamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…