Nashindwa kuelewa, hapa kuna upendo kweli au napotezewa muda?

kiss ov love

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2025
Posts
9,388
Reaction score
16,188
NRNE
Habari za muda mrefu wana jukwaa, mimi msichana, niko kwenye mahusiano na mwanaume amenizidi miaka 15, yeye ana mtoto mmoja mimi sina.

Mimi nipo Dar, yeye yupo mkoani, tulipoanza mahusiano nilijua kwakuwa ni mtu mzima pengine, tutaenda sawa kwani na mimi huwa sipendi mambo ya hovyo. Lakini pia nilijua anaweza kuwa amechoka kukaa mwenyewe hivyo atanioa haraka tu (lakini hii haikuwa dhamira yangu kubwa)

Sasa kuna vitu huwa vinanikosesha amani mno, kwanza huyu mwenzangu unaweza ukaongea tu kitu cha tofauti kinaweza kuwa kidogo tu lakini atakishikilia na kukufanya ujione umekosea sana, hapo utaanza kuomba na misamaha ya kutosha. Lakini yeye ikitokea amekosea atalipindisha hilo kosa hadi lisionekane kama ni kosa.

Kama wiki kadhaa zimepita aliniambia ameenda kwao kusalimia, wakati yupo njiani tulikuwa tunawasiliana hadi anafika, sasa kama siku mbili mbele akaniambia ile siku ameenda alimpitia na mtoto wake ameenda naye, nikamuuliza mbona hukuniambia, akaniambia mambo mengi alipitiwa mh! Nikashangaa.

Wakati yupo huko huko akanipigia akaniambia yupo maeneo ya stendi, sasa sikusikia vizuri kumbe alisema kuna mzigo ameufuata nikamuuliza tena umesema umefata mzigo, akanijibu " hivi maswali yako unayoulizaga huwa unafikiriaga kweli" guys hii kauli iliniuma yaani ameniona mimi sina akili, nikamwambia haya baadae, nikakata simu nikatafakari kama siku tatu nikampigia maana na yeye alinikaushia, hakupokea simu, ila huku status whatsapp anapost, hizi si ni dharau jamani. Na yeye kakaa kama siku mbili tatu hivi akanitumia msg whatsapp " habari yako" na mimi sikuijibu ile siku nijibu "salama" after two days, akajibu kwa kureact akakausha, leo naona kanicheki normal, mimi nikampigia hajapokea.

Nashindwa kuelewa ni upendo gani huo wa kumkasirikia mpenzi wako, kwa vitu vidogo vidogo ambavyo mnaweza kueleweshana tu, wakati mwingine unaweza kukuta usiku ikatokea mmegombana hivi ukimpigia ili muongee muyamalize hapokei kabisa ila msg anajibu anasema hajisikii kuongea, hatakagi suluhisho, sasa najiuliza kama huku mwanzoni yupo hivi je ikitokea tukaingia kwenye ndoa huko si ndo atakuwa akikasirika na matumizi anasusa kutoa kabisa🤕

I'm not perfect, hata mimi nina madhaifu na mapungufu yangu, lakini huwa nina amini kwenye kurekebishana ila mwenzangu naona hilo swala hataki kabisa, niliplay part yangu vya kutosha kujishusha nimejishusha sana misamaha nimeomba mingi mno ila kwa sasa moyo umechoka kuvumilia haya mambo, maisha yanipe stress bado na mapenzi tena yanipe stress si nitajifia na presha.

Naombeni ushauri wenu, wakubwa zangu.
 
anakutafutia sababu achana nae njoo inbox
 
Yupo Mkoa tofauti na anaoishi yeye na huyo mtoto wao, na anaishi na mwanaume mwengine kwa maelezo ya huyu mwenzangu
nna experience na single faza mmoja,,yupo ivo ivo pia inatokana na aloyapitia kwa mama mtoto wake,kama alimuumiza sana basi moyo wake haupo sana katika mapenzi ila ni vile basi tu,pia fatilia ujue kuhusu uyo baby mama wake labda bado wanawasiliana vizuri kabisa........ aaah nashindwa hata nkwambie nini maana yalonikuta kwa huyo kiumbe na baby mama wake sina hamuuuu🙌🏾

Mama double 2 njoo saidia kwanza m bado npo kwenye majonzi
 
Kwenye mahusiano ya siku hizi uwe ke au me, jitahidi sana usiwe namba mbili.

Eidha we ndo uwe unayaongoza au basi msipishane sana kwenye kutoa maamuzi.
Wewe ukiwa ndio muomba misamaha kila siku, utahenya.

Na kingine wanawake jitahudini muwe na vipato.
 
Back
Top Bottom