Nashindwa kuelewa, hapa kuna upendo kweli au napotezewa muda?

Nashindwa kuelewa, hapa kuna upendo kweli au napotezewa muda?

NRNE
Habari za muda mrefu wana jukwaa, mimi msichana, niko kwenye mahusiano na mwanaume amenizidi miaka 15, yeye ana mtoto mmoja mimi sina.

Mimi nipo Dar, yeye yupo mkoani, tulipoanza mahusiano nilijua kwakuwa ni mtu mzima pengine, tutaenda sawa kwani na mimi huwa sipendi mambo ya hovyo. Lakini pia nilijua anaweza kuwa amechoka kukaa mwenyewe hivyo atanioa haraka tu (lakini hii haikuwa dhamira yangu kubwa)

Sasa kuna vitu huwa vinanikosesha amani mno, kwanza huyu mwenzangu unaweza ukaongea tu kitu cha tofauti kinaweza kuwa kidogo tu lakini atakishikilia na kukufanya ujione umekosea sana, hapo utaanza kuomba na misamaha ya kutosha. Lakini yeye ikitokea amekosea atalipindisha hilo kosa hadi lisionekane kama ni kosa.

Kama wiki kadhaa zimepita aliniambia ameenda kwao kusalimia, wakati yupo njiani tulikuwa tunawasiliana hadi anafika, sasa kama siku mbili mbele akaniambia ile siku ameenda alimpitia na mtoto wake ameenda naye, nikamuuliza mbona hukuniambia, akaniambia mambo mengi alipitiwa mh! Nikashangaa.

Wakati yupo huko huko akanipigia akaniambia yupo maeneo ya stendi, sasa sikusikia vizuri kumbe alisema kuna mzigo ameufuata nikamuuliza tena umesema umefata mzigo, akanijibu " hivi maswali yako unayoulizaga huwa unafikiriaga kweli" guys hii kauli iliniuma yaani ameniona mimi sina akili, nikamwambia haya baadae, nikakata simu nikatafakari kama siku tatu nikampigia maana na yeye alinikaushia, hakupokea simu, ila huku status whatsapp anapost, hizi si ni dharau jamani. Na yeye kakaa kama siku mbili tatu hivi akanitumia msg whatsapp " habari yako" na mimi sikuijibu ile siku nijibu "salama" after two days, akajibu kwa kureact akakausha, leo naona kanicheki normal, mimi nikampigia hajapokea.

Nashindwa kuelewa ni upendo gani huo wa kumkasirikia mpenzi wako, kwa vitu vidogo vidogo ambavyo mnaweza kueleweshana tu, wakati mwingine unaweza kukuta usiku ikatokea mmegombana hivi ukimpigia ili muongee muyamalize hapokei kabisa ila msg anajibu anasema hajisikii kuongea, hatakagi suluhisho, sasa najiuliza kama huku mwanzoni yupo hivi je ikitokea tukaingia kwenye ndoa huko si ndo atakuwa akikasirika na matumizi anasusa kutoa kabisa🤕

I'm not perfect, hata mimi nina madhaifu na mapungufu yangu, lakini huwa nina amini kwenye kurekebishana ila mwenzangu naona hilo swala hataki kabisa, niliplay part yangu vya kutosha kujishusha nimejishusha sana misamaha nimeomba mingi mno ila kwa sasa moyo umechoka kuvumilia haya mambo, maisha yanipe stress bado na mapenzi tena yanipe stress si nitajifia na presha.

Naombeni ushauri wenu, wakubwa zangu.
Hapo hakuna upendo kabisa tena itakuwa mwamba ana mwanamke ambae anampenda,kwako anakuja tu kama kujifurahisha,usipoteze muda hapo angalia mishe zako nyingine za kufanya.
 
nna experience na single faza mmoja,,yupo ivo ivo pia inatokana na aloyapitia kwa mama mtoto wake,kama alimuumiza sana basi moyo wake haupo sana katika mapenzi ila ni vile basi tu,pia fatilia ujue kuhusu uyo baby mama wake labda bado wanawasiliana vizuri kabisa........ aaah nashindwa hata nkwambie nini maana yalonikuta kwa huyo kiumbe na baby mama wake sina hamuuuu🙌🏾


Mama double 2 njoo saidia kwanza m bado npo kwenye majonzi
Najikuta lakusema sina ila hakunaga mapenzi ya hivo aangalie tu namna ingine ikibidi
 
Pole sana mkuu apo inavyoonesha tu huyo mwamba Hana plan na wewe hvo anakutafutia sababu tu ujae upepo Ili u react iwe mwisho kwenye mahusiano yenu ..Bora umuwahi mapema tu ku.move on muda bado unao tengeneza maisha yako kwanza mambo mengne baadae.usiwekee tegemeo kubwa Kwa mwanaume Kwa Dunia ya sasa ya 50%^50% mambo yamebadilika sana hata mwanamke unaweza kusimama pekee Yako na ukafanya mambo mengi tu ya kimaendeleo
 
Hapo hakuna upendo kabisa tena itakuwa mwamba ana mwanamke ambae anampenda,kwako anakuja tu kama kujifurahisha,usipoteze muda hapo angalia mishe zako nyingine za kufanya.
Mkuu tupo mbali mbali inaweza ikapita hata 3. Months hatujaonana kwanini anifanyie hivyo si aniache tu pengine naweza kupata mtu sahihi
 
Pole sana, inaelekea umeumizwa Sana in the past kiasi huoni mwingine au unadhani wote ni walewale tu. Mamii move on if he is the right one you will always be happy na hutakuwa na mashaka mashaka saa zote....
Ni kweli kabisa hapo nyuma nilipitia mahusiano magumu magumu tu, nilivyoanza na huyu nikaona ngoja tu nikomae naye nitakuwa mtu wa kuanza upya mpaka lini, na kuna mambo alikuwa ananionyesha sikuzingatia ila naona kabisa hayakuwa sawa na nadhani ningechukuwa hatua tusingefika hapa leo, nimeamua kwa sasa hata kama ntaumia ila ntapona tu akinitafuta tena ntamwambia ukweli siwezi kukaa kwenye mahusiano yasiyonipa furaha.
 
Wanaume kwa sasa wapo wachache wanaokuambia piga chini wanakudanganya .

Jifunze kwa zuchu jinsi alivyomganda diamond hadi akaolewa .

Pia if I'm not mistaken upo late 20s so kwanini usivumilie zama hizi ndoa niyakukabia juu kwa juu .

Keep show up
 
Wanaume kwa sasa wapo wachache wanaokuambia piga chini wanakudanganya .

Jifunze kwa zuchu jinsi alivyomganda diamond hadi akaolewa .

Pia if I'm not mistaken upo late 20s so kwanini usivumilie zama hizi ndoa niyakukabia juu kwa juu .

Keep show up
Nashindwa kuvumilia maana furaha imekuwa ni mara chache sana kwenye haya mahusiano na siku hizi hata baadhi ya vitu amepunguza unaweza ukamwambia kitu akafanya nusu akasema atamalizia kesho ndiyo imetoka hiyo na unakuta ni jambo la muhimu
 
Back
Top Bottom