Nashindwa kuelewa, hapa kuna upendo kweli au napotezewa muda?

Nashindwa kuelewa, hapa kuna upendo kweli au napotezewa muda?

ushauri wako muhimu mkuu kumuepusha na depression
Ila kikubwa mapenzi ni mawasiliano na maelewano usipomtafuta lazma akutafute ila ukimute na yy anamute aah ukinuna ubembelezwi unanuniwa zaidi,usiendelee kuwa mtumwa wa mapenzi hali ya kuwa ni ngumu kukubali ukweli ila ikibidi pita hvii
Najikuta lakusema sina ila hakunaga mapenzi ya hivo aangalie tu namna ingine ikibidi
 
Kwa mujibu wa sensa wanaume ni wengi sana,
Tafuta mwanaume atakaekufaa taratibu,
Usiendeshwe na swala ndoa ama umri kwenda,
Huyo jamaa ACHANA NAE, ukiamua kuendelea nae ni juu yako
 
Yaani story yako kama yangu na hii hali naichukia sana kwanini napata single father tu sipatagi fresh na nikipata fresh anakuwa kibentenii na mimi siwatakii

Mpk imefaya ni relate Hii issue nikiwa Advance tulikuwa tunapiga story nikasema sitokuja kuolewa na mwanaume mwenye mtoto kuna roommate akadakia akasema tena wewe utakuwa mama wa kambo tena wa watoto wawili 😭😭

Nahisi kama aliniroga yule binti jamani seriously sijawahi kupata mahusiano strong kwa vijana fresh napataga kwa hawa single faza sema nao wazinguajii 😃
 
Kupata ndoa siyo kufanikiwa unaweza kuipata na ukanyanyasika humo ndani, kama mapicha picha yanaanza mapema hivi huko ndani itakuwaje, hapana sitaweza kuvumilia manyanyaso
Kwa wanawake wa kiswahili most of them mna -chase ndoa ili mpate life security kulipwa bills zenu Kama Chakula. Mavazi , n.k

Hata unalalamika Ila huyo jamaa anagekuwa anakuhudumia to the fullest kuanzia chakula ,mavazi na kukupa pocket money yakutosha sifikirii Kama ungelalamika.

Wanawake wakiswahili mpo selfish Sana .

Ungekuwa upo na huyo mwanaume with no interest he could never push you away

(Asingekuwa anakuweka mbali)

Mimi mwenyewe niliachana na Kuku wa kienyeji baada ya kujua they have nothing to offer in my life than pussy .
 
Lazima u-Apply mbinu mbali mbali ili kufanikisha lengo Fulani.

Jifunzeni kwa zuchu
Sawa labda hatuzijui mbinu ndio utuambie hapa

Ila Zuchu wapo karibu na Diamond tofauti na sisi..
na ukisema tuwe karibu maana ake tuache kazi tuwafate mikoa yao walipo kitu ambacho hakiwezekani of
 
Yaani story yako kama yangu na hii hali naichukia sana kwanini napata single father tu sipatagi fresh na nikipata fresh anakuwa kibentenii na mimi siwatakii

Mpk imefaya ni relate Hii issue nikiwa Advance tulikuwa tunapiga story nikasema sitokuja kuolewa na mwanaume mwenye mtoto kuna roommate akadakia akasema tena wewe utakuwa mama wa kambo tena wa watoto wawili 😭😭

Nahisi kama aliniroga yule binti jamani seriously sijawahi kupata mahusiano strong kwa vijana fresh napataga kwa hawa single faza sema nao wazinguajii 😃
Single father wengi wanacheza na hisia za Kuku wa kienyeji kwakuwa Kuku wa kienyeji wao huwa hawafikirii maisha zaidi ya kuomba omba
 
yani hapo wa kuamua niwewe ndugu angu,kukaza au kulegeza,nimevumilia yote hayo unayopitia hadi sasa sielewi nikae upande gani
Pole sana mimi sitaweza kuvumilia kabisa
 
Mimi nishamua kuacha kama ilivyo akinitafuta nita respond ila sitokaa nimtafute mwisho wa siku nionekane desperate

Nimebakiza 4 years nifike 30 naamini ndani ya hiyo miaka nitapata wangu tu 🙄🙄
 
Mkuu tupo mbali mbali inaweza ikapita hata 3. Months hatujaonana kwanini anifanyie hivyo si aniache tu pengine naweza kupata mtu sahihi
Yaani unataka mpaka akuche yeye tena? Kwani wew hauwezi kujiongeza mkubwa?

Kitendo cha kumuona haeleweki hiyo tayar ni sababu ya kumuacha yeye.

Labda kama una mipaka yako tofauti na hiyo.
 
Hapa Tatizo ni Mwanamke, Mwanamke anaeshindana na Mwanaume ni ngumu sana kuendana na mwanaume yoyote aliesawa.
 
Huku ushauri hutaupata mzuri, watu wanakazania njoo PM.

Mimi nakushauri wewe ndo uwe dereva, take control ya mahusiano mwenyewe. Mf. Haya unayoeleza hapa, ungekaa nae ukamueleza, ukaona reaction yake. Hiyo ndo itakupa picha halisi unadate na mzee wa namna gani

Kuanzia apo unaamua, unapiga chini au unavumilia
 
Sawa labda hatuzijui mbinu ndio utuambie hapa

Ila Zuchu wapo karibu na Diamond tofauti na sisi..
na ukisema tuwe karibu maana ake tuache kazi tuwafate mikoa yao walipo kitu ambacho hakiwezekani of
Mkuu unajua watu wamekariri mbinu moja ya kupata jambo .

Mfumo wa kukabia juu kwa juu ndo mfumo bora wa kupata ndoa .

Kwakuwa people do change ukiachana na MTU kwakuwa hapokei simu au hajibu sms je utaachana na watu wangapi .
 
Single father wengi wanacheza na hisia za Kuku wa kienyeji kwakuwa Kuku wa kienyeji wao huwa hawafikirii maisha zaidi ya kuomba omba
Aisee sio kweli
Mimi hawa niao kuambia nimekutana nao sijawahi kuomba hela hata simuni labda waniombe wao

Na jambo zuri nina kazi na sina majukumu nakaa kwetu Silipi kodi pesa yangu nafanyia mambo yangu so sitegemei pesa ya mwanaume

Sema singo faza ni pasua kichwa
 
NRNE
Habari za muda mrefu wana jukwaa, mimi msichana, niko kwenye mahusiano na mwanaume amenizidi miaka 15, yeye ana mtoto mmoja mimi sina.

Mimi nipo Dar, yeye yupo mkoani, tulipoanza mahusiano nilijua kwakuwa ni mtu mzima pengine, tutaenda sawa kwani na mimi huwa sipendi mambo ya hovyo. Lakini pia nilijua anaweza kuwa amechoka kukaa mwenyewe hivyo atanioa haraka tu (lakini hii haikuwa dhamira yangu kubwa)

Sasa kuna vitu huwa vinanikosesha amani mno, kwanza huyu mwenzangu unaweza ukaongea tu kitu cha tofauti kinaweza kuwa kidogo tu lakini atakishikilia na kukufanya ujione umekosea sana, hapo utaanza kuomba na misamaha ya kutosha. Lakini yeye ikitokea amekosea atalipindisha hilo kosa hadi lisionekane kama ni kosa.

Kama wiki kadhaa zimepita aliniambia ameenda kwao kusalimia, wakati yupo njiani tulikuwa tunawasiliana hadi anafika, sasa kama siku mbili mbele akaniambia ile siku ameenda alimpitia na mtoto wake ameenda naye, nikamuuliza mbona hukuniambia, akaniambia mambo mengi alipitiwa mh! Nikashangaa.

Wakati yupo huko huko akanipigia akaniambia yupo maeneo ya stendi, sasa sikusikia vizuri kumbe alisema kuna mzigo ameufuata nikamuuliza tena umesema umefata mzigo, akanijibu " hivi maswali yako unayoulizaga huwa unafikiriaga kweli" guys hii kauli iliniuma yaani ameniona mimi sina akili, nikamwambia haya baadae, nikakata simu nikatafakari kama siku tatu nikampigia maana na yeye alinikaushia, hakupokea simu, ila huku status whatsapp anapost, hizi si ni dharau jamani. Na yeye kakaa kama siku mbili tatu hivi akanitumia msg whatsapp " habari yako" na mimi sikuijibu ile siku nijibu "salama" after two days, akajibu kwa kureact akakausha, leo naona kanicheki normal, mimi nikampigia hajapokea.

Nashindwa kuelewa ni upendo gani huo wa kumkasirikia mpenzi wako, kwa vitu vidogo vidogo ambavyo mnaweza kueleweshana tu, wakati mwingine unaweza kukuta usiku ikatokea mmegombana hivi ukimpigia ili muongee muyamalize hapokei kabisa ila msg anajibu anasema hajisikii kuongea, hatakagi suluhisho, sasa najiuliza kama huku mwanzoni yupo hivi je ikitokea tukaingia kwenye ndoa huko si ndo atakuwa akikasirika na matumizi anasusa kutoa kabisa🤕

I'm not perfect, hata mimi nina madhaifu na mapungufu yangu, lakini huwa nina amini kwenye kurekebishana ila mwenzangu naona hilo swala hataki kabisa, niliplay part yangu vya kutosha kujishusha nimejishusha sana misamaha nimeomba mingi mno ila kwa sasa moyo umechoka kuvumilia haya mambo, maisha yanipe stress bado na mapenzi tena yanipe stress si nitajifia na presha.

Naombeni ushauri wenu, wakubwa zangu.
Pole sana Mama Ndege hapo hakuna upendo wala nini yaani huyo Jamaa atakuharibia tu future yako na inaonekana wewe ndio unayejitoa sana kwake na umempenda kupitiliza na ndio maana unaumia.

Huyo jamaa yako ana mademu wengine ambako anaumia kihisia kama vile wewe unavyoumia kwake. Na akipigwa matukio ya kuumiza zaidi huwa anakuja kwako kukupetipeti na wewe kwa sababu umempenda kupitiliza huwa unampokea lakini baada ya muda anakuanzishia vitimbwi na kuanza kukusirikia.

La kukushauri Jipende sana mwenyewe, Kula vizuri, vaa vizuri na ufanye kazi zako kwa bidii. Acha kuhangaika na mtu anayekugeuza kama tambala la deki.

Hata kama huwa unamnunulia vizawadi kama kunogesha upendo Acha na usifanye hivyo. Usimpe nafasi mtu mwenye hizo tabia.
 
Mimi nishamua kuacha kama ilivyo akinitafuta nita respond ila sitokaa nimtafute mwisho wa siku nionekane desperate

Nimebakiza 4 years nifike 30 naamini ndani ya hiyo miaka nitapata wangu tu 🙄🙄
Hata mimi nataka nifanye hivyo akinitafuta niwe najibu tu normal, na hivi tuko mbali huku mimi naangalia zangu ustaarabu mwingine yeye aendelee kununa
 
Mkuu unajua watu wamekariri mbinu moja ya kupata jambo .

Mfumo wa kukabia juu kwa juu ndo mfumo bora wa kupata ndoa .

Kwakuwa people do change ukiachana na MTU kwakuwa hapokei simu au hajibu sms je utaachana na watu wangapi .
Hivi mfano unakutana na mtu nyie mnawasilianaga WhatsApp tu Hakuna normal calls wala sms ina maana usipokuwa na bando ndio hamuongei hivyo ukimuuliza why so anakwambia I hate calls

Mpnz wako kusikia sauti yake ni mpk mtake kuonana tena mpo mikoa tofauti

Ndugu yangu hapo nguvu ya kukabia kwa juu unaipata wapi
 
Back
Top Bottom