Nashindwa kuelewa, hapa kuna upendo kweli au napotezewa muda?

Nashindwa kuelewa, hapa kuna upendo kweli au napotezewa muda?

Mkuu wewe jitahidi kuacha negativity lazima una tatizo .

Hauwezi kuwa MTU mzuri then ukapata watu wabaya hiyo ngumu not only soulmate even friends
Kwaiyo nifanyaje sasa
Hebu niambie kitu nifanye yaani nianze Leo

Mapenzi yanatesa sana yaani mpk nimebaki mdogo mdogo sinenepi 😂
 
NRNE
Habari za muda mrefu wana jukwaa, mimi msichana, niko kwenye mahusiano na mwanaume amenizidi miaka 15, yeye ana mtoto mmoja mimi sina.

Mimi nipo Dar, yeye yupo mkoani, tulipoanza mahusiano nilijua kwakuwa ni mtu mzima pengine, tutaenda sawa kwani na mimi huwa sipendi mambo ya hovyo. Lakini pia nilijua anaweza kuwa amechoka kukaa mwenyewe hivyo atanioa haraka tu (lakini hii haikuwa dhamira yangu kubwa)

Sasa kuna vitu huwa vinanikosesha amani mno, kwanza huyu mwenzangu unaweza ukaongea tu kitu cha tofauti kinaweza kuwa kidogo tu lakini atakishikilia na kukufanya ujione umekosea sana, hapo utaanza kuomba na misamaha ya kutosha. Lakini yeye ikitokea amekosea atalipindisha hilo kosa hadi lisionekane kama ni kosa.

Kama wiki kadhaa zimepita aliniambia ameenda kwao kusalimia, wakati yupo njiani tulikuwa tunawasiliana hadi anafika, sasa kama siku mbili mbele akaniambia ile siku ameenda alimpitia na mtoto wake ameenda naye, nikamuuliza mbona hukuniambia, akaniambia mambo mengi alipitiwa mh! Nikashangaa.

Wakati yupo huko huko akanipigia akaniambia yupo maeneo ya stendi, sasa sikusikia vizuri kumbe alisema kuna mzigo ameufuata nikamuuliza tena umesema umefata mzigo, akanijibu " hivi maswali yako unayoulizaga huwa unafikiriaga kweli" guys hii kauli iliniuma yaani ameniona mimi sina akili, nikamwambia haya baadae, nikakata simu nikatafakari kama siku tatu nikampigia maana na yeye alinikaushia, hakupokea simu, ila huku status whatsapp anapost, hizi si ni dharau jamani. Na yeye kakaa kama siku mbili tatu hivi akanitumia msg whatsapp " habari yako" na mimi sikuijibu ile siku nijibu "salama" after two days, akajibu kwa kureact akakausha, leo naona kanicheki normal, mimi nikampigia hajapokea.

Nashindwa kuelewa ni upendo gani huo wa kumkasirikia mpenzi wako, kwa vitu vidogo vidogo ambavyo mnaweza kueleweshana tu, wakati mwingine unaweza kukuta usiku ikatokea mmegombana hivi ukimpigia ili muongee muyamalize hapokei kabisa ila msg anajibu anasema hajisikii kuongea, hatakagi suluhisho, sasa najiuliza kama huku mwanzoni yupo hivi je ikitokea tukaingia kwenye ndoa huko si ndo atakuwa akikasirika na matumizi anasusa kutoa kabisa🤕

I'm not perfect, hata mimi nina madhaifu na mapungufu yangu, lakini huwa nina amini kwenye kurekebishana ila mwenzangu naona hilo swala hataki kabisa, niliplay part yangu vya kutosha kujishusha nimejishusha sana misamaha nimeomba mingi mno ila kwa sasa moyo umechoka kuvumilia haya mambo, maisha yanipe stress bado na mapenzi tena yanipe stress si nitajifia na presha.

Naombeni ushauri wenu, wakubwa zangu.
Pole sana ungejaribu kuongea nae mueleze vile unakwazika na majibu yake lakini pia ujiulize huyo mkaka miaka yote hyo hajaoa shida ni nn labda anashindwana na watu sababu ya gubu lake.
 
Achana nae mrembo,,njoo kwangu mimi nimekuzidi miaka 10 na sina mambo ya kijinga. PM yangu iko wazi njoo huko tuanze maisha.

Umri:Nimekuzidi miaka 10
Kazi:Mjasiria mali
Status:Single sina mtoto
 
Mimi huyu kwenye mawasiliano hana shida shida mkikwazana ndiyo hivyo anakukalia kimya siku tatu hakutafuti, kuna siku nilimwambia hutaki tuongee yakaisha nikiamka asubuhi nimefariki je utajisikiaje?
Ndugu sitaki kuongea maana wanaume wa jf watanisimanga bure ila ila ila 🤨
 
Tena hapo kuna mengine tu sijayasema, nilikuwa navumilia nikaona atabadilika ila naona hakuna mabadiliko kabisa
Mwanaume mwenye upendo wa dhati hawezi kupitisha siku bila kukutafuta hii tabia ya kukasirika asili yetu ni sisi Wanawake ukiona Mwanaume ana tabia hizo ujue mkifunga ndoa atakuwa mara tatu yake.
 
Eeerr tatizo kubwa sana hilo!

Mi'naingiza ushauri wangu kwako kwa njia ya maswali!

Hivi kwa nini wazee wetu wa zamani, wale waliobuni mila pamoja na desturi za jamii, tena zenye kufanana takribani makabila yote kwamba: ' ni mwiko wachumba kukaribiana, kuishi pamoja na kufanya mapenzi kabla ya ndoa?

Kama unajua maana yake basi nijibu ili tujadili tu majibu ya swali hili pekee, maana mwisho wa mjadala lazima tutapata majibu ya moja kwa moja kuhusu 'mtanziko' wako!

Lakini kama hujui, basi nitatengeneza swali jengine usiloweza kuumiza sana kichwa:
Natumia mfano wa vijana watatu:
Wa kwanza kampenda msichana kwa dhati, kaenda nyumbani kwa wazazi wa msichana huyo na kuchumbia, kakubaliwa, kapangiwa kiasi cha gharama za mahari, hana pesa kaondoka kwenda kufanya kazi kwa ajili ya kuja kutoa mahari ili amuoe huyo mchumba wake.

Wa pili kampenda msichana kwa dhati, kisha kaenda kwa wazazi na kuomba aishi na mchumba wake akimtunza kisha akikamilisha mambo flani flani pamoja na kukamilisha mahari aliyopangiwa, atalipa mahari hiyo na watafunga ndoa.

Wa tatu, ni kijana kampenda msichana kwa dhati kisha akaenda kwa wazazi kujitambulisha, kapangiwa kiasi cha mahari, lakini uchumi wake hohe hahe hana hizo pesa, kaamua kumrubuni huyo mchumba wakalala naye, mimba ikaingia na sasa mtoto kazaliwa tayari.

Je kati ya wachumba hao watatu, ni yupi anayeweza kujinyima hadi kulala njaa, ili kukusanya pesa ya mahari na kwenda kutimiza adhima yake ya kumuoa mchumba bila kuweka visingizio?

Naomba majibu ya mifano hii ili nitiririke kwa ufasaha zaidi na jibu la matendo unayofanyiwa na hawara yako yatapatikana menyewe bila mimi na wewe kuweka hisia zetu kutengeneza majibu hayo.
Hakuna atakayejinyima kumuoa huyo msichana tena maana kashazalishwa, kwa mtazamo wangu.
 
Mkuu wewe hujawahi kuumizwa?
Sijawahi kuumizwa wala kuumiza I'm very genius and you can't shutdown genius.

Hayo mambo huwa nayasikia kwa watu .

Kwanza Mimi ni MTU positive Sana mwenye upendo halisi , nikisema upendo halisi nampenda MTU not only for sex or anything nampenda kwakuwa najua ni binadamu anahitaji kupendwa. So akiniacha yeye ndo anakuwa amepoteza so why niumie na kitu nachojua hapa duniani good people are very rare

So ni ngumu Sana Mimi nikutane na watu wasioeleweka na kujenga nao bond.
 
Kweli situation za mahusiano zinafanana
Mimi wangu ndio yuko hivyo tangu najuana nae yaani hata mkiachana now hakuulizi hata kama umefika salama atakaa hata wiki ndio anakutafuta halafu anajifanya mbona umenichunia

Natamani ningekuwa mchawii angenikomaa pumbavu zake 😫😫
Kwanini mnateseka jamani na wanaume tunaojua kupenda tupo.

Haya sogelea PM hapo nikupe mapenzi ya kisharukhan
 
Ila kikubwa mapenzi ni mawasiliano na maelewano usipomtafuta lazma akutafute ila ukimute na yy anamute aah ukinuna ubembelezwi unanuniwa zaidi,usiendelee kuwa mtumwa wa mapenzi hali ya kuwa ni ngumu kukubali ukweli ila ikibidi pita hvii
ila watu mloolewa tayar kwa kutwambia wenzenu tupite iviii,,sasa tutanyanduliwa na wangap ad kuja kupata wa kutuwowaaaaa
 
Sijawahi kuumizwa wala kuumiza I'm very genius and you can't shutdown genius.

Hayo mambo huwa nayasikia kwa watu .

Kwanza Mimi ni MTU positive Sana mwenye upendo halisi , nikisema upendo halisi nampenda MTU not only for sex or anything nampenda kwakuwa najua ni binadamu anahitaji kupendwa. So akiniacha yeye ndo anakuwa amepoteza so why niumie na kitu nachojua hapa duniani good people are very rare

So ni ngumu Sana Mimi nikutane na watu wasioeleweka na kujenga nao bond.
Dah! Hongera sana mkuu nilitamani sana kupata mwanaume anayejua thamani ya upendo ila naona huyu hayupo tayari kabisa
 
Kwaiyo nifanyaje sasa
Hebu niambie kitu nifanye yaani nianze Leo

Mapenzi yanatesa sana yaani mpk nimebaki mdogo mdogo sinenepi 😂
Kuwa positive Sana hakikisha unampatia energy huyo soulmate wako .

Ile kulalamika ,kulaumu , kumfokea ,chuki ,hasira , wivu n.k hayo mambo hayafai .

You have to tune his frequency
 
Kuwa positive Sana hakikisha unampatia energy huyo soulmate wako .

Ile kulalamika ,kulaumu , kumfokea ,chuki ,hasira , wivu n.k hayo mambo hayafai .

You have to tune his frequency
Mpnz wangu huyu ambae tangu tulipo achana j4 mpk Leo hajanitafuta halafu anajipost tu huko social networks 😒😒
 
Kuwa positive Sana hakikisha unampatia energy huyo soulmate wako .

Ile kulalamika ,kulaumu , kumfokea ,chuki ,hasira , wivu n.k hayo mambo hayafai .

You have to tune his frequency
Mpnz wangu huyu ambae tangu tulipo achana j4 mpk Leo hajanitafuta halafu anajipost tu huko social networks 😒😒
 
ila watu mloolewa tayar kwa kutwambia wenzenu tupite iviii,,sasa tutanyanduliwa na wangap ad kuja kupata wa kutuwowaaaaa
😄😄😄Uzuri ni kwamba kila mmoja anapitia changamoto zake kwaiyo aah wengine tamu wengine ndohivooo akirud haya akilala huko sawa
 
Back
Top Bottom