Nashindwa kuelewa, hapa kuna upendo kweli au napotezewa muda?

Nashindwa kuelewa, hapa kuna upendo kweli au napotezewa muda?

NRNE
Habari za muda mrefu wana jukwaa, mimi msichana, niko kwenye mahusiano na mwanaume amenizidi miaka 15, yeye ana mtoto mmoja mimi sina.

Mimi nipo Dar, yeye yupo mkoani, tulipoanza mahusiano nilijua kwakuwa ni mtu mzima pengine, tutaenda sawa kwani na mimi huwa sipendi mambo ya hovyo. Lakini pia nilijua anaweza kuwa amechoka kukaa mwenyewe hivyo atanioa haraka tu (lakini hii haikuwa dhamira yangu kubwa)

Sasa kuna vitu huwa vinanikosesha amani mno, kwanza huyu mwenzangu unaweza ukaongea tu kitu cha tofauti kinaweza kuwa kidogo tu lakini atakishikilia na kukufanya ujione umekosea sana, hapo utaanza kuomba na misamaha ya kutosha. Lakini yeye ikitokea amekosea atalipindisha hilo kosa hadi lisionekane kama ni kosa.

Kama wiki kadhaa zimepita aliniambia ameenda kwao kusalimia, wakati yupo njiani tulikuwa tunawasiliana hadi anafika, sasa kama siku mbili mbele akaniambia ile siku ameenda alimpitia na mtoto wake ameenda naye, nikamuuliza mbona hukuniambia, akaniambia mambo mengi alipitiwa mh! Nikashangaa.

Wakati yupo huko huko akanipigia akaniambia yupo maeneo ya stendi, sasa sikusikia vizuri kumbe alisema kuna mzigo ameufuata nikamuuliza tena umesema umefata mzigo, akanijibu " hivi maswali yako unayoulizaga huwa unafikiriaga kweli" guys hii kauli iliniuma yaani ameniona mimi sina akili, nikamwambia haya baadae, nikakata simu nikatafakari kama siku tatu nikampigia maana na yeye alinikaushia, hakupokea simu, ila huku status whatsapp anapost, hizi si ni dharau jamani. Na yeye kakaa kama siku mbili tatu hivi akanitumia msg whatsapp " habari yako" na mimi sikuijibu ile siku nijibu "salama" after two days, akajibu kwa kureact akakausha, leo naona kanicheki normal, mimi nikampigia hajapokea.

Nashindwa kuelewa ni upendo gani huo wa kumkasirikia mpenzi wako, kwa vitu vidogo vidogo ambavyo mnaweza kueleweshana tu, wakati mwingine unaweza kukuta usiku ikatokea mmegombana hivi ukimpigia ili muongee muyamalize hapokei kabisa ila msg anajibu anasema hajisikii kuongea, hatakagi suluhisho, sasa najiuliza kama huku mwanzoni yupo hivi je ikitokea tukaingia kwenye ndoa huko si ndo atakuwa akikasirika na matumizi anasusa kutoa kabisa🤕

I'm not perfect, hata mimi nina madhaifu na mapungufu yangu, lakini huwa nina amini kwenye kurekebishana ila mwenzangu naona hilo swala hataki kabisa, niliplay part yangu vya kutosha kujishusha nimejishusha sana misamaha nimeomba mingi mno ila kwa sasa moyo umechoka kuvumilia haya mambo, maisha yanipe stress bado na mapenzi tena yanipe stress si nitajifia na presha.

Naombeni ushauri wenu, wakubwa zangu.
Hayo yoote ndo mapenzi yenyewe usiwe na mengi sabbu huyo hukumzaa wewe,komaa na Mbanga zako kula utamu usiingie msitumi na kiwembe,fita ni fita mura.
 
Dah! Hongera sana mkuu nilitamani sana kupata mwanaume anayejua thamani ya upendo ila naona huyu hayupo tayari kabisa
Watu tumetofautiana na level of consciousness zipo tofauti.

Kile kitu. Unachotaka soul mate wako akufanyie jaribu kuanza kumfanyia wewe.

Mfano unaweza kuwa unataka akupe zawadi basi aanza kumpatia wewe.


Unajua kuna mambo mengi you have to learn kujua MTU mliekutana ukubwani hamuwezi kuendana kwa baadhi ya mambo ikiwemo mitazamo , maamuzi , kujali , n.k


Sehemu unayohisi upo vizuri ebu ifanye kwanza wewe.


Mfano Mimi tangia nazaliwa I never cerebrating birth day Ila Leo hii MTU umekutana nae ni mwanamke anataka birth day yake umpatie zawaidi ,um post n.k

So sometimes you have to understand this
 
NRNE
Habari za muda mrefu wana jukwaa, mimi msichana, niko kwenye mahusiano na mwanaume amenizidi miaka 15, yeye ana mtoto mmoja mimi sina.
Ulikosa vijana wenzio mpaka tutako sisi wazee? No reforms no erection!😁😁😂😂
 
Hahaha Mimi nishazoeaga Kuna muda naumia ila nazoea… tu et mtu manakaa mikoa tofauti ila anauchuna hivyo ni kwamba yuko na ka mtu kake tu
Kabisa hapo kuna namna, fanya ustaarabu wako tu
 
Kwahiyo nivumilie haya mambo?
Nakwambia hiivii,hayo ndo.mapenzi yenyewe,ratiba yako iwe single entry,akiibuka unaibuka akizama nawe unazama,jitahidi kuhesabu single line zide akiibuka unampa unatulia,endelea na ratiba yako usizime data,hesabu uhuru wako katika majukumu
 
Watu tumetofautiana na level of consciousness zipo tofauti.

Kile kitu. Unachotaka soul mate wako akufanyie jaribu kuanza kumfanyia wewe.

Mfano unaweza kuwa unataka akupe zawadi basi aanza kumpatia wewe.


Unajua kuna mambo mengi you have to learn kujua MTU mliekutana ukubwani hamuwezi kuendana kwa baadhi ya mambo ikiwemo mitazamo , maamuzi , kujali , n.k


Sehemu unayohisi upo vizuri ebu ifanye kwanza wewe.


Mfano Mimi tangia nazaliwa I never cerebrating birth day Ila Leo hii MTU umekutana nae ni mwanamke anataka birth day yake umpatie zawaidi ,um post n.k

So sometimes you have to understand this
Mkuu nimeshajishusha sana nimeshakubali makosa hata yasiyoeleweka but this is too much
 
Mpnz wangu huyu ambae tangu tulipo achana j4 mpk Leo hajanitafuta halafu anajipost tu huko social networks 😒😒
Mkuu kumbuka mwanaume na mwanamke wapo tofauti.

Kosa lako unataka mambo anayotakiwa kuyafanya mwanamke ayafanye mwanaume.

Mwanume kikawaida upendo wetu huwa haupo kwa styles ya hivyo .

Mwanaume anapenda scarcity Sana , kwakuwa unajua the guy is safe na wewe upo safe hiyo pekee inatosha Ku-keep love
 
Yaani mimi mtu mpya sitaki kabisa nitazunguka kwenye cycle hapohapo labda mtu mpya awe mume

Mimi siwezi kulala na kila mwanaume kwasasa Sitaki
Haya endelea kumvumilia anaweza akakuwowa
 
Huyo single faza hana mapenzi na wewe anakutumia sababu kakuona unaitaka ndoa kwa nguvu..!!
Na kwenye hilo penzi wewe ndo unajitoa sana jipe muda wa kujipenda mwenyewe. Kama ndoa itajileta yenyewe automatically sio kwa kuforce hata na furushi ili tu uitwe Mrs furushi..!! 😹😹
 
Mkuu nimeshajishusha sana nimeshakubali makosa hata yasiyoeleweka but this is too much
Tengeneza kitu kinaitwa scarcity hii itakusaidia Sana in life and not in relationship Ila hata kwa maisha.

Unachobidi kufanya ni kuhakikisha unaitawala akili ya MTU na hisia Ila sio call ,sms n.k

There's so many ways unaweza kutumia .

Unajua nyie young generation mambo mengi hamjifunzi na inamfanya MTU apoteze excitement kwako mapema.
 
Back
Top Bottom