Humu sio sehemu ya kufanya uteseke hivyo kisa miandiko ya watu, usijinyime nafsi yako eti kisa humu, changanua maushauri ila kamwe usiruhusu yakandamize amani na furaha yako,, jipende
Cha kufanya unatakiwa ukiri ulivyompenda huyo ex mbele yake Yani namaanisha kwa njia ya simu au sms sio ana kwa ana tafadhali, ila tu hakikisha usirudiane nae hiyo itakusaidia kupunguza mtukutiko wa nafsi,,, hii mbinu ilinisaidia Sana kwa wanaume (2) niliowahi kuwapenda kwa moyo, akili na hisia zote kuwasahau kwa haraka sana
Kingine jiapie iwe Ni Kama mwiko wako kurudiana na ex, katika vitu kwangu nimeviheshimu Ni huo mwiko, sirudii matapishi na mpaka sasa nimefanikiwa