Nashindwa kuielewa tabia ya huyu dada kwangu mimi!

Kuna ofisi moja nimekuwa nikienda tangu siku nyingi kupata huduma, katika hiyo ofisi receptionists ni wanawake. Katika hao receptionists kuna mmoja kila akiona nikizungumza na mwenzake yeyote hapo kwenye desk lao la reception anaonesha ishara za kukasirika. Ingawa kila nikifika tu ofisini kwao kupata huduma ananichangamkia ila inaonekana hapendi nikiongea zadi na wenzake hata mbele yake tena akiwa anasikia ninachozungumza na mwenzake yeyote ni mazungumzo yanayohusu huduma za ofisi yao tu na sio kitu kingine.

Hivi karibuni nilifika ofisini kwao huyu dada kupata huduma na baada ya hapo nikumuita pembeni huyu dada kumuomba tuongee na baada ya story za fupi nikamuomba namba zake za simu ila akataa kabisa kunipa namba zake akaniambia yeye ni mke wa mtu yaani ameolewa, nikaenda tena baada ya kama wiki moja kupata huduma, baada ya huduma nikamuita pembeni kama siku ile kumuomba namba akakataa kwa mara nyingine kunipa namba akinisisitiza yeye ni mke wa mtu hawezi kutoa namba.

Lakini sasa najiuliza, je kama kweli huyu dada ni mke wa mtu, KWASABABU gani aoneshe kutopenda mimi kuongea na mwenzake yeyote ofisini kwao? Nimejiuliza sana, je huyu dada huwa anapenda sana wateja wote awahudumie yeye tu, yaani ni kama ni mbinafsi? Na je anawafanyia kama mimi kwa kukasirika wateja wengine wanaofikaga hapo wakihudumiwa na mwenzake ambaye yuko nae reception?

Naombeni msaada wenu wadau kunifafanulia juu ya tabia ya huyu dada, je ni tabia gani hii mbona sielewi! cc Robert Heriel Mtibeli, Da'Vinci
Kila ishara Ina lake jambo, huwezi jua labda wadangaji, watumia dawa, wake za watu pia, last but not least ushindani wa kike na ana mvuto kwa wateja, na kamisheni kama ipo ushindani wa kuhudumia wateja closing the deal means something.
 
asee huyo muhudumu atakuwa na tatizo...lakini kwa kuwa ni mwanamke jaribu kumdadisi utajua tatizo lake ..kwanini akiombwa namba aseme yeye ni mke wa mtu..anajua wewe shida yako ni kugusa unyevu tu na inawezekana ameshakutamani
 
Kuna ofisi moja nimekuwa nikienda tangu siku nyingi kupata huduma, katika hiyo ofisi receptionists ni wanawake. Katika hao receptionists kuna mmoja kila akiona nikizungumza na mwenzake yeyote hapo kwenye desk lao la reception anaonesha ishara za kukasirika. Ingawa kila nikifika tu ofisini kwao kupata huduma ananichangamkia ila inaonekana hapendi nikiongea zadi na wenzake hata mbele yake tena akiwa anasikia ninachozungumza na mwenzake yeyote ni mazungumzo yanayohusu huduma za ofisi yao tu na sio kitu kingine.

Hivi karibuni nilifika ofisini kwao huyu dada kupata huduma na baada ya hapo nikumuita pembeni huyu dada kumuomba tuongee na baada ya story za fupi nikamuomba namba zake za simu ila akataa kabisa kunipa namba zake akaniambia yeye ni mke wa mtu yaani ameolewa, nikaenda tena baada ya kama wiki moja kupata huduma, baada ya huduma nikamuita pembeni kama siku ile kumuomba namba akakataa kwa mara nyingine kunipa namba akinisisitiza yeye ni mke wa mtu hawezi kutoa namba.

Lakini sasa najiuliza, je kama kweli huyu dada ni mke wa mtu, KWASABABU gani aoneshe kutopenda mimi kuongea na mwenzake yeyote ofisini kwao? Nimejiuliza sana, je huyu dada huwa anapenda sana wateja wote awahudumie yeye tu, yaani ni kama ni mbinafsi? Na je anawafanyia kama mimi kwa kukasirika wateja wengine wanaofikaga hapo wakihudumiwa na mwenzake ambaye yuko nae reception?

Naombeni msaada wenu wadau kunifafanulia juu ya tabia ya huyu dada, je ni tabia gani hii mbona sielewi! cc Robert Heriel Mtibeli, Da'Vinci

Uwezo wako na tafsiri zako zina shida, huyo Dada kwa kifupi hana time na wewe hata kidogo, wewe ndo una kiherehere, fanya kazi na mambo yanayokupeleka hapo.
 
mkuu King Kong III busara yako pia hapa naomba

Heshimu maamuzi yake kama amekwambia mke wa tu achana naye ,wewe ukienda ofisini kwao fuata ulichokifata ,ongea nao wote peaceful including huyo mke wa mtu ,usionyeshe interest kwa yeyote kati ya hao wanawake.

Mwanamke akishakwambia hivyo(2 Times) ukinga'ang'ania hapo kifuatacho ITV hautokaa kuamaini.
 
asee huyo muhudumu atakuwa na tatizo...lakini kwa kuwa ni mwanamke jaribu kumdadisi utajua tatizo lake ..kwanini akiombwa namba aseme yeye ni mke wa mtu..anajua wewe shida yako ni kugusa unyevu tu na inawezekana ameshakutamani
Yes, inawezekana ameshanitamani na anajua naomba namba kwaajili ya kugusa unyevu
 
Heshimu maamuzi yake kama amekwambia mke wa tu achana naye ,wewe ukienda ofisini kwao fuata ulichokifata ,ongea nao wote peaceful including huyo mke wa mtu ,usionyeshe interest kwa yeyote kati ya hao wanawake.

Mwanamke akishakwambia hivyo(2 Times) ukinga'ang'ania hapo kifuatacho ITV hautokaa kuamaini.
Thanks mkuu King Kong III kwa ushauri wako, kweli hakuna haja ya kung'ang'ania
 
Hii story umeiweka kama yeye ni predator na wewe ni victim. Si uKubali tu kuwa wewe ndiye unamtaka zaidi ndio maana vitendo vyake flani vinakuathiri kiasi cha kumuanzishia thread. Usingemuelewa asingekuhangaisha na kingine kuwa na kiasi, kama ni mke wa mtu achana nae

Usije kuwa sababu ya anguko la ndoa yake maana yawezekana AMEKUTAMANI Ila bado nafsi inamsuta. Msaidie kwa kukaa mbali
 
Busara kubwa sana hii Eyce
 
sio kila kitu kina umuhim mpaka utake kuvielewa.Mengine unapiga kimya unaachana nayo
 
Hii story umeiweka kama yeye ni predator na wewe ni victim. Si uKubali tu kuwa wewe ndiye unamtaka zaidi ndio maana vitendo vyake flani vinakuathiri kiasi cha kumuanzishia thread. Usingemuelewa asingekuhangaisha na kingine kuwa na kiasi, kama ni mke wa mtu achana nae

Usije kuwa sababu ya anguko la ndoa yake maana yawezekana AMEKUTAMANI Ila bado nafsi inamsuta. Msaidie kwa kukaa mbali
Akijipendekeza acha aliwe tuu..si ni mtu mzima
 
Umalaya umetokea wapi hapo? Kuomba namba ni umalaya KENZY ?
Si ashakuambia ni mke wa mtu two times!!!
Ulivyo hasidi gaidi husikii umeendekeza tamaa mbele mauti nyuma,ile binamu nyama ya hamu naona inakutoa ufahamu shauri yako.. endelea kusema huuoni umalaya hapo utakuja kuonyeshwa ukiwa umeshachelewa!...😂
 
Siku zote nikiona hili jina huwa nadhani ni mdada kumbe ni mwanaume
Utandawazi oyee
 
Back
Top Bottom