Nashindwa kuielewa tabia ya huyu dada kwangu mimi!

Nashindwa kuielewa tabia ya huyu dada kwangu mimi!

17_32.gif

Qur'an 17:32. Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya.32
 
kwahiyo kukuchangamkia tu ndo ushajua anakutaka? acha umalaya mzee fata unachofuata mengine achana nayo.
 
Kuna ofisi moja nimekuwa nikienda tangu siku nyingi kupata huduma, katika hiyo ofisi receptionists ni wanawake. Katika hao receptionists kuna mmoja kila akiona nikizungumza na mwenzake yeyote hapo kwenye desk lao la reception anaonesha ishara za kukasirika. Ingawa kila nikifika tu ofisini kwao kupata huduma ananichangamkia ila inaonekana hapendi nikiongea zadi na wenzake hata mbele yake tena akiwa anasikia ninachozungumza na mwenzake yeyote ni mazungumzo yanayohusu huduma za ofisi yao tu na sio kitu kingine.

Hivi karibuni nilifika ofisini kwao huyu dada kupata huduma na baada ya hapo nikumuita pembeni huyu dada kumuomba tuongee na baada ya story za fupi nikamuomba namba zake za simu ila akataa kabisa kunipa namba zake akaniambia yeye ni mke wa mtu yaani ameolewa, nikaenda tena baada ya kama wiki moja kupata huduma, baada ya huduma nikamuita pembeni kama siku ile kumuomba namba akakataa kwa mara nyingine kunipa namba akinisisitiza yeye ni mke wa mtu hawezi kutoa namba.

Lakini sasa najiuliza, je kama kweli huyu dada ni mke wa mtu, KWASABABU gani aoneshe kutopenda mimi kuongea na mwenzake yeyote ofisini kwao? Nimejiuliza sana, je huyu dada huwa anapenda sana wateja wote awahudumie yeye tu, yaani ni kama ni mbinafsi? Na je anawafanyia kama mimi kwa kukasirika wateja wengine wanaofikaga hapo wakihudumiwa na mwenzake ambaye yuko nae reception?

Naombeni msaada wenu wadau kunifafanulia juu ya tabia ya huyu dada, je ni tabia gani hii mbona sielewi! cc Robert Heriel Mtibeli, Da'Vinci
Unataka msaada gani?
 
Heshimu maamuzi yake kama amekwambia mke wa tu achana naye ,wewe ukienda ofisini kwao fuata ulichokifata ,ongea nao wote peaceful including huyo mke wa mtu ,usionyeshe interest kwa yeyote kati ya hao wanawake.

Mwanamke akishakwambia hivyo(2 Times) ukinga'ang'ania hapo kifuatacho ITV hautokaa kuamaini.
Kwa nini asionyeshe intereste kwa yoyote? Kama huyo kamkataa ana weza pick yoyote.
 
Kwa nini asionyeshe intereste kwa yoyote? Kama huyo kamkataa ana weza pick yoyote.

Si kashaeleza kwamba akionyesha interest kwa wengine yule Mke wa mtu anakasirika so ili kusiwe na makasiriko inabidi aplay fair ground na pia ajikite zaidi ya kilichompeleka kama kuna mambo yao nje ya kazi wakayafanyie mtaani na si ofisini wasije wakaharibu kazi.
 
Si kashaeleza kwamba akionyesha interest kwa wengine yule Mke wa mtu anakasirika so ili kusiwe na makasiriko inabidi aplay fair ground na pia ajikite zaidi ya kilichompeleka kama kuna mambo yao nje ya kazi wakayafanyie mtaani na si ofisini wasije wakaharibu kazi.
Maisha hayako fair, pili huyo mke wa mtu amkasrikie mumuwe,
 
Back
Top Bottom