Nashindwa kuitawala pesa. Laki Tano inaisha ndani ya wiki Moja. Natumia dawa za matatizo ya akili. Nifanye nini?

Nashindwa kuitawala pesa. Laki Tano inaisha ndani ya wiki Moja. Natumia dawa za matatizo ya akili. Nifanye nini?

Nina shida ya kiakili natumia dawa zinatwa resperidone. Changamoto niliyonayo ni kuwa hata nifanye Nini nkipata kipato haichukui wiki laki Tano imeisha. Hata niweke mikakati ghani nitajikuta tu baada ya wiki nipo kwenye stress Sina pesa. Nmefikia hatua Sasa hii hali imenichosha naomba ushauri bila matusi Wala kebehi nifanye Nini kuondokana na hii hali.
kitu cha kwanza ni afya ya akili sasa tayari unatumia dawa hapo ndio tatizo linapoanzia, hata hivyo hujasema pesa zako zinaishia kwenye mambo gani maana yanawezekana ni mambo ya maendeleo hivyo unataka kuyafanya yote kwa pamoja bila kufuata hatua . ebu elezea matumizi yako ya pesa yalivyo.
 
Kula pekee hakumalizi pesa ila kama upo ktk hivi vifuatavyo jua pesa haitokaa mfukoni

Ulevi wa kamari
Ulevi wa pombe/madawa ya kulevya
Ulevi wa wanawake (kununua malaya)
Nani amekwambia kula hakumalizi pesa? Unatakiwa kusema ugali na maharage ndio havimalizi pesa.
Ila kama unakula chakula haswa pesa lazima ipukutike
 
Fungua account soecial inayo kuruhusu kutoa pesa mara 2 tu kwa mwaka tena bila kutumia kadi, yaani ili utoe ni lazima upange foleni.

Baada ya hapo ukipata laki 5 toa zaka na sadaka then chukua laki 1 nanusu iweke kwenye account special, inayobaki nunua chakula cha kukutosha, lipa bili zote then inayobaki itumie kwa kifua mbele.
 
Nina shida ya kiakili natumia dawa zinatwa resperidone. Changamoto niliyonayo ni kuwa hata nifanye Nini nkipata kipato haichukui wiki laki Tano imeisha. Hata niweke mikakati ghani nitajikuta tu baada ya wiki nipo kwenye stress Sina pesa. Nmefikia hatua Sasa hii hali imenichosha naomba ushauri bila matusi Wala kebehi nifanye Nini kuondokana na hii hali.

Limit access ya pesa yako, ulichonacho ni addiction, ukipunguza access taratibu utakaa sawa
 
Dawa unazokunywa inaonesha unatatizo kubwa
Usikute huna hizo hela ni mawazo yako tu
 
Pole Mkuu, hongera pia mana kujua tatizo ni nusu ya kulitatua.. fungamana na ibada
 
Back
Top Bottom