Nashindwa kuitawala pesa. Laki Tano inaisha ndani ya wiki Moja. Natumia dawa za matatizo ya akili. Nifanye nini?

kitu cha kwanza ni afya ya akili sasa tayari unatumia dawa hapo ndio tatizo linapoanzia, hata hivyo hujasema pesa zako zinaishia kwenye mambo gani maana yanawezekana ni mambo ya maendeleo hivyo unataka kuyafanya yote kwa pamoja bila kufuata hatua . ebu elezea matumizi yako ya pesa yalivyo.
 
Kula pekee hakumalizi pesa ila kama upo ktk hivi vifuatavyo jua pesa haitokaa mfukoni

Ulevi wa kamari
Ulevi wa pombe/madawa ya kulevya
Ulevi wa wanawake (kununua malaya)
Nani amekwambia kula hakumalizi pesa? Unatakiwa kusema ugali na maharage ndio havimalizi pesa.
Ila kama unakula chakula haswa pesa lazima ipukutike
 
Fungua account soecial inayo kuruhusu kutoa pesa mara 2 tu kwa mwaka tena bila kutumia kadi, yaani ili utoe ni lazima upange foleni.

Baada ya hapo ukipata laki 5 toa zaka na sadaka then chukua laki 1 nanusu iweke kwenye account special, inayobaki nunua chakula cha kukutosha, lipa bili zote then inayobaki itumie kwa kifua mbele.
 

Limit access ya pesa yako, ulichonacho ni addiction, ukipunguza access taratibu utakaa sawa
 
Dawa unazokunywa inaonesha unatatizo kubwa
Usikute huna hizo hela ni mawazo yako tu
 
Pole Mkuu, hongera pia mana kujua tatizo ni nusu ya kulitatua.. fungamana na ibada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…