Nashindwa kulielewa hili gari

Nashindwa kulielewa hili gari

Bmw huwa haitengenezwi kwa Fundi Maiko ndugu yangu.
Nenda gereji ya maana au DT Dobie mkuu.
Vinginevyo akina fundi Maiko watakuagua mwishowe utalitelekeza gari.
Jambo la mwisho.
Kama usivyoweza kumwazima mtu mke wako au mpenzi wako, kadhalika gari bora uonekane mchoyo.
[emoji3][emoji3] yan gari yangu hajawahi endesha mtu mwingine hata siku moja..kwangu ni mwiko aisee.
 
Imezima mitaa ya vingunguti nikawasha, nikama haitaki niachie mafuta sana kwahiyo kwenye kona niingie mazima ndani nasikia petrol harufu
Hamna gar hapo pole sana
 
Kama 300k inakufanya upaki gari achana nayo. Msivamie vitu bila utafiti. Sasa kuna electric water pump humo siku chache zijazo itakufa ukitajiwa bei utakufa kabisa.
Inashangaza sana mtu anakimbia kisa 300k na anasema [emoji3][emoji3]
 
We jamaa ukiona sedan unaiona kama chapati sio? Kwamba inatambaa?

Sema niwe mkweli, natoboaga sana flexible pipes za exhaust kwenye barabara mbovu. Nimekaa Dom mwezi barabara nzuri sijaigusa, nimefika tu Dar in two weeks jana nimeingia mahali nikaskia imegota. Muda si mrefu nikapata matokeo, inavuja exhaust. Kwenye underbody ya Fuga flex pipe ndio iko most exposed.

Sedan zina hasara zake na raha zake.
Hapa wazungu ndipo nawapendea gari chini imefichwa haswaa hakuna kitu kipo wazi wazi.. iwe pipe au nini ila specific kwa Benz, na Audi, ila kwa Jaguar ina uwazi na one week nikapasua pipe exhaust ikaanza kuvuja
 
Wameweka skid plate? Kwamba mpaka exhauset imefichwa?? Kama hamna skid plate maana yake vitu viko exposed mkuu its just matter of nini kitagusa kwanza na hiyo sehemu umeingia kwa angle gani.

Kama hujaona vizuri au umekosea hesabu penye ncha pakawa katikati lazima uguse kitu huko chini no way out. Ila kama ncha umezipitia na tairi itakita frame ya gari ambayo japo inalia vibaya haina madhara.

Kuna mtu humu anabadili sana ID sijui anatumia ipi now ila alikuwa anapiga trip akatoboa oil sump ya Audi A3/4 barabarani.
 
Namna walivyo weka vitu vyao kwa chini na vilivyokuwa fixed kwa hizo gari husika Benz na Audi, siwezi sema kama skid plate ile, the way walivyo vi fix hata kuingizia mkono shughuli pevu. Audi A4, ile guard yake ilitoka ilienda fanyiwa services mafundi hawakufinga vyema ikawa imetoka na chini paka wazi samp kufikiwa ma chochote plus gari ilikuwa chini sana.. Sedan changamoto ya kutambalia tumbo haikwepeki kwa mazingira yetu na makazi yetu
 
Nimeleta kesi ya traffic kwa polisi
 
Nimenunua BMW 5 series 2006 kwa mtu ikiwa fresh nimeendesha kama mwezi ilikuwa poa mpaka nilipompa jamaa alikuwa na safari ya Bagamoyo aliporudi nikaichukua kuendesha kidogo nikaona kama nakanyaga sana mafuta gari haiendi.

Nimeenda kwa fundi akasema shida plug nikanunua zikafungwa baada ya kuendesha naona mambo ni yale yale. Nikamuuliza fundi mwingine kasema nibadilishe pump, sijawahi kumiliki BMW before naomba uzoefu wenu wadau kabla sijanunua tena fuel pump.
😁😁😁😁 Bavaria Extrovert njooni mumsaidie ndugu yenu huyu
 
Wadau wapi naweza pima ubora wa mafuta diesel na petrol Ili kumeet standard itakiwayo.
 
Mkuu wabongo washazoea service ni kumwaga oil tu, tena hapo bajeti unakuta kaweka top top elfu 50. Oil ya 30k, filter 10k na fundi 10k. Mbongo kupeleka gari garage ikakaguliwe yote hafanyi hiyo kazi hata akiwa na safari ya kwenda mbali atamwaga oil tu tena hapo kama imemaliza au imekaribia kilomita. Tyre wananunua hizi za kichina na hapo kubadilisha ni mpaka iwe kipara. Tyre za kichina sio reliable kabisa, tena hasa kwa safari ndefu ila kwakuwa tunapenda vya bei rahisi tunaona poa tu.

Gari ya kizungu lazıma ukubali kila baada ya miezi sita at least uipeleke check up, tena sio zile chini ya mti ni ile unakabidhi gari na email yako wewe unaendelea na mambo yako. Check up ikiwa tayari unakutana na Invoice kwenye email unalipa unaenda na slip yak unachukua mali yako na guarantee juu.

Nilijisikia fahari sana nimepeleka gari service siku naenda kuchukua nikakaa na Muhasibu wao kuongea akaniambia ile garage Mzee Jakaya ndio garage ya magari yake. Na wala bill haikuwa kubwa, walikagua gari na wakatoa spare ambayo waliona inaelekea mwisho wakaweka nyingine basi, ningepeleka chini ya mwembe vingebadilishwa mpaka vizima ili kazi iwe kubwa na wao apate pesa nyingi.
Endelea tu kukabidhi gari na email, iko siku utakuta email invoice bei ya nusu gari na gari haitoki bila malipo. Washakuvuta hapo tayari bado kukupiga sasa wewe na jakaya ardhi na mbingu mwenzako kuacha million 20 kwa service ya V8 siyo tatizo.
 
Back
Top Bottom