Mkuu wabongo washazoea service ni kumwaga oil tu, tena hapo bajeti unakuta kaweka top top elfu 50. Oil ya 30k, filter 10k na fundi 10k. Mbongo kupeleka gari garage ikakaguliwe yote hafanyi hiyo kazi hata akiwa na safari ya kwenda mbali atamwaga oil tu tena hapo kama imemaliza au imekaribia kilomita. Tyre wananunua hizi za kichina na hapo kubadilisha ni mpaka iwe kipara. Tyre za kichina sio reliable kabisa, tena hasa kwa safari ndefu ila kwakuwa tunapenda vya bei rahisi tunaona poa tu.
Gari ya kizungu lazıma ukubali kila baada ya miezi sita at least uipeleke check up, tena sio zile chini ya mti ni ile unakabidhi gari na email yako wewe unaendelea na mambo yako. Check up ikiwa tayari unakutana na Invoice kwenye email unalipa unaenda na slip yak unachukua mali yako na guarantee juu.
Nilijisikia fahari sana nimepeleka gari service siku naenda kuchukua nikakaa na Muhasibu wao kuongea akaniambia ile garage Mzee Jakaya ndio garage ya magari yake. Na wala bill haikuwa kubwa, walikagua gari na wakatoa spare ambayo waliona inaelekea mwisho wakaweka nyingine basi, ningepeleka chini ya mwembe vingebadilishwa mpaka vizima ili kazi iwe kubwa na wao apate pesa nyingi.