Umri wako na muda uliotumia,hizo sindano wala hazina uhusiano na tatizo lako la kutozaa!
Ushauri ni huu;
Mpangilio wa hedhi upo sawa!? Km upo sawa unafahamu siku za hatari yaani siku za kukutana na mmeo kwa lengo la kupata mtoto!?? Km majibu yote ni NDIYO basi kuna haja ya kwenda kuwaona madaktari.
Kwa wewe utamuona daktari wa magonjwa ya wanawake,atakuandikia vipimo kulingana na historia ya tatizo lako. Baada ya uchunguzi km utaonekana huna tatizo,basi tatizo litakuwa kwa baba.
Hapa kwa baba ndo kwenye shida kubwa,kwa kawaida mwanaume km anafanya tendo la Ndoa na kufikia mshindo,ni vigumu sana kumshawishi aende kwenye tiba ya uzazi. Wengi wanaamini km anatoa manii(sperms) basi atajua ana uwezo wa kuzaa na km hampati mtoto tatizo hilo litaangushiwa kwa mama!
Mwanaume ili awe na uwezo wa kuzaa,mbali na kuwa na mbegu tu za kiume,mbegu hizo pia zinapaswa kuwa hai na zenye kasi..
Mwanaume anapofikia mshindo,km mbegu zake ni hafifu(zisizo na mikia) hushindwa kuogelea kulifikia yai la mwanamke kwa ajili ya kulirutubisha na hivyo hufia njiani..
Mshauri mkamuone daktari wa magonjwa ya wanaume,atapima uwezo wa mbegu za baba km zina mikia.
Iwapo baba nae atakuwa hana tatizo,basi tatizo lipo kwenye hesabu ya siku ya kutungisha mimba. Km ukiijua,baba inabidi awe na mbegu za kutosha siku hiyo,awe amekula vizuri na hana mawazo ya kukera. Asiwe amefanya tendo la Ndoa angalau siku 2 kabla. Km hujui siku ya kupata mimba,nambie hapa hapa mzunguko wako ni wa siku ngapi ili nikuambie siku ya kukutana na baba. Mzunguko wako unahesabu kuanzia siku uliyoona damu mpaka siku ya kuona damu mwezi unaofuata...!
Pole kwa maelezo marefu....