Nashukuru Mchumba wangu Amenisamehe baada ya Kumfumania

endelea kumbembeleza huyo ulomfumania maana ndiyo faraja pekee ulonayo baada ya dada yako na shemejio kupatana.
 
Duu! Kuna watu na viatu
 

[emoji23][emoji23][emoji23]
 


Lete Maneno.....

By JK Wa Msoga Chalinze Tanzania
 
Kaa chini natafakari sana maisha yako hasa uko mbeleni. Umeonyesha kukubali hicho kitendo je utakubali hata hukombele, kumbuka hakuna lolote litakalobadilika ukioa maana mtu na tabia ni yuleyule. Kama umeukubali huo udhaifu wake basi sawa, we endelea. Ila kitu kimoja tu shika, upendo huisha na kwakuwa dunia imefanya vile sio lazima nawewe ufanye. Misimamo yako ya leo ndio misimamo itakayoisimamia familia yako huko mbeleni. Ninani aijuaye kesho, ila kamwe usizembee kuweka msingi wa maisha yako. Mwanamke sio ndugu, ni partner au companion na hivi huisha. Tumia akili na hekima nasio hisia. Hisia huisha, acha kuweka furaha yako kwamtu mwingine, utaumia sana. Simamia nafasi yako ka mwanaume, tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna mapenzi hapo sema we ni mtumwa wake. Unahitaji ushauri wa kutoka utumwani.
 
Never settle for less kwasababu utajilaumu na kuumia sana mbeleni. Wote wenye hizo tabia wapo ila kucheat ni combination ya vyote. Ukiogopa kusimamia ukitakacho basi utabaki kujilaumu sana mbeleni. Kuoa sio lazima, ukimkosa mwenye msingi mizuri ya maisha acha tulia kwakuwa ukiendelea naye atakuvuruga kabisa hata hapo ulipo maana ataiharibu afya yako ya akili. Na bila afya njema basi huna utakaloweza fanya. Uzinzi upo, ila mimi si mzinzi basi sitakubali niishi mtu mzinifu maana itaniharibia msingi mzima wa maisha yangu. Ukikosa mtu sahihi wa maisha, achana na mahusiano lasivyo utalea familia mbovu huku ukiwa na uchungu, kama utaishi hivyo mpaka kuingia kaburini basi sawa ila kamwe usipige kelele. Ukiharibu msimamo wako ili tu kumpata mtu basi utaharibu misimamo yote ya maisha yako. Kuoa sio lazima mkuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…