TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 5,771
- 17,849
Never settle for less kwasababu utajilaumu na kuumia sana mbeleni. Wote wenye hizo tabia wapo ila kucheat ni combination ya vyote. Ukiogopa kusimamia ukitakacho basi utabaki kujilaumu sana mbeleni. Kuoa sio lazima, ukimkosa mwenye msingi mizuri ya maisha acha tulia kwakuwa ukiendelea naye atakuvuruga kabisa hata hapo ulipo maana ataiharibu afya yako ya akili. Na bila afya njema basi huna utakaloweza fanya. Uzinzi upo, ila mimi si mzinzi basi sitakubali niishi mtu mzinifu maana itaniharibia msingi mzima wa maisha yangu. Ukikosa mtu sahihi wa maisha, achana na mahusiano lasivyo utalea familia mbovu huku ukiwa na uchungu, kama utaishi hivyo mpaka kuingia kaburini basi sawa ila kamwe usipige kelele. Ukiharibu msimamo wako ili tu kumpata mtu basi utaharibu misimamo yote ya maisha yako. Kuoa sio lazima mkuu!
Sent using Jamii Forums mobile app
Kusimamia ukitakacho ni pamoja na kuoa mwanamke unaempenda na ndio anachotaka kufanya jamaa yetu hapo. Pia huenda huyo mwanamke ndio anampa afya ya akili, pengine akimuacha ndio afya yake ya akili itazorota na atachanganyikiwa kabisa! Haya maisha yana mambo mengi..