Nasikitika kuona Mr Kuku akienda kuwatapeli baadhi ya watanzania wenzetu kwa mara nyingine.

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
21,387
Reaction score
44,030
Baada ya kuwatapeli watu zaidi ya mara tatu kupitia mradi wa kuku, Kijana Tariq kaja kivingine kupitia mradi anaoita mbuzi pesa. Utaratibu wake ni uleule wa kuchangisha watu pesa. Ikumbukwe mara baada kuachiwa kupitia plea bargain mara baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kuchezesha upatu, Mr Kuku alianzisha upya mradi wake wa kuku kwa kuwachangisha watu. Lakini kama kawaida alianza blahblah na watu wakaishia kupigwa hela zao.

Hadi ninavyoandika Tariq au Mr Kuku anadaiwa na watu wengi huku mwenyewe akikiri hana hela kabisa na kutaka watu wasubiri. Cha kushangaza ni huu ujasiri wake wa kuanzisha upya mradi wa mbuzi pesa ambao hata kipofu anaona ni upigaji mwingine.

Wewe mtanzania mwenzangu tafadhali usijiingize kwenye huu utapeli kwa tamaa ya mafanikio ya haraka. Mr Tariq ni tapeli mwenye uzoefu mkubwa. Kaa naye mbali.

Ninaisihi serikali iwe macho na huyu kijana kwa sababu pia anatumika kutakatisha pesa. Ingependeza serikali ingewakamata watu wote waliowekeza kwa Tariq ili watoe maelezo ya vyanzo vyao vya pesa. Kuna mwanamke aliwekeza cash Tsh 75m kwa Tariq na akaishia kuzipoteza. Kimsingi wengi wa wanaowekeza kwa Tariq sio mafukara.
 
Attachments

  • Screenshot_20250720-203011_Instagram.jpg
    Screenshot_20250720-203011_Instagram.jpg
    155.5 KB · Views: 39
Baada ya kuwatapeli watu zaidi ya mara tatu kupitia mradi wa kuku, Kijana Tariq kaja kivingine kupitia mradi anaoita mbuzi pesa. Utaratibu wake ni uleule wa kuchangisha watu pesa. Ikumbukwe mara baada kuachiwa kupitia plea bargain mara baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kuchezesha upatu, Mr Kuku alianzisha upya mradi wake wa kuku kwa kuwachangisha watu. Lakini kama kawaida alianza blahblah na watu wakaishia kupigwa hela zao.

Hadi ninavyoandika Tariq au Mr Kuku anadaiwa na watu wengi huku mwenyewe akikiri hana hela kabisa na kutaka watu wasubiri. Cha kushangaza ni huu ujasiri wake wa kuanzisha upya mradi wa mbuzi pesa ambao hata kipofu anaona ni upigaji mwingine.

Wewe mtanzania mwenzangu tafadhali usijiingize kwenye huu utapeli kwa tamaa ya mafanikio ya haraka. Mr Tariq ni tapeli mwenye uzoefu mkubwa. Kaa naye mbali.
Hii kamali
 
Back
Top Bottom