Nasikitika kusema, baada ya miaka 13 kwenye ndoa leo mimi na mke wangu tumetalakiana

Ni mtu ambaye niliishi naye miaka kumi na tatu na tulibahatika kupata watoto wanne.

Ila leo mama Agness nimempa talaka mahakamani bila kupenda. Imeniuma sana nilimzoea sana mke wangu.

Mama Agness ameniliza sana. Daaah talaka inauma sana kwa mtu uliyemzoea. Nimemuuzi mtu niliyempenda.

Ndiyo hivyo tena hatimaye mimi na mke wangu leo mwendo tumeumaliza.

We jamaa si ndio ulipigaga ila pisi iliyotoka Mwanza ukampa 7800 au nimekufananisha?

Leo yamekukuta wewe
 
Mtu umemzalisha watoto wa nne una wasi wasi gani?...yeye ndo amepoteza mkuu...hakuna mtu atakayekubali kuoa mtu ana watoto wanne...ingekuwa mm ningefanya sherehe na kuvuta chombo kipya within a week!
 
Wewe ndio mafala duniani. Kama unampenda bado mpaka kukuliza kwa nini unamuacha?. Mimi nilijua unaweka sherehe kabisa kufanikisha kufikia kitu kigumu Talaka??.

Mimi natamani hata kufikia leo Talaka,lakini mwanamke huyu ni king'ang'anizi hatari. Nimetumia kila njia nifikie hatua uliyofikia wewe.

Mpaka siku nikabeba vitu vyote ndani na loli nilimwambia ndio nakupeleka kwenu na vitu vyote vya humu ndani. Aliita watu wote ninaofahamiana nao mpaka wachungaji sio kwamba anaomba samahani ili tu wasuruhishe abaki. Nimesema kwamba kuomba samahani mke ni jeuri,kiburi. Tunaweza tukakaa hata miezi mi3 amenuna tu. Tunaishi kama jehanum karibia mwaka wa 15. Kuachana ndio hataki kabisa.

Mimi nikifikia hatua uliyofikia wewe ni sherehe. Sitarudi nyuma kumfikiria hata nusu,. Halafu sitaoa tena maisha yangu yote yaliyobakia.
Sasa si uendee mahakamani ukachukue talaka
 
Ndio pale niliposema kwa vijana wa kiume wanapambana na mengi. Ksbb wengi wanapitia magumu kwenye ndoa lakini ksbb ya ile hali ya uanaume anabaki nayo moyoni.

Pia ambacho kwangu ni kinanisumbua ni muda sina. Nina shughuri zangu nyingi,kwa hiyo si unajua mambo ya mahakama...! Siku ambazo una kazi MUHIMU ofisini kwako ya kuingiza hela,ndio inatakiwa na wewe uende mahakamani.

Mwisho wewe mwanaume kwenda mahakamani kudai Talaka ndio ufala nao wa hali juu. Bora upambane kivingine,lakini sio mimi kwenda mahakamani. Ikishindikana bora hata uandae gunia mbili,au hata tatu za mkaa (natania mkuu,siwezi kufikia huko,ila kwenda mahakamani nako siwezi)
 
Kwanini uishi maisha artificial wakati maisha ni haya haya mafupi??
Yani uishi na mtu ambaye ushamchoka kwa kuwa tu unataka kuonesha uanaume?
Si uhame umuachie nyumba akichoka ataendelea na yake...
Maisha ya amani ni kila kitu asee maana stress unazopata Leo au maumivu unayopitia Leo ndo cancer au stroke ya kesho.
Ninaona watu 2 ambao wanapitia hizi illness kwa sababu ya stress na maumivu waliyopitia kwenye ndoa ila kwa sasa ni too late
 
Ni kama kusogeza siku tu.

Hii ndoa imenifundisha mambo mengi. Zamani wazee ilikuwa mtoto mmojawapo iwe wa kike au kiume akilalamikia ndoa wanamwambia vumilia tu ndio ndoa zilivyo. Kumbe huko ndani anaungulia hatari. Ndio maana kuna wimbi kubwa la wanandoa kuuana.

Hasa vijana wa kiume wanapitia magumu sana kwenye ndoa ksbb ile hali ya uanaume inakufanya uugulie peke yako ndani kwa ndani.

Mimi ksbb najua nimeji-control ili nisiuumize moyo. Kwa hiyo lolote mi poa tu,ili maisha yasonge. Sio kwamba niko vibaya kimaisha...! Yeye mwenyewe nimenunulia usafiri. Wapo watu ambao ni forward tu wanawaza. Hafikiri nyuma,yeye akiwaza jambo usimpinge.
Aisee pole sana, ila ndugu yangu unajua duniani humu hatuishi miaka mingi sana, ikizidi sana wanasema average ni 70. Sasa wewe huoni kuwa maisha yako duniani yatakuwa ni ya kuteseka? Kwanini iwe hivyo? mimi asingeniambia mtu kitu siwezi ishi maisha hayo tungeachana tu. Watoto najua ningefanya namna yoyote waishi vyema.
 
Ndio pale niliposema kwa vijana wa kiume wanapambana na mengi. Ksbb wengi wanapitia magumu kwenye ndoa lakini ksbb ya ile hali ya uanaume anabaki nayo moyoni.

Pia ambacho kwangu ni kinanisumbua ni muda sina. Nina shughuri zangu nyingi,kwa hiyo si unajua mambo ya mahakama...! Siku ambazo una kazi MUHIMU ofisini kwako ya kuingiza hela,ndio inatakiwa na wewe uende mahakamani.

Mwisho wewe mwanaume kwenda mahakamani kudai Talaka ndio ufala nao wa hali juu. Bora upambane kivingine,lakini sio mimi kwenda mahakamani. Ikishindikana bora hata uandae gunia mbili,au hata tatu za mkaa (natania mkuu,siwezi kufikia huko,ila kwenda mahakamani nako siwezi)
Wewe oa mwanamke mwingine yeye ataenda Mahakamani.
 
Mwaka 2015 nikampiga mimba mdada mmoja huko wilayani. Lakini sijamuoa,ila nilikuwa nimekubaliana nae jambo. Ksbb nilimwambia hali halisi kwamba nina familia. Tukaelewana ABC.

Alipojifungua,mtoto amekua kua wa kiume. I see usiambiwe watoto wa kuiba mkuu. Mtoto ametoka copy tembea,kutabasamu,upole,kila kitu kachukua yule mtoto.

Kama kawaida Wazee wa ubuyu wakamtonya mke. Akapita njia zake akamfahamu yule mtoto. Ugomvi huo ulikuwa sio wa nchi hii. Mke akajifanya ameumia sana. Kiukweli ni kama nimemuachia maumivu. Ksbb mpaka aliumwa. Japo sikutaka afikie kwenye kuumwa,ila nilitaka sana apate funzo.

Lakini sio kwamba ndio amejifunza. Na utetezi wangu ni mmoja tu sipewi heshima ya mume ninayostahili kama mume. Kila kitu hapo ndani ni mimi tu ananitegemea. Lakini nafikiri ndio nikajua maana ya watu kusema usioe Mnyakyusa
 
Aisee pole sana, ila ndugu yangu unajua duniani humu hatuishi miaka mingi sana, ikizidi sana wanasema average ni 70. Sasa wewe huoni kuwa maisha yako duniani yatakuwa ni ya kuteseka? Kwanini iwe hivyo? mimi asingeniambia mtu kitu siwezi ishi maisha hayo tungeachana tu. Watoto najua ningefanya namna yoyote waishi vyema.
Ndio hivyo mkuu. Zipo ndoa nyingi tu ambazo watu wamo wanaishi,ila namna ya kuachana inakuwa ngumu sana. Kama mimi hataki,anang'ang'ana.

Unajua nini mambo ya dharau za wanawake ndani ya nyumba ni ndogo ndogo lakini zenye maumivu makali ndani ya moyo. Unaweza ukafika nyumbani umeleta vyakula na vitu vingine vingine mahitaji ya nyumbani. Lakini yupo sebuleni anaperuzi amenyoosha miguu. Wewe unahangaika kushusha vitu na HG.

Ukienda kumcheck ni mzima tu. Ukimuuliza hata kuja kuangalia tu?. Anaweza kukujibu kwani nakula mimi tu,si wanakula wanao. Check kama hivyo.

Natamani hata nimfumanie hivi ili iwe ndio ushahidi usiosameheka namna ya kumuacha. Kuna siku hata nilileta uzi mwenye kujua namna ya kudukua simu
 
Mwaka 2015 nikampiga mimba mdada mmoja huko wilayani. Lakini sijamuoa,ila nilikuwa nimekubaliana nae jambo. Ksbb nilimwambia hali halisi kwamba nina familia. Tukaelewana ABC.

Alipojifungua,mtoto amekua kua wa kiume. I see usiambiwe watoto wa kuiba mkuu. Mtoto ametoka copy tembea,kutabasamu,upole,kila kitu kachukua yule mtoto.

Kama kawaida Wazee wa ubuyu wakamtonya mke. Akapita njia zake akamfahamu yule mtoto. Ugomvi huo ulikuwa sio wa nchi hii. Mke akajifanya ameumia sana. Kiukweli ni kama nimemuachia maumivu. Ksbb mpaka aliumwa. Japo sikutaka afikie kwenye kuumwa,ila nilitaka sana apate funzo.

Lakini sio kwamba ndio amejifunza. Na utetezi wangu ni mmoja tu sipewi heshima ya mume ninayostahili kama mume. Kila kitu hapo ndani ni mimi tu ananitegemea. Lakini nafikiri ndio nikajua maana ya watu kusema usioe Mnyakyusa
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] muhaya je hao ndoo balaaa
 
Tatizo mume na mke wakigombana kqa jamii za kitz ndugu wanaingilia pande mbili zinavurugika inakuwa ni uhasama najiulizaga nakosa jibu ni kwann inakuwa ivo hasa ndugu wa mume wanatoka huko kila mtu na lake wanatukana mke mara malaya, na hawajui hata chanzo.

Je unafikiri km mkuu MAGALLAH R ndo mkosaji kuna ndugu anaweza kwenda kuongea na mkewe
Familia wasionkuwa na adabu ndio uwa hivyo lkn wenye hekima mtasumbuana sana..
Mke/Mme inambidi kuolewa/kuoa na mtu/familia sahihi.. Mida ndio huu kurudi zama za Babu zetu..
 
Ni kama kusogeza siku tu.

Hii ndoa imenifundisha mambo mengi. Zamani wazee ilikuwa mtoto mmojawapo iwe wa kike au kiume akilalamikia ndoa wanamwambia vumilia tu ndio ndoa zilivyo. Kumbe huko ndani anaungulia hatari. Ndio maana kuna wimbi kubwa la wanandoa kuuana.

Hasa vijana wa kiume wanapitia magumu sana kwenye ndoa ksbb ile hali ya uanaume inakufanya uugulie peke yako ndani kwa ndani.

Mimi ksbb najua nimeji-control ili nisiuumize moyo. Kwa hiyo lolote mi poa tu,ili maisha yasonge. Sio kwamba niko vibaya kimaisha...! Yeye mwenyewe nimenunulia usafiri. Wapo watu ambao ni forward tu wanawaza. Hafikiri nyuma,yeye akiwaza jambo usimpinge.
Pole mkuu, wanaume tunakufa na mapema kwa sababu nyingi..ikiwemo hili la kuishi na Hawa viumbe kwa lengo la kunusuru maisha na malezi ya watoto.
 
Back
Top Bottom