Nasikitika kusema kwamba, Katiba Mpya tunayoitafuta kwa nguvu nyingi haiwezi kutusaidia

Nasikitika kusema kwamba, Katiba Mpya tunayoitafuta kwa nguvu nyingi haiwezi kutusaidia

Pslmp

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2021
Posts
1,622
Reaction score
2,458
Ndiyo na ni ukweli kabisa, Katiba tunayojaribu kuitafuta kwa jasho jingi na Energy nyingi, nasikitika kusema, haitatusaidia popote kama nchi.

Kama kuna mtu anapingana na mimi, Embu atusaidie kujibu maswali haya

Ni kweli tumekuwa na katiba isiyokidhi matakwa yetu hususani katika mizania ya kisiasa, kwa maana, katiba iliyopo, ilitungwa chini ya Chama kimoja, hivyo kuvifanya vyama vingine kukosa uhalali wa kulindwa na katiba hii tuliyonayo

Kingine, Katiba hii iliyopo, inamfanya Rais wetu kuwa mfalme, ni kama yeye ni mtu wa kwanza na wa mwisho, kwa lugha ys kiyunani, ni Alfa na Omega, n.k

Sasa basi, Ukisikiliza kwa umakini, wengi wa wanaharakati wetu kwenye majukwaa ya kisiasa na majumkwaa mbalimbali mbali, Utasikia wakisema, Tunataka katiba itakayotuwezesha kuwaajibisha wote wanaovunja katiba

Ni jambo jema, maana mtu yeyote anayediriki kuvunja makubaliano yetu na katiba yetu , ni sawa na matusi kwa watu woote kama taifa

Tumeshuhudia katiba yetu ikivunjwa waziwazi na baadhi ya viongozi wetu,

Bahati mbaya ni kwamba, kuna waliovunja katiba hata kwa wale ambao, katiba hailindi ouvu wao kama ilivyo kwa Maraisi wa nchi, lakini wanapovunja, Hasira zetu tunazielekeza kwa kiongozi mkuu, tunamsagia meno, Wakati huohuo, Katiba yetu mbovu tuliyonayo, ni kumlinda Raisi wa nchi na maovu yote kipindi awapo madarakani, na kwamba Hawezi kushitakiwa kwa kosa lolote awapo madarakani

Na bila shaka, shida yetu inaanzia hapo

Okay, Achilia mbali makosa ya Rais kwa mjibu wa katiba mbovu tuliyonayo kwamba, hatoshitakiwa kwa makosa yoyote aliyotenda akiwa madarakani, Hili tunaweza kusema, lipo juu ya mamlaka ya kawaida ya mwananchi kumwajibisha Raisi wao kwa kuwa katiba inamlinda

Upande wa pili kwa kosa hilohilo la kikatiba, Tumeshuhudia Bunge lisilo halali, Ni bunge ambalo wabunge wenginewe waliomo humo bungeni si wabunge halali kwa mjibu wa katiba za vyama vyao pia kwa mjibu wa katiba ya nchi, kwamba hawana uhalali wa kuwa wabunge kwa kuwa, hawatambuliki na vyama vyao na katiba haitambui mtu wa aina hiyo kuwa sehemu ya bunge

Sasa basi

Nionyesheni ni wapi ambapo huyo mkuu wa mhimili huu wa Bunge alipohalalishiwa na katiba hii mbovu tuliyonayo kwamba naye hawezi kuwajibishwa,

Je, sasa, ni nani wa kumwajibisha?
Ni kwa nini tunataka katiba mpya, Je, ni nani atakuwa mbadala wetu wa kusimama na kuwawawjibisha wote wavunja katiba?

Je, katiba hii mbovu ilipokuwa ikivunjwa, ni nani anafahamika ambaye yeye anapaswa kudili na wavunja katiba yetu? Je, alifanya kazi yake?

Na kama alishindwa kuwashughurikia hao waharifu wa kikatiba, Ni kwa vipi anadhani itakuwa rahisi kuwashughurikia kukiwepo katiba mpya?

Ni nani asiyejua kwamba, Watanzania, Watanzania kwao ni wazuri wa kuhamaki mitandaoni pekee ila nje ya hapo ni watu wanafiki na wapole kama maji ya mtungi? na ndiyo maana hata Asiyelindwa na katiba aweza kuvunja katiba na ikawa salama?

Mkinionyesha atakayekuwa zamu ya kuwashughurikia wahalifu wa kikatiba badala yetu, ndipo nitakubali kwamba, Tunataka kweli katiba na tumemaanisha

Katiba haijilimdi, haijipeleki mahakamani, haiandamani na wala haimtishi mvunja katiba, Nionyesheni mlinzi wa katiba

Tanzania hoye?
 
Mkuu umeambiwa kuwa katiba iliyopo hairuhusu rais kushitakiwa popote wala kuwekwa mtu kati.
Jamaa anakubaliana na wewe, ila anauliza, Mbona wanaoivunja katiba ni wengi tu na hata wale ambao katiba haiwalindi nao kwa nini hawadhughulikiwi?

Anasema, Je katiba mpya tunayoitaka, Itajipeleka mahakamani yenyewe kushitaki kwa nini inavunjwa?

Je, Itajiandamanisha kupinga kwa nini inavunjwa?

Au ni kwa namna gani hao wavunja katiba watashughurikiwa ikiwa Watanzania hawajui kudai haki zao na kama wakijua, sana sana wataandamana Mitandaoni na kudai haki hizo Mitandaoni?
 
Haiwezi kwani yanayopiganiwa ni maslahi ya wanasiasa pekee.
Kilichonishangaza kingine, ni kuona na kusikia MMK wa Chadema akisema, Katiba eti ni agenda ya nchi?

Alomdanganya hivyo ni nani Wakati wananchi wengi hawana habari na hicho kinachodaiwa ni agenda ya kiraifa, sisi tunaona ni kikundi kidogo tu tena ni chama kimoja pekee chadema ndio wanahangaika

Wameshindwa hata kuviunganisha na kuvishawishi vyama vingine pinzani ili angalau kuonekane hako kasura ka kitaifa ka uwongo na kweli
 
Wanao taka Katiba mpya wote wanataka Katiba itakayo wapa urais kwenye ushindani na sio sababu ya wananchi ndio mana ukiangalia CHADEMA, CCM, NCCR, ACT na wengine wengi kila siku wanaivunja Katiba yetu wazi wazi
 
Wanao taka Katiba mpya wote wanataka Katiba itakayo wapa urais kwenye ushindan na sio sababu ya wananch ndiomana ukiangalia chadema ccm nccr Act na wengine wengi kila siku wanaivunja Katiba yetu wazi waz
Siyo kweli. Tupo ambao hatuna vyama lakini tunaona lililojema na lisilojema.

Kwa katiba hii tutakuja kumpata dikteta mwingine aivuruge nchi kuliko hata jiwe. Katiba hii inalea ujinga wa kujipendekeza kwa rais kuogopa kutumbuliwa. Haijengi uwajibikaji bali unafki.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kilichonishangaza kingine, ni kuona na kusikia MMK wa Chadema akisema, Katiba eti ni agenda ya nchi?

Alomdanganya hivyo ni nani Wakati wananchi wengi hawana habari na hicho kinachodaiwa ni agenda ya kiraifa, sisi tunaona ni kikundi kidogo tu tena ni chama kimoja pekee chadema ndio wanahangaika

Wameshindwa hata kuviunganisha na kuvishawishi vyama vingine pinzani ili angalau kuonekane hako kasura ka kitaifa ka uwongo na kweli
Tunawetaka katiba mpya lakini sio hiyo wanayoitaka wao ya kuwaingiza ikulu kufanya biashara.
 
Ni kweli kwamba kwa katiba hii ya sasa tutakuja kupata rais wa hovyo ambaye Magufuli hataona ndani.

Eti katiba ya nchi inakuwa na ibara fulani fulani zinazosema "Kama ikimpendezea Mheshimiwa Rais". Hiyo sio katiba.. ni waraka fulani ya kihuni tu.
 
Kilichonishangaza kingine, ni kuona na kusikia MMK wa Chadema akisema, Katiba eti ni agenda ya nchi??

Alomdanganya hivyo ni nani Wakati wananchi wengi hawana habari na hicho kinachodaiwa ni agenda ya kiraifa, sisi tunaona ni kikundi kidogo tu tena ni chama kimoja pekee chadema ndio wanahangaika

Wameshindwa hata kuviunganisha na kuvishawishi vyama vingine pinzani ili angalau kuonekane hako kasura ka kitaifa ka uwongo na kweli
Ila kipindi rais Kikwete anafanya mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya kwa kutumia pesa nyingi za walipa Kodi ndo ilikuwa agenda ya nchi??
 
Siyo kweli. Tupo ambao hatuna vyama lakini tunaona lililojema na lisilojema.
Kwa katiba hii tutakuja kumpata dikteta mwingine aivuruge nchi kuliko hata jiwe. Katiba hii inalea ujinga wa kujipendekeza kwa rais kuogopa kutumbuliwa. Haijengi uwajibikaji bali unafki.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Alafu mkuu Kuna Jambo linanishangaza akionekana mtu kudai katiba basi Ni CDM na anayepinga Ni CCM huu umekuwa ujinga mkubwa sana
 
Kwa mujibu wa katiba rais ni kama tu Mungu wa nchi

Na hiyo imefanya mihimili yote kuwa chini yake

nadhani viongozi wa hii mihimili wanatokana na rais pia kwahiyo mambo Meusi yanayofanyika huko yana baraka za Mungu wa nchi kwa hiyo hilo shtaka utalipitishia wapi

Rais hana hofu ya kuvunja sheria
Anatoa order tu
Maelekezo kutoka juu
Sasa hii inawahakikishia usalama hawa viongozi wa huku chini na wao wakiwa na mambo yao binafsi yanayoenda kinyume na sheria hawana hofu kwa kuwa ni wanafamilia tu wa bwana mkubwa.

Nguvu ya kumshtaki mkuu wa wilaya tu utaitoa wapi kwenye mahakama gani kesi hiyo itapita.

Yote hii ni katiba tupunguze mamlaka ya rais kupitia katiba hawa viongozi wengine wapatikane kwa njia nyingine isiyohusiana na connection na rais. Na rais ashtakiwe akienda wrong.

Mihimili ijitegemee na rais ashtakiwe hii itasaidia, kesi zitakuwa nyingi tu tofauti na unavyofikiri wewe

Lakini lengo la kubadili katiba siyo hili tu la kuwapunguzia madaraka na kushtaki watu hapana. Lakini kumbuka pia lengo la katiba ni kupunguza madaraka ya viongozi wa serikali ambao ni CCM.

CCM wewe na wenzio hamko tayari kwa hilo kwa namna yoyote ile kwa kuwa madaraka yakipungua hamtakuwa na uhakika wa kulindana na kubaki na madaraka ndiyo mana mnakuja na hoja dhaifu kiasi hichi hapa.

Hoja yenye mashiko hamna.

Jambo dogo tu, tuangalie uchaguzi uliopita ni zao la katiba tulio nayo ndiyo maana tunafikiria kuibadilisha, kuachana na hayo mengine yote hoja na hitaji la katiba mpya ni uchaguzi uliyopita wewe unaongeleaje uchaguzi uliopita ni sahihi kwa kilichotokea?

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Ndiyo na ni ukweli kabisa, Katiba tunayojaribu kuitafuta kwa jasho jingi na Energy nyingi, nasikitika kusema, haitatusaidia popote kama nchi.

Kama kuna mtu anapingana na mimi, Embu atusaidie kujibu maswali haya
Hayo ni mawazo ya wana CCM ambao kula kwao, kuvaa kwao na kuendesha maisha yao hapa dunian wanaitegemea CCM hawataki kupoteza fulsa lkn katiba mpya ni lazima tutaidai kwa nguvu zote.
 
Kwa mujibu wa katiba rais ni kama tu Mungu wa nchi
Na hiyo imefanya mihimili yote kuwa chini yake
nadhani viongozi wa hii mihimili wanatokana na rais pia kwahiyo mambo Meusi yanayofanyika huko yana baraka za Mungu wa nchi kwa hiyo hilo shtaka utalipitishia wapi
Mkuu suala hili linapaswa kuwa agenda ya taifa maana ishatumika pesa nyingi katika mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya ila leo unashangaa mtu anasimama sio agenda ya wananchi ukimuuliza tume ya jaji warioba ilitumika kukusanya maoni kwa wananchi wa nchi gani mpaka wewe unasema sio agenda ya wananchi hana jibu

Kuna baadhi ya vitu Kama taifa watu tunapaswa kushikamana imefika wakati mtu kupata haki yake Mpaka kiongozi fulani aumue huu ni ujinga Kama taifa tunapaswa kupinga vita ujinga maana hata Baba wa taifa aliona mbali kusema ujinga ni miongoni mwa maadui wa taifa
 
Hayo ni mawazo ya wanaCCm ambao kula kwao,kuvaa kwao na kuendesha maisha yao hapa dunian wanaitegemea CCm hawataki kupoteza fulsa lkn katiba mpya ni lazima tutaidai kwa nguvu zote
Na huu ndo unatakiwa kuwa msimamo wa taifa katiba ni hitaji la nchi sio hisani ya kiongozi fulani kuamua kitu hata nicha kijinga basi Kiko sawa hapana
 
Back
Top Bottom