Ndiyo na ni ukweli kabisa, Katiba tunayojaribu kuitafuta kwa jasho jingi na Energy nyingi, nasikitika kusema, haitatusaidia popote kama nchi.
Kama kuna mtu anapingana na mimi, Embu atusaidie kujibu maswali haya
Ni kweli tumekuwa na katiba isiyokidhi matakwa yetu hususani katika mizania ya kisiasa, kwa maana, katiba iliyopo, ilitungwa chini ya Chama kimoja, hivyo kuvifanya vyama vingine kukosa uhalali wa kulindwa na katiba hii tuliyonayo
Kingine, Katiba hii iliyopo, inamfanya Rais wetu kuwa mfalme, ni kama yeye ni mtu wa kwanza na wa mwisho, kwa lugha ys kiyunani, ni Alfa na Omega, n.k
Sasa basi, Ukisikiliza kwa umakini, wengi wa wanaharakati wetu kwenye majukwaa ya kisiasa na majumkwaa mbalimbali mbali, Utasikia wakisema, Tunataka katiba itakayotuwezesha kuwaajibisha wote wanaovunja katiba
Ni jambo jema, maana mtu yeyote anayediriki kuvunja makubaliano yetu na katiba yetu , ni sawa na matusi kwa watu woote kama taifa
Tumeshuhudia katiba yetu ikivunjwa waziwazi na baadhi ya viongozi wetu,
Bahati mbaya ni kwamba, kuna waliovunja katiba hata kwa wale ambao, katiba hailindi ouvu wao kama ilivyo kwa Maraisi wa nchi, lakini wanapovunja, Hasira zetu tunazielekeza kwa kiongozi mkuu, tunamsagia meno, Wakati huohuo, Katiba yetu mbovu tuliyonayo, ni kumlinda Raisi wa nchi na maovu yote kipindi awapo madarakani, na kwamba Hawezi kushitakiwa kwa kosa lolote awapo madarakani
Na bila shaka, shida yetu inaanzia hapo
Okay, Achilia mbali makosa ya Rais kwa mjibu wa katiba mbovu tuliyonayo kwamba, hatoshitakiwa kwa makosa yoyote aliyotenda akiwa madarakani, Hili tunaweza kusema, lipo juu ya mamlaka ya kawaida ya mwananchi kumwajibisha Raisi wao kwa kuwa katiba inamlinda
Upande wa pili kwa kosa hilohilo la kikatiba, Tumeshuhudia Bunge lisilo halali, Ni bunge ambalo wabunge wenginewe waliomo humo bungeni si wabunge halali kwa mjibu wa katiba za vyama vyao pia kwa mjibu wa katiba ya nchi, kwamba hawana uhalali wa kuwa wabunge kwa kuwa, hawatambuliki na vyama vyao na katiba haitambui mtu wa aina hiyo kuwa sehemu ya bunge
Sasa basi
Nionyesheni ni wapi ambapo huyo mkuu wa mhimili huu wa Bunge alipohalalishiwa na katiba hii mbovu tuliyonayo kwamba naye hawezi kuwajibishwa,
Je, sasa, ni nani wa kumwajibisha?
Ni kwa nini tunataka katiba mpya, Je, ni nani atakuwa mbadala wetu wa kusimama na kuwawawjibisha wote wavunja katiba?
Je, katiba hii mbovu ilipokuwa ikivunjwa, ni nani anafahamika ambaye yeye anapaswa kudili na wavunja katiba yetu? Je, alifanya kazi yake?
Na kama alishindwa kuwashughurikia hao waharifu wa kikatiba, Ni kwa vipi anadhani itakuwa rahisi kuwashughurikia kukiwepo katiba mpya?
Ni nani asiyejua kwamba, Watanzania, Watanzania kwao ni wazuri wa kuhamaki mitandaoni pekee ila nje ya hapo ni watu wanafiki na wapole kama maji ya mtungi? na ndiyo maana hata Asiyelindwa na katiba aweza kuvunja katiba na ikawa salama?
Mkinionyesha atakayekuwa zamu ya kuwashughurikia wahalifu wa kikatiba badala yetu, ndipo nitakubali kwamba, Tunataka kweli katiba na tumemaanisha
Katiba haijilimdi, haijipeleki mahakamani, haiandamani na wala haimtishi mvunja katiba, Nionyesheni mlinzi wa katiba
Tanzania hoye?