Nasikitishwa na uhusiano wetu na Kenya, unaumiza wakulima na wafanyabiashara

We unaeandika utumbo huu ni mkulima au umejiskia tuu uandike!!?
Unajua shida tunayoipata sisi mipaka ikifungwa mbeha wewe!!?

Alafu nmekumind kishenzi yaan.
Achanane tu huyo anafurahisha mdomo wake, hapo hata kulima tu nusu eka ukute ajawai
 
Wewe ni mkulima ama unaongea tu? Unafahamu shuruba na gharama za kilimo? Unajua bei za pembejeo na vibarua?? Hilo ni tatizo kwa mkulima hakuna mfano jamaa wakibana wakulima msimu ujao wa mavuno twafa!
 
Ni kweli, serikali ilitazame suala hili kwa mapana yake. Kwa kuongzea tu ndugu mleta mada, suala hili halijawaathiri tuu wafanyabiashara Bali hata sisi wakulima.
Hivi Sasa gunia la mahindi Katavi linauzwa kwa Elf 35000 badala ya 80000 Kama zamani. Mwaka Jana wakulima waliitikia vizuri wito wa Mh Rais kuchapa kazi. Basi serikali itusaidie kwa kuweka mazingira mazuri/ kututafutia solo la mazao hayo.
 
Bwana kwa sababu ukitoka kucheza pool table na kubet unakuta chakula kwenye hotport una haki ya kuongea haya. Lakini kwa wale tunaoshinda maporini uko tukilima tunajua madhara yaliyoko mbele yetu. Hoja kwamba tutauza nchi zingine nayo ni kujipa matumaini tu. Sijui kama una kumbukumbu vizuri mwa 2017 tulihangaika kutafuta soko la mahindi hadi yakaharibikia ndani. Kwa kipindi hicho tumbo lako ulimwazima nani? Unakumbuka kilichowakuta wakulima wa Mbaazi ? Bei imeporomoka kutoka 3,000/= hadi TZS 200/= kwa kilo. Korosho mnakumbuka pia kilichotokea? Kwahiyo tusijipe matumaini. Hali itakua mbaya. Ni kilio kwa wakulima wa mahindi.
Musimu huu soon tutauza gunia la kilo 100 kwa elfu 20, imagine umelima ekari moja kwa sh laki moja na ishirini, umepanda mbegu kilo kumi kwa ekari, una walipa watu wa kuhudumia shamba, na wastani wa ekari moja ni gunia 15. ACHENI USHABIKI KUNA WATU WATAUMIA.
 
Fuatilia hotuba ya JK akilihutubia bunge la kenya wakati akitoa salamu zake za kuwaaga majirani zetu kenya, yule aliyetabiliwa na JK kwamba anaweza kuja na akaharibu mahusiano Kati yetu tayari yupo ikulu ya TZ"
 
Awamu hii kila mjinga anaishauri Serikali cha kufanya na bahati mbaya sana ushauri huo unasikilizwa na kukubalika zaidi kuliko wa Watalaamu. Waganga wa kienyeji wanashauri dawa bora za mitishamba, huyu nae anashauri mbegu zilizitumiwa na Mtwa Mkwawa ndo zitumike badala ya zile zinazoboreshwa mara kwa mara. Mbegu hizo za mahindi za kuvuna magunia matatu kwa eka bado zipo na Wakulima wengi bado wanazitumia siyo kwa sababu anazotoa huyu mjinga bali ni kukosekana kwa uelewa. Mabeberu hawatumii mahindi kwa chakula wala hawalimi sana mahindi ingawa wanatumia sana kama chakula cha mifugo kwa hiyo hawawezi kutumia raslimali zao na wakati kuboresha mmea ambao ni mgeni katika mazingira yao. Watalaamu wetu wanajitahidi sana na wanafanikiwa kuboresha hizo mbegu asili ili mkulima avune magunia 40 kwa eka ili apate chakula cha kutosha familia na ziada wauziwe wengine pamoja na mabeberu wakalishe mifugo yao. Magonjwa ya mimea, wanyama hata ya Binadamu yapo tu na mapya yanaendelea kujitokeza kama Changamoto ya kupumua na vita ya kuyaangamiza ni endelevu kwa juhudi za Watalaamu wetu na mabeberu.
 
Pamoja na kutopinga kila uliloandika, lakini nakuomba ujielimishe kwanza ili ujue tatizo kwa kina zaidi ya hivyo unavyodhani.

Hapa unaona upande mmoja tu wa Tanzania, umejaribu kutazama na huko kwingine mchango wake katika tatizo ukoje?

Kwa sasa nakupa hiyo 'homework' fupi kwa kuanzia.

Ukitaka tutalijadili hili kwa kina chake.

Na ifahamike, sijatetea makosa ya serikali hii kama yapo, naitetea Tanzania tu.
 
Mi natamani mpaka wetu na kenya ufungwe kabisa,tusihusiane kabisa yan..hawa wakenya si wenzetu kama si tunavyowachukulia..anyway,jamaa wanaumia sana na lile bomba la hoima,
 
kwa hivyo wewe unaona ni sawa wananchi wa pande zote waumie kwa sababu ya UJINGA wa viongozi wao?!.

kumbuka hao maviongozi mshahara na posho zao ziko palepale!.
Sasa kwanini usilaumu ujinga wa viongozi wa Kenya?
 
Kosa la Magufuli kwenye hili ni nini?

Kwamba uhusiano na Kenya siyo mzuri?
 
ww fala kilimo cha tz wateja wetu wakubwa ni kenya
mipaka ikifunguliwa gunia la mahindi linauzwa hadil 120k na sometimes wanalifata hap hapa
tangu wafunge gunia linacheza 30-50k
Sasa hapa unamlaumu nani? Waliofunga si wakemya kwamba hayo mahindi yenu yana sumu? Selikali ya tz kosa lake liko wapi?
 
Acha ujinga maana hata tuta la viazi huna. Leo Rukwa na Katavi mahindi gunia 30000 na mengine yanakomaa shambani. Tunapigwa pin ya soko unasema viongozi wako siyo wajinga!? Viongozi gani unaoongelea? Hawa wanaojali posho za vikao kuliko ustawi wa wakulima!?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…