Nilitamani kuanzisha uzi kuhusu hili suala lakini nashukuru kwa bandiko hili maana limelenga kile nilichotaka kusema.
Binafsi nimekuwa mdau wa kilimo kwa muda mrefu sana, kuanzia kulima mpaka kushiriki makongamano mbalimbali yanayohusiana na sekta ya kilimo na kuna hoja kadhaa ambazo wakulima wamekuwa wakizitoa kwa Serikali lakini kutofanyiwa kazi na hii sasa ndio majibu yake, japo inabidi kutafiti zaidi kama kweli Kenya wanasema ukweli au ndio VITA YA KIUCHUMI.
Hoja kubwa ambayo imekuwa ikitoka mara kadhaa ni kuhusu suala la mbegu, wadau wameshauri mara nyingi turudi kwenye mbegu zetu za asili maana hizi tunazoambiwa za kisasa zina changamoto nyingi sana, mojawapo ni hii ya kushambuliwa na wadudu hali inayopelekea wakulima kutumia madawa mengi sana ili kuweza kulinda mazao yao, na hili nimelishuhudia kwa macho yangu, sasa kwa hali hii tutajiteteaje kwamba mahindi yetu hayana sumu?
Wakulima watanielewa vizuri kwenye hili,
Na hapo nimeongelea madawa kwenye mahindi pekee, rudi kwenye nyanya, matikiti nk, huko ndio usiseme, dawa inayomwaga huko huwezi amini kwamba inaingia tumboni kwa binadamu.
Mimi nashauri wadau wa kilimo wasikilizwe, ianzishwe bank ya mbegu zetu za asili kuliko kutegemea hizi za kisasa tunazoletewa maana wakati mweingine kuzitunza ni ngumu sana kwasababu ya kushambuliwa na wadudu.
Halafu kama hatuwaamini Mabeberu ( Bill Gates) kwenye chanzo za COVID kwa nini tunahamasisha wakulima wetu watumie mbegu zao, Rejea matumizi ya mbegu zilizofanyiwa GMO huku nako kuna madhara mengi zaidi.