Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Nilitabiri humu na ikawa kweli kuwa Wagombea wakuu wa uchaguzi mkuu wa Rais mwaka huu ni Wakili Msomi mwenzangu Tundu Lissu (Upinzani/CHADEMA) na Dr. John Pombe Magufuli (CCM). Ni katika andiko langu hili: Uchaguzi 2020 - Utabiri wangu 2020: Ni Dr. John Pombe Magufuli (CCM) na Wakili Msomi Tundu Antipas Lissu (Upinzani) Urais. Tuwafuatilie; tuwachambue na tuwachague!. Katika andiko langu hilo, niliahidi mgombea wa kusimama naye katika kuelekea uchaguzi mkuu huu.
Wengi wetu tunajua kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeshakamilisha uteuzi wa wagombea wa Urais. Pia, tunafahamu kuwa kampeni za Urais zinaanza leo ambapo CHADEMA watazindua kampeni zao Mbagala, jijini Dar es Salaam. Kesho itakuwa zamu ya CCM kuzindua kampeni zao huko jijini Dodoma. Wapo wagombea wengi katika ngazi ya Urais. Lakini, Dr. John Pombe Magufuli, Rais wa sasa wa Tanzania na mgombea wa CCM pamoja na Wakili Msomi Tundu Antiphas M. Lissu wanabaki kuwa wagombea wanaofuatiliwa Zaidi.
Ndiyo kusema, katika ngazi ya Urais, mchuano mkali utakuwa kati ya wagombea hao wawili. Kama mtanzania wa kawaida, mfuatiliaji wa siasa na nisiye mwanachama wa chama chochote cha siasa hapa Tanzania na kwingineko, nawiwa kusimama na Dr. John Pombe Magufuli, mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM. Naahidi kumuunga mkono katika kampeni zake atakazozianza kesho na kumuombea kura pale itakapobidi kwa nafasi yangu. Sababu za kumuunga mkono nitazieleza katika siku zijazo humuhumu JF zikichagizwa na yatakayosemwa kwenye kampeni.
#Nasimama na JPM kwa miaka mitano mingine!