Uchaguzi 2020 Nasimama na Dkt. John Pombe Magufuli, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM




Peter tumepingulua urafiki rasmi kuanzia leo!😣😣😣😣
 
Mkuu, anza na hili halafu nitarudi:Nani amewajazia 'kitaalamu na kiusahihi' wagombea wa CCM? Inaruhusiwa kujaziwa fomu za kugombea?
 
Mkuu wanaccm tunachagua chama,hayo Mambo ya sera sijui nini ni secondary kwetu
Mkuu Magufuli anabebwa na silka yake, mwaka 2015 kipindi vikao vinaendelea pale Dodoma Kila mtu alitega sikio kujua nani atapewa kijiti kupeperusha bendera ya chama Cha CCM, binafsi kipindi hicho nilikuwa dilema! Sikujua Nani naweza kumpa kura yangu zaidi ya Dr. Slaa, lakini nafsi yangu nikisema Lowasa siwezi kumpa ata Membe siwez kumpa kura yangu!

Matokeo yakatangazwa pale ukumbi wa Jakaya Kikwete na JPM akashika usukani! Kwakweli sikuitaji kusikia sera wala maneno ya ziada cos CV ya Magufuli kwenye utendaji kazi naikubali Sana, nikaamua pasi na shakha kuwa Dr. Magufuli anaenda kupata kura yangu na kweli nilimpa kura yangu.

Watu huwa wanafanya mamuzi pale mgombea anapojulikana tu ila Kuna watu wanasubiri sera na hapa wapo wachache Sana ila pia wengine hufata mkumbo Kama mtu kujaza watu wengi viwanjan wakati wa kampen nao uhunga mkono hapohapo, hapa ndiyo Kuna kundi la vijana.
 
Usichoke mivyeo bado iko mingi
 
Kwasababu sheria ni taaluma ya makidai. Wao ndio wanajiona wamesoma kuliko watu wote. Wanasema katika kila fani/taaluma kuna aspect ya sheria

Bora wanajiita hivyo, unajua unaweza kujiita kitu chochote.

Kuna vitu wanafanya unabaki na maswali mengi.

Kupika kura ni haki yavkila mwenye vigezo. Lakini tunaambiwa kura ni siri. Mtu kumpenda au kuungana na mgombea sio tatizo ni haki yake, lakini ni siri yako unabaki nayo wewe.

Izingatiwe kampeni ndio rasmi zinaanza leo kwa wagombea kuanza kujinadi majukwaani, huyu anayejiita wakili msomi hata hajataka kusubiria asikilize wanasemaje wagombea ameshachagua upande huku akimalizia maamuzi yake yatazingatia kitakachosemwa, seriously?
 
Kura za upinzani zimeshagawanywa kwa wao kwa wao. Ccm itashinda maeneo mengi nafikiri mpaka level ya uraisi.

Hizo barabara ziandaliwe tu.

Hii hoja ya kura za upinzani kugawanyika huwa siielewi elewi sana kama chama kinakubalika kinakubalika tu ni kufanya kampeni na kujiamini tu huko kujifanya kuungana na hizo CCM B ndo kuzidi kujipoteza ni vema vyama serious vikasimsma vyenyewe na kujipigania badala ya kusema kura zinagawanyika hata za CCM pia zinagawanyika pia mbona kuna majimbo ya ubunge wapinzani huwa wanashinda bila hata ya wapinzani kuungana.
 

Achana naye huyu ana njaa Kali..lazima alambe makalio
 


TANZANIA HAKUNA UCHAGUZI KUNA UCHAFUZI NA NDIKO TUNAKOELEKEA KONGO MPYA HII
 
Upo sahihi, ila jiandae kuoga matusi na tuhuma kuwa ''umenunuliwa''.
Wakudadavua mlimuaminisha Mzee kuwa ni yeye tu, vyama vingine vimekufa . Sasa hila zote kwa wapinzani za nini kama kweli vyama vyao vimekufa ?!

Kutekana, kukimbia ofisi, mapingamizi ya kubumba , kunyang'anywa fomu, kuwekana ndani nk . Yoote haya ya nini kama upinzani umekufa !!
 
Nina matatizo makubwa sana na tabia za Magufuli, ila ninakubaliana 100% kwa misimamo yake kutetea maslahi ya kitaifa, na vile vile nina matatizo makubwa sana na busara za lissu ingawa nakubaliana naye 80% kuwa inabidi sheria zifuatwe.
Tatizo lenu mnadhani ccm ndio Taifa yani kuilinda ccm na bunduki ndio kulinda Taifa? hebu kuweni serious
 
Hapa at least ulisema jambo!!! Sio kwa hizo thread ulizoleta hapo juu ambazo hukukemea lolote!!!

Sasa kwa haya uliyoyasema mwaka 2017??? How comes unam support mgombea wa hicho chama na hicho Chama kwenye uchaguzi huu???? Au kwa sababu kipindi hichi kabudi hakuwepo kwenye ulaji????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…