Nasimama na Mkuu wa mkoa wa Dar, kutukumbusha kuwajibika

Sio kweli mkuu
Hata kama, kuchangia gharama za kujifungua haipaswi kuwa jambo la kupigia kelele
Sasa tutawezaje kupinga rushwa za rasimali zetu, ikiwa hata mtu unashindwa kuchangia elfu 50 ili mkeo ajifungue
Mkuu usitetee ujinga serikali yetu imezidi kutowajibika ipasavyo we hujui tu!, hili swala mimi ningekuwa ndo rais namuondosha huyo mkuu wa mkoa napia naenda kwenye hiyo hospital ana kwa ana nione wanakwama wapi mpaka wanakosa vitu basics kama hivyo!, hospital mnakosa gloves fungeni sasa mkalale tujue hakuna huduma!.. mkuu hivi we unajisikiaje majority of people wanategemea hospitali za serikali, hii haijalishi uwe tajiri ama maskini halafu private vitu vipo ila government vitu hakuna!. swala ni uwajibikaji tu!.
Msitetee ujinga badilikeni fikra hizo!.
 
Mweny akili timamu anajua ni laZima
1. Tuwajibike Kwa afya hasa ya uzazi ya mkeo
2. Elimu ya mwanao
Tusijitoe akili
 
Watu wanapitia Mengi kama wewe umebarikiwa hongera sana
Hayo matatizo najua yapo
Ila nasema wale wana uweZo na wanapuuza kugharimikia afya za uzazi za wake zao au elimu ya watoto, watabisha hadi kesho
 
Watu wanalipa kodi! Jana nimenunua umeme wa 5k wakakata VAT 750 sasa hii hela inaenda wapi?

Gloves gani zinauzwa 50k?
Watz wana vichwa vigumu kwaiyo umedhani gloves kweli n 50k.
Kuna huduma za kulipia ikiwepo na gloves sio gloves peke yake
 
Hayo matatizo najua yapo
Ila nasema wale wana uweZo na wanapuuza kugharimikia afya za uzazi za wake zao au elimu ya watoto, watabisha hadi kesho
Ila basi tu, halafu mtu kamtia mtu mimba wala hawazi haudumii chochote
 
Huo ndio ukweli Wabongo wanapenda mserereko sana.
Mzee wa kuropoka leo kaongea ukweli
 
Sitetei serikali ila napinga mazoea ya dezo Kwa wananchi
Me naona kiasi cha elfu 50 mtu kuchangia huduma ya kujifungua sio jambo la kupigia kelele
 
Ila basi tu, halafu mtu kamtia mtu mimba wala hawazi haudumii chochote
Kweli kabisa
Mimba ni process na maandalizi
Imeingia hadi miezi 9 huna pesa ya tahadhari hata elfu 50
Ila misiba na harusi unachanga kujionyesha Kwa watu
 
Mtu anaeshindwa kulipa hata gharama kidogo ya kuwezeshwa kujifungua salama huyo anakuja kuongeza idadi ya masikini
atataka na mtoto watu wamlelee bure
 
Watu wanalipa kodi! Jana nimenunua umeme wa 5k wakakata VAT 750 sasa hii hela inaenda wapi?

Gloves gani zinauzwa 50k?
Hebu acheni utani hata ungelipa 7500 Vat ambayo ni mara 10 ya hio uliosema na Watanzania wote wakalipa hadi kitoto kichanga kinachozaliwa leo haitoshi kulipa mishahara tu ya wafanyakazi wa Uma kama waalimu, madaktari nanwengineo wanaokusaidia kila siku.

Hela zote zinazokusanywa nchi nzima hata isipoibiwa hata sh 10 hazitoshi ku cover budget yetu.

Watanzania hatutaki kuwajibika, ni ukweli mchungu ambao watu wengi hawataki kuusikia, mtu yupo radhi achangie harusi ama akanunue Nguo nzuri ila kuchangia maendeleo hawataki.
 
Watu wanalipa kodi! Jana nimenunua umeme wa 5k wakakata VAT 750 sasa hii hela inaenda wapi?

Gloves gani zinauzwa 50k?
Gloves Surgical kwa Ajili ya Kupima Mjamzito Zinatumika Kwa uchache sana Kuanzia 6 , Kuna Receiver ya Kumpokea Mtoto, Kuna Baadhi ya Vifaa ambavyo Ni disposable (Hutumika mara Moja) jumla ya Vyote ni Zaidi ya 50k Ila Unaombwa Uchangie 50k tu..

Hapo kwa Gloves kila Surgical Moja huwa ni 2500 sasa Piga Hesabu 6 Ni Kiasi gani?
Ni kama 15k kwa Gloves peke yake bado vifaa Vingine Vya PPE na Hata Vingine..

Mimi Nafanya kazi karibu sana Na Madaktari na Wauguzi wanaozalisha Maana mimi Ni daktari wa watoto..

Na Ninamuona mtu anayetake Risk Kugoma Kununua Vifaa Kwa ajili ya Kujiokoa Mwenyewe Hana Akili
 
Sitetei serikali ila napinga mazoea ya dezo Kwa wananchi
Me naona kiasi cha elfu 50 mtu kuchangia huduma ya kujifungua sio jambo la kupigia kelele
Kuna vitu napigia kelele hapa ni uwajibikaji na pia kauli ya huyo mkuu wa mkoa!.

ndugu huwezi kuona tofauti mpaka ufatilie mambo ndo utakuja kuelewa, swala sio hiyo 50000, swala ni uwajibikaji hata mimi siwezi muacha mama kijacho wangu kisa hiyo 50000 nitatoa ili apate huduma lakini tunakila sababu ya kuhoji kwanini serikali haiwajibiki ipasavyo kama sisi tunavyowajibika kulipa kodi..?

Mi nafikiri waafrika ndio maana kuna vitu vingi sana vinatushinda kuendesha kwasababu tunachukulia simple sana vitu!.
Hivi unahabari unatakiwa uwe na maelezo yakutosha kitendo tu chakujibu kitu hakipo halafu kwenye mali ya umma..?! sijui kama unalitambua hilo!.
Ningekuwa kiongozi ningetumia hili jambo kuwafundisha kimatendo halafu ndo mngeelewa hivihivi ni kama kupiga gitaa kwenye masikio ya mbuzi!.
 
Kulipa Kodi ni jukumu
Ila piga hesabu serikali inalipa mishahara kiasi Gani Kwa watumishi wanaotuhudumia?
Unakanyaga rami, miradi mingine n. K
Kuchangia serikali ilipokwama mbona tunaona sio wajibu
Yaani hospital, wauguzi na wakunga serikali imekuwekea Bure hadi kuchangia elfu 50 ya vifaa simu hadi Kwa Mkuu wa mkoa
 
Unaweza kuwa na 1M ukatae kulipia 50k mkuu?
...
Watanzania walio wengi tunaishi maisha ya kubangaiza hata mlo tunakula ili tusife sio kula kujenga mwili, tunachangia kwa kulipia kodi bidhaa tunazonunua na njia nyinginezo.
...
Kwako 50k ni ndogo na unaona ni kutowajibika. Anyway angalau hio gharama ingepunguzwa na kuwa 20k for benefit of majority
...
Kuchangia ni muhimu(wengine tusipoombwa tunatoa kama shukrani mke kasaidiwa kajifungua salama), na pia RC katumia lugha isiyokubalika
...
Maoni yangu:
-Gharama ipunguzwe isiwe 50k iwe angalau 20k
-RC awajibishwe kwa kutumia lugha isiyofaa
-Gharama zote za kujifungua na watoto chini ya miaka mitano zijumuishwe kwenye bima za CHF
-Watoe matumizi ya neno "bure" hamna cha bure labda mvua,jua,na hewa tunayovuta, badala yake waseme gharama nafuu
Asante!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…