Nasimama na Mkuu wa mkoa wa Dar, kutukumbusha kuwajibika

Gharama za kujifungua ni elfu 50?
Ndo ukilipa Kodi usinunue nepi ya mtoto, soksi, gloves, usinunue kitabu cha mtoto wa shule, usilipe pesa ya tuition ya mwanao,
Tuwajibike, ujamaa ulidumaza tunawaza kuhurumiwa na kusaidiwa tu
 
Chalamila anawambia ukweli
Tatizo ukweli ni machungu
Tuwaze mbali huwezi kuuza uduvi na nguvu unazo ukatoboa
Kwanini kijana una nguvu upate wazi la kuuza uduvi hiyo biashara ya mabibi
Usiwe na mtazamo finyu.Mvuvi anayeutoa baharini huo uduvi,wanaouanika,mpaka wachuuzi wake wote ni wauza uduvi!
Ni KAZI halali na watu wanaendesha Maisha yao na familia zao kwa Kazi hiyo!
Kuhusu kutoboa,ni jambo la mtazamo binafsi dhana ya kutoboa ni Pana.
Mwingine akijenga Nyumba ndio anaona ametoboa,mwingine akinunua gari,mwingine pikipiki,mwingine shamba,nk!
Kila mtu ana mahitaji na malengo yake,na namna yake ya kuyafikia!
Kuuza uduvi kunaweza kuwa Daraja la kukupeleka kumiliki bucha ya kuuzia samaki!
Acheni dhihaka na Maisha,heshimu anachofanya mtu.
 
Gharama za kujifungua ni elfu 50?
Ndo ukilipa Kodi usinunue nepi ya mtoto, soksi, gloves, usinunue kitabu cha mtoto wa shule, usilipe pesa ya tuition ya mwanao,
Tuwajibike, ujamaa ulidumaza tunawaza kuhurumiwa na kusaidiwa tu
Kama unalipa kodi huduma muhimu zinatakiwa ziwe bure hasa kwa watu wenye kipato kidogo. Wewe utakuwa mdogo sana. Sisi tuliosoma shule za msingi kuanzia 80-90 tulikuwa tunapewa hadi madaftari bure. Chakula shuleni bure hii hadi sekondari. Hospitali matibabu bure na dawa zilikuwepo. Leo hii kodi inakusanywa nyingi(wenyewe ndio wanatoa hizi takwimu) lakini hata kuwapa wajawazito huduma haiwezekani? Unatetea uozo watu wanatumia mabilioni kila mwaka kununua magari huku hela ya dawa na gloves atoe mgonjwa? Kama unatetea hii jifikirie mara mbili.
 
Kama daraja la kukufikisha mahala sawa
Nadhani RC alimaanisha wale walioridhika na hiyo biashara
Usikae miaka 10 unauza uduvi
 
Kwa hiyo hela zinazopelea wewe ndiye huwa unajazia, si ndiyo babu?
 
Mke ni wako
Mtoto akizaliwa unataka aitwe u bin wako
Kuchangia elfu 50 tu unaona unateswa
Sasa wewe utakuwa baba wa namna Gani?
 
ELIMU!!!

ELIMU!!!

ELIMU!!!

📌KUNA MIJITU INABEBA MIMBA IKIDHANI INAIKOMOA SERIKALI,KUMBE INAJIKOMOA YENYEWE😁😁


📌WATANZANIA WAHUBIRIWE UWAJIBIKIKAJI,NCHI HII MTU ANALALAMIKA MPAKA VITU AMBAVYO NI WAJIBU WAKE!!
 
MTU HUNA HATA ELFU HAMSINI,EBU WAPITISHE ROLL CALL WATU WASIO NA PESA WAFUNGWE VIZAZI HARAKA,TUMECHOKA KELELE ZA MASKINI.


#YAANI MASKINI YEYE KAZI KULA KULALA,KUZALIANA NA UHARIBIFU.
 
Mke ni wako
Mtoto akizaliwa unataka aitwe u bin wako
Kuchangia elfu 50 tu unaona unateswa
Sasa wewe utakuwa baba wa namna Gani?
Aidha wewe bado mtoto sana au una tatizo lingine kiasi hujui kuwa kuna watu hio 50k hawana.
 
Aidha wewe bado mtoto sana au una tatizo lingine kiasi hujui kuwa kuna watu hio 50k hawana.
Mkuu kuzaa ni mipango na sio ajali
Mwanamke anapata hedhi, mnahesabu tarehe
Unakojoa shahawa
Unajua baada ya miezi 9 hili sio la kukwepa
Sasa iweje ujiandae mwaka mzima uwe huna Elfu 50?
Huo ni upumbavu na kutojali
Hawa watu kwenye masherehe ndo wako kwenye kama kuchangia
Wanabeti
Sikukuu wanaokula nyama
Bia mtaani zinanywewa
Ila kuchangia elfu 50 unaona kama umeombwa million
 
Sawa.
 
Tunalipa Kodi Mkuu... Huduma za afya na elimu bure Tena zenye kiwango inawezekana ...... Basi tu Kuna miamba michache imeamua isiwe hivyo.
 
Mkuu wa mkoa hiyo kwake ni kama 50 ya sarafu au haoni nivya mtu kushindwa kulipa yule Mzee alikuwa anajua mpaka mtz wa kawaida anakula nn ..... Afanye nini kumgusa legacy yake itaishi sana
 
Tunalipa Kodi Mkuu... Huduma za afya na elimu bure Tena zenye kiwango inawezekana ...... Basi tu Kuna miamba michache imeamua isiwe hivyo.
Jiongeze huduma za afya haziwezi kuwa Bure
Haya umekuta hospital ipo, Dokta yupo, wauguzi, na wakunga, vitanda
Bado unataka serikali ikununulie nepi, chupi, beseni, gloves, nyembe, kanga na vitenge, taulo laini, chakula lishe cha mzazi Bure
Tusipende dezo
 
Mkuu wa mkoa hiyo kwake ni kama 50 ya sarafu au haoni nivya mtu kushindwa kulipa yule Mzee alikuwa anajua mpaka mtz wa kawaida anakula nn ..... Afanye nini kumgusa legacy yake itaishi sana
Changia huduma za kujifungua acheni kupenda dezo
 
Nenda hospital kaone masikini na mimba zao ndo uje useme hayo kuna mtu hana hatq mia
Huna hata mia unazaa ili umleaje mtoto.
Watu wa ivo ni wajinga tu na sio kwamba wanakosa 50k kwa ajili ya mtoto wao.
Mkuu wa mkoa kajibu vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…