Hakuna historia ya mtu mzima wakati wa utoto wako kutaka kukufanyia molestation ukiwa mdogo na sasa ile worst memory inakurejea?!
Sababu kuna watoto unakuta chini ya umri wa miaka 10 kuna ndugu bazazi alikuwa akilala nae usiku alikuwa anamchezea sehemu za siri au kumfanyia vitendo vya kingono, kwa mtoto hayo mambo kama aidha alihisi au aligundua anafanyiwa ila sababu ya utoto alishindwa kuelewa nini kinaendelea then akiwa mkubwa ile fikra au kumbukumbu ya lile tukio huwa inakuja tena na kutaka kufanyiwa clarification yaani ufafanuzi wa nini kilikuwa kinatokea na iwe fikra mtambuka na sio fikra tu isiyo na maana.
Hebu jaribu kukumbuka, enzi za utoto wako, someone hakukuwahi kukufanyia vitendo vyenye sexual intent ndani yake?! Jaribu kukumbuka ndugu, jamaa, rafiki yaani mtu yoyote wa utotoni ambaye kwasasa ukikumbuka tukio mojawapo unashindwa kuelewa lilikuwa ni tukio la aina gani ila kwako kwa sasa ni tukio la mashaka sana.
Hebu kumbuka, jaribu sana kukiuliza kichwa chako kinakukumbusha nini kilichowahi kukukuta.