Nasumbuliwa na Jinamizi hili kila nikilala naomba Msaaada na Ushauri

Ungekuwa Muisilam ningekushauru kabla ya kulala uchukue udhu yaani utawadhe then ungeswali laka 2 ulale,hapo unakumbatiwa na Maraika mpaka asubuhi,nani atakugusa
Sasa hao malaika wakiwa midume balaa si ndo litaongezeka..... Nao wanaweza wakakolea wakataka mzigo.....
 
Jinamizi sio uchawi.
Ipo kisayansi. Ukilala kuna muda hewa haifiki vizuri kwenye ubongo. Unashindwa hata kunyanyua mguu au mikono ilihali fahamu zako zipo sawa .

Angalia jinsi unavyolala . Jaribu kuacha kutumia mto kwa muda lala kama nyoka
 
Ukilala weka kipande cha mkaa kidogo tu kwenye mto wako utakao ulalia au mchagoni, Au weka mfupa wa mnyama nguruwe arimaarufu kitimoto kwenye uvungu wa kitanda chako hutaona takataka hizo huu sio uchawi lakini.
 
Tatizo kama lako liko kwa wengi,ingawa wanaona aibu kuelezea. Lengo la uchawi huo ni mikosi ya kufilisi ili uishi kimaskini hata kama una kipato kizuri.Utatuzi ni njia mojawapo kati ya hizi: 1. Kumwomba Mungu kwa muda wakutosha kabla hujalala, angalao lisaa 1 kila siku mfululizo bila kuruka. 2. Uwe unatumia chumvi ya mawe kuogea asubuhi na jioni kila siku, bila kuruka. Tatizo lako ni la muda mrefu, kwa hiyo tumia hata miezi mitatu. 3. Kuna njia ya dawa za miti shamba zipatikanazo maduka ya dawa za asili. Kanunue unga wa miti hii 4 size ya robo kilo kwa kila mti: mwembe pori, msungwa,moyo mmoja na mfagio wa chuma. Uchanganye unga huo wa miti 4 kwa pamoja. Utakuwa unaogea mara 2,asubuhi na jioni na kujifusha mara 1 jioni. Hii utafanya kwa siku 21. Chagua njia mojawapo ya kutibu tatizo lako kati ya hizi 3.
 
 
Pole sana kwa tatizo hilo, mimi pia ninalo kwa mda mrefu sana, najua kwa.sehemu kubwa linahusu ushirikina. Wachawi wanapenda kuchezea roho na akili za watu wasio na hatia.
 
Hujawahi kutafuta pesa za majini, hujawahi kukuacha mwanamke akakuambia atakuonyesha? Inakuwaje unalala mchana mpaka unaota
 
Mkuu njoo pm, tafadhali
 
Ndugu mm nataka niseme na ww cha kwanza usijibishane na coment za watu wajinga wanaotoa ushaur wa kukudhihak pil tafuta mafuta ya mzaituni OG km upo dsm yanapatikana msikiti wa mtoro yale nyunyuzia ndani kwako na uwe unaogea hiyo ni kinga tosha kwa wachawi na majini na mapepo, cha tatu km ww ni muislam bhas soma suratul Yatul-qurusih hii silaha hatar san kwa viumbe vibaya cha mwisho kabisa kuwa na Imani zingatia huu ushaur wangu hizo ndoto zitakoma
 
Nimejitahidi sana kwenda mkuu. Inaniumiza sana kwa kweli,
Me nakushauri ufanye toba ya kweli, Mungu akutakase halafu Sasa ufanye maombi ya kukataa hayo majini mahaba ikiwezekana funga kabisa mlilie Mungu atakusikie hiyo hali haitokurudia tena.

Ukiona umeombewa imeshindikana, jiombee mwenyewe mradi uwe na imani kwamba Mungu anasikia usiseme hujui kuomba, hayohayo maneno utakayo tamka jua Mungu anasikia na atakujibu. Amen
 
Pole sana mwanajamii mwenzetu kwa changamoto inayokukuta. Hili tatizo wengi limewakuta, kuna jamaa yangu kipindi tupo JKT hali hii ilikuwa ikimtokea mara kwa mara, kwa kweli alikuwa ni mtu mwenye mawazo muda wote. Ila nakumbuka alishauriwa aogee maji ya chumvi ya mawe. Pia Kuna mtu alimshauri akiwa anaenda kulala ajipake unga wa mkaa katikati ya makalio. Nafikiri njia hizi zilimsaidia kwani hakulalamika tena na hadi sasa hivi anadunda.

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Popo bawa huyo ingia mtaani umtangaze kuwa anakupiga bakora za kimkakati ukinyamaza kimya ataendelea kukutafuna maana ataona unamfichia Siri kwahiyo atajua unampenda
 
Asante kwa taarifa na ushuhuda mkuu. Sikujua hivi visa vya kishetani vinawakuta wengi! Thanks
 
Pole sana kwa tatizo hilo, mimi pia ninalo kwa mda mrefu sana, najua kwa.sehemu kubwa linahusu ushirikina. Wachawi wanapenda kuchezea roho na akili za a mkuu.
Sikujua hivi visa vya kishetani vinawakuta watu wengi! Pole sana mkuu.
 
Sijawahi kuishi mazingira ya kufanyiwa molestation . Nimekuwa katika mazingira yenye afya ya kiume na hali hiyo sijawahi kukumbana.
Hivi vitu ni vya kishetani nimekumbana navyo ukubwani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…