Siku ya jana, kiongozi wa kidini, Boniface Mwamposa akiongozwa na rais wa Tanzania, Samia Suluhu amezindua hema la kisasa na kubwa la thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 15 za kitanzania.
Kumbukumbu zinaonyesha, miaka kadhaa nyuma, Boniface Mwamposa aliwahi kusimika hema kubwa kiasi katika viwanja vya King George Memorial (lililopo soko kubwa lisilo rasmi sana la Mitumba mjini Moshi) ili kuwapata waumini ambao ni wateja na wauzaji wa mitumba mjini Moshi. Lakini kwa sababu, wachaga wengi ni wajanja wajanja na wezi wakubwa wakamshtukia mapema na mwitikio taratibu ukapungua mpaka kukosa kabisa waumini na Mwamposa kuamua kulitelekeza mazima na kutimkia zake Dar mahali alipo sasa.
Lile hema la Moshi, liligeuka kuwa pagale, likajaa majani, uchafu, kichaka cha wanyama wadogo kujifichia, 'watu kujisitiri' na huenda shughuli zingine haramu kufanyika faster faster nyakati za usiku
Kwa kuwa anachokifanya Mwamposa kidini kimekaa kitapeli mnoo, ujanja ujanja na wizi wizi, uendelevu wake sio wa uhakika, maana kadri muda unavyokwenda mbele, vichwa vya waumini wasaka mafanikio ya chap chap vitazidi kufunguka na wengi kusepa taratibu na wakati huo huo washindani wake wakizidi kumporomoa.
Ni suala la muda tu, natabiri hema lake jipya hapo Kawe (Tanganyika Packers) litakosa waumini, kupwaya na taratibu kugeuka kuwa gofu.
Muda ni mwalimu mzuri sana.