Kwanza kabisa, niseme mimi si mtetezi wa Magufuli wala CCM. Ni mtetezi wa haki na mchambuzi wa siasa na mantiki.
Magufuli nishamsema sana, hivyo, ninachoandika hapa si kwa sababu ya kumtetea Magufuli.
Twende kwenye hoja baada ya dibaji hiyo.
Magufuli ameshasema mara kadhaa hataki kuongeza muhula wa urais.
Kwa nini mnafanya hili suala kuwa hoja?
Hususan kama kuna makosa mengi sana ambayo Magufuli ameshayafanya ambayo yanaweza kujadiliwa kama hoja halali, factually, na si speculation?
Mimi naona wapinzani wa Magufuli kuongelea hili kunaonesha yafuatayo.
1. Hawana focus. Wanakuwa kama mtu tajiri mwenye hela nyingi sana (wana hoja nyingi sana halali za kumsema Magufuli) lakini ambaye bado anaenda kukopa hela benki kwa riba kubwa sana (licha ya kuwa na hoja nyingi halali za kumsema Magufuli, wanaenda kukopa hoja ambayo haina uhalali ya kuhusu makosa ambayo hayajafanyika,kiasi cha kufanya watu wahoji umakini wao).
2. Hawajadili mambo kwa facts. Bali kwa speculations.
3. Wanahukumu kosa ambalo wanafikiri litatetendeka, badala ya kuhukumu kosa lililotendeka. Hili ni jambo hatari. Kwa msingi huu, Magufuli anaweza kuamka siku moja akasema ameota waponzani wanataka kumpindua. Akawafunga wote.
4. Wanapoteza muda na nguvu kujadili speculations wakati kuna mambo muhimu ya kubana sasa hivi kama wizi wa kura katika uchaguzi, tume huru ya uchaguzi, katiba mpya etc.
5. Wanaonesha paranoia. Kitu ambacho hakifai katika uongozi.