Nilikueleza, ni-'address' mimi na siyo hao unaowaingiza kwenye mjadala ambao umekushinda kuuchangia na sasa unaingiza maneno yasiyosaidia chochote kama hayo ya "kelele, kijinga" n.k.
Sijui kama unaelewa kiasi ulichojifunua wewe ni mtu wa aina gani kutokana na uliyochangia katika mada hii.
Nakuchanganya wewe na watu wengine wanaofikiri kama wewe kwenye kundi moja.
Kusema kwamba mjadala wa kumjadili mtu mmoja si muhimu, tunahitaji mjadala wa kubadilisha mfumo kuna tatizo gani?
Kusema kwamba, hata mkimzuia Magufuli kujiongezea muda, hamjamzuia kupachika kibaraka wake na kuongoza kwa remote control kuna makosa gani?
Siasa za Afrika zinazunguka katika personalities.
Tunaangalia watu, badala ya mfumo.
Na kwa siasa hizi, mtatawaliwa sana.Mkiendelea hivi, mtapigwa hata 2025, hata 2030.
Maana Magufuli msiyemtaka ataondoka bila kuongeza muda, lakini atapokewa na "Magufuli" type mwingine atakayeendeleza kuangalia interests za watu wachache.
Sasas hapo napo mtashangilia mmemzuia Magufuli kuongeza muda wa urais?
Mchezo mnaocheza ni mchezo wa kushindwa.
Kwa sababu, hata mkifanikiwa, bado mmeshindwa.
1. Magufuli akiongeza muda wa urais, mmeshindwa, kwa sababu ataendeleza uozo wake.
2.Magufuli akishindwa kuongeza muda wa urais, akamuweka kibaraka wake au mtu mwingine wa CCM akaja kuchukua nchi - kitu ambacho bila kubadili katiba/ tume ya uchaguzi ni wazi kitatokea tena- bado mtakuwa mmeshindwa, kwa sababu atakuja mtu mwingine wa CCM atakayeendeleza ujinga wa kila siku wa CCM.
You are playing a lose-lose game.
Whatever the outcome, you lose.