Hao wapambe mbona walikuwepo tangu utawala wa Nyerere.
Nyerere alitoa hotuba moja akasema kila alipokuwa akitaka kujiuzulu, wapambe wakawa wanamuambia, Mwalimu, usituache, taifa linakuhitaji sana.
Akawa anaongeza miaka mitano, anasema hii ya mwisho.
Ikiisha, wapambe wanamwambia "Mwalimu, usituache, taifa linakuhitaji sana".
Mwisho akastuka. Akagundua kwamba issue si kwamba taifa linamuhitaji.
Issue ni kwamba hao wapambe walikuwa wanamuhitaji kwa faida zao binafsi. Walikuwa hawajui rais anayekuja atakuwa nani na atakuja na watu gani.
Akawakatalia, akajiuzulu.
Kwa hiyo hizi kelele za wapambe zipo tu.
Lakini je, rais mwenyewe anataka nini?
Rais kashasema hataongeza muda.
Na hakuna factual evidence kwamba ataongeza.
Ni speculations tu.