Natabiri jaribio lolote la kubadilisha Katiba na ukomo wa Rais litaibua mazito

Natabiri jaribio lolote la kubadilisha Katiba na ukomo wa Rais litaibua mazito

Kwa kweli hata mimi nampinga Magufuli kwa mengi sana, lakini katika hii hoja nasema kweli naiona ni hoja dhaifu sana.

Kwa sababu.

1. Magufuli ameshasema haongezi muda.Wapinzani wake wanataka nini zaidi?..
Magufuli hatobadili katiba hii, bali ataleta mpya (May be ile ya Chenge) ambayo inamruhusu hata yeye kuanza upya!, Maana mkiwa na katiba mpya saa inakuwa reset, nyote mnaanza upya kwa sababu ile ya zamani haifanyi kazi tena.
Do you get the point?
 
Hata kama humuamini Magufuli, unatakiwa kutomuamini kimantiki.

Ama sivyo, unaweza kubakia unajadili speculations za ajabu..
Tulishajibizani juu ya hili huko nyuma, na tunarudia yale yale tuliyokubaliana kutokukubaliana.

Kuna "kutomuamini 'kimantiki'" zaidi ya ushahidi uliopo kuhusu matendo yake yanayoonekana, au mantiki hiyo inahusu vitu gani?

Kuna sababu maalum juu ya huu ubishi mbali ya kuaminisha watu kwamba "Magufuli is a village bumpkin"; na hiyo ndiyo iwe 'credential ya kuonekana kuwa hatetewi.
 
Kwanza kabisa, niseme mimi si mtetezi wa Magufuli wala CCM. Ni mtetezi wa haki na mchambuzi wa siasa na mantiki.

Magufuli nishamsema sana, hivyo, ninachoandika hapa si kwa sababu ya kumtetea Magufuli...
Sorry ina maana hata nyakati kusoma hujuwi? Basi poa asante
Mkuu TumainiEl japo hata kidogo ukiri Kiranga kakujibu kwa hoja nzito badala ya kumwuliza swali la kitoto kama hilo.

Nami nasisitiza, kama wafuasi wa upinzani humu JF na mitandao mingine ya kijamii, mnahitaji upinzani imara nchini, mwanze kuwashambulia viongozi wenu. Ndani ya hivyo vyama vya upinzani kuna ombwe la upinzani. Viongozi wanaongozwa na maslahi binafsi.

Mnatia aibu kila tatizo la ndani ya vyama mnasingizia CCM na Serikali. Kuna ushahidi wa kutosha kuhusu hoja yangu hiyo, km:
√ kusambaratika kwa CUF;
√ Madiwani na Wabunge wa CHADEMA kuhama;
√ kususia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, 2019;
√ matokeo mabaya katika Uchaguzi Mkuu, 2020;
√ sakata la uteuzi wa wabunge wa viti maalumu; na
√ sasa waja na hoja ya kubadili Katiba ili muda wa kikomo cha Urais uongezwe.
 
Tulishajibizani juu ya hili huko nyuma, na tunarudia yale yale tuliyokubaliana kutokukubaliana.

Kuna "kutomuamini 'kimantiki'" zaidi ya ushahidi uliopo kuhusu matendo yake yanayoonekana, au mantiki hiyo inahusu vitu gani?

Kuna sababu maalum juu ya huu ubishi mbali ya kuaminisha watu kwamba "Magufuli is a village bumpkin"; na hiyo ndiyo iwe 'credential ya kuonekana kuwa hatetewi.

Magufuli kafanya nini kinachokufanya ufikiri atajiongezea muda?

Facts please.

Taja kitu specific cha kuonesha ushahidi Magufuli anataka kuongeza muda wa urais. Sio speculation. Fact.

Habari za kuiba kura, kuminya upinzani hazi qualify kwa sababu hizo hazina specificity kwenye kuongeza muda wa urais.

Zaidi, kwa nini tunamjadili mtu badala ya kujadili mfumo?

Magufuli asipojiongezea muda, akamuweka kibaraka wake awe rais aendeleze mambo yake, awe mbaya kuliko Magufuli, mtaona sawa?

Hamuoni kwamba ku focus kwenye kutaka rais huyu asijiongezee muda kuna distract habari kubwa zaidi ya kupunguza madaraka ya rais (yeyote yule), mabadiliko ya katiba, tume huru ya uchaguzi etc?
 
Magufuli kafanya nini kinachokufanya ufikiri atajiongezea muda?

Facts please...
Wafuasi wa upinzani huleta habari za vijiweni, udaku na umbea tu. Kamwe hawajadili mawazo (ideas) sana sana ni matukio
 
Kwa kweli hata mimi nampinga Magufuli kwa mengi sana, lakini katika hii hoja nasema kweli naiona ni hoja dhaifu sana.

Kwa sababu..
Wenzetu kweli mna imani zimejaa mpaka mnazitumia ovyo..

Mtu ambaye leo anasema maendeleo hayana chama kesho anasema sikuleta maendeleo sababu mlichagua upinzani, alafu huyohuyo unamuamini akitoa kauli..???

Mtu anayesema hadharani hakuna kufanya siasa mpaka kipindi cha uchaguzi ,wakati katiba inaruhusu na aliapa mbele ya jaji mkuu na wananchi huku kashika kitabu cha Mungu kuilinda katiba hiyohiyo..???

Aiseeee ......
 
Wenzetu kweli mna imani zimejaa mpaka mnazitumia ovyo...

Wewe ndiye unasema Magufuli atajiongezea muda kwa imani.

Nimeomba fact iliyo specific kwenye kuongeza muda, hujaleta.

Unaleta habari za ukandamizaji wa kawaida wa kila siku wa Magufuli.

Unaelewa kwamba Magufuli anaweza kuwa kigeugeu, anaweza kuwa kaongoza wizi wa kura 2020, anaweza kuminya upinzani, lakini asijiongezee muda wa urais? The former does not necessitate the latter.

Kwa nini unataka kumhukumu mtu kwa kosa ambalo hajalifanya, unalobashiri atalifanya 2025, wakati ana makosa ambayo kashayafanya 2020 tayari?

Magufuli akisema haongezi muda wa urais, na asipoongeza kweli, lakini akamuweka kibaraka wake awe rais anayefuatia, na huyo rais akawa mbaya kuliko Magufuli, utaona sawa? Utafurahi?

Kwa nini tunajadili mtu badala ya kubadilisha mfumo mzima ili rais yeyote asiweze ku abuse presidential powers?
 
Hilo shairi la Jadakiss ni fasihi, sasa kama huelewi fasihi, kuelewa ni vigumu.

Hapa kuna mambo mawili...
Nanukuu " Sina uhakika kama kuna MTU atayaendeleza haya baada ya Mimi"
"Tuna kaz ndogo Tu tukiletewa mapendekezo yakubadili katiba na kuongeza ukomo wa Rais"
Hili soko litaitwa Ndugai?
"MTU anaye faa Kuwa sipika atakuwa Ndugai"
"Upinzani kufutwaa bungeni"
Mwisho tunamaliza KAZI. Watanzania Wana akili Sana sema niwaugwana.
 
Nanukuu " Sina uhakika kama kuna MTU atayaendeleza haya baada ya Mimi"
"Tuna kaz ndogo Tu tukiletewa mapendekezo yakubadili katiba na kuongeza ukomo wa Rais"
Hili soko litaitwa Ndugai?
"MTU anaye faa Kuwa sipika atakuwa Ndugai"
"Upinzani kufutwaa bungeni"
Mwisho tunamaliza KAZI. Watanzania Wana akili Sana sema niwaugwana.
Bado hujatoa fact inayoonesha Magufuli ana mkakati wa kutaka kuongeza muhula.

Mimi nakuwekea habari, imetangazwa dunia nzima. Magufuli kakataa kutaka kuongeza muda.



MON AUG 7, 2017 / 12:14 PM EDT

Tanzania's Magufuli rejects calls to extend rule beyond two-term limit

Fumbuka Ng'wanakilala

DAR ES SALAAM (Reuters) - Tanzanian President John Magufuli on Monday rejected calls from some of his supporters to extend his rule beyond the constitutional limit of two, five-year terms, bucking a trend in the region.
Several leaders including Uganda's President Yoweri Museveni, Rwanda's Paul Kagame and Burundi's Pierre Nkurunziza have all tinkered with or defied their constitutions to extend their rule.

"It's impossible. I will respect the constitution," Magufuli told a public rally in the coastal Tanzanian town of Tanga after a member of parliament from the ruling CCM party called for an extension of his rule to at least 20 years.

"I have sworn to defend the constitution ... I shall play my part and pass on the leadership reins to the next president when the time comes."

Tanzania, one of sub-Saharan Africa's most stable democracies, has held five relatively peaceful multi-party elections since 1995, all won by the ruling party.
Magufuli was elected in October 2015 for his first term and he has not indicated whether he will seek re-election at the next polls in 2020. But if he does and wins, he would then be ineligible to contest the vote in 2025.

Some opposition leaders say there is a shadow campaign being carried out by Magufuli's supporters to find ways of prolonging his rule beyond the two terms.
Former president, Ali Hassan Mwinyi, from the ruling CCM party, who himself served only terms in 1985-1995, first publicly raised the idea in June.

"If it wasn't for term limits, I would have suggested that Magufuli should be our president for eternity," Mwinyi told a cheering crowd in Tanzania's commercial capital Dar es Salaam at the time.


Nicknamed "the Bulldozer" for his strict leadership style, Magufuli has won praise from some Western donors for his tough anti-corruption fight.

Opponents, however, accuse him of cracking down on dissent and limiting democratic space. He has denied the allegations, saying he was not a dictator.
The drive to root out corruption has felled ministers, the head of government's anti-graft body, the tax chief and thousands of civil servants.

(Reporting by Fumbuka Ng'wanakilala; Editing by Elias Biryabarema and Alison Williams)
 
Natabiri yakuwa jaribio lolote la kubadili katiba na kurefusha ukomo wa Rais litazuwa Moto wa kisiasa ambao haukuwahi kutokea tangu kuwepo kwa Taifa hili.

Yani hamtoamini wala kudhania. Itakuwa ni siku mbaya na nzito kwa Taifa ndipo sote tutaamini kweli kuna deep state in side state.

Nasali Jambo hili lisitokee wala kusemwa tu. Madhara yake yatatutesa sana kama Taifa.

Mungu ibariki Tanzania.
Wewe Tumaini weww!
 
Yes.

Nimeandika hayo sana kama umenifuatilia hapa.

Haya mambo sikusikia kwenye hotuba tu...
Unafikiri dawa ya kutibu hili gonjwa ni nini? Gonjwa la wapambe kutaka rais aendelee na hasa hili la wateuliwa kufanya sarakasi nyingi za hovyo (ambazo baadhi hata rais mwenyewe hazijui, wanajipendekeza).
 
Umetumwa kuja kusoma upepo? Amalize mi5 yake, aondoke!

Akiona yafaa arudi aombe ubunge.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Magufuli kafanya nini kinachokufanya ufikiri atajiongezea muda?

Facts please...
"Speculation"?
Ni 'facts' zipi zinazokufanya wewe uamini hatajiongezea muda? Ziweke hapa tuzione.

Mtu akija kwako akope halafu asilipe, keshokutwa anakuja tena kukulaghai juu ya 'favor' nyingine unaendelea kuamini kwamba mtu huyo ni 'dependable na kumtimizia matakwa yake bila kuwa na wasiwasi wowote juu yake, wewe utakuwa na sababu zako za kuamini ushawishi wake huo mpya.

Ili kukuonyesha kwamba madai yako ya kutokuwa mtetezi wa Magufuli kama unavyojitambulisha hapa ni msisitizo wako wa lawama kwa watu wanaoonewa na huyo unayemtetea.

Unatafuta 'specificity' gani kwa kiongozi asiyeamini kabisa kwamba kuna katiba inayomzuia asifanye mambo kivyake tu bila kuikiuka; kuna jambo gani gumu zaidi ya mtu kufanya mambo anavyoona mwenyewe nje ya katiba?
Halafu watu wanakuja hapa kutetea mtu huyo huyo kwamba hawezi kamwe kufanya aonavyo inampendeza yeye wakati atakapojisikia kufanya hivyo.

Unakazania hizi 'specificity' na 'speculation', hebu tuonyeshe za kwako unazoona kwamba huko kusema kwake kwamba "hataongeza muda' zinazokufanya ukubaliane na hadaa hiyo.

Uchaguzi uliofanyika, hukusikia akisema utakuwa "huru na wa Haki"? Hizi 'specificity' zako zikoje?

Ni ku'speculate', kusema kwamba Magufuli aliahidi uchaguzi kuwa "Huru na wa Haki", hata kama haikuwa hivyo? Hiyo sio "fact"; unataka 'fact' ya namna gani hiyo?
 
Natabiri yakuwa jaribio lolote la kubadili katiba na kurefusha ukomo wa Rais litazuwa Moto wa kisiasa ambao haukuwahi kutokea tangu kuwepo kwa Taifa hili...
Kwa hali hii tuliyofikia ya kupora hata haki ya raia kuchagua kiongozi anayemtaka; lolote lile linaweza kufanyika. Tusubiri kuona.
 
Wenzetu kweli mna imani zimejaa mpaka mnazitumia ovyo..

Mtu ambaye leo anasema maendeleo hayana chama kesho anasema sikuleta maendeleo sababu mlichagua upinzani, alafu huyohuyo unamuamini akitoa kauli?...

Busara ikuelekeze kupata tafsiri sahihi ya hiyo kauli sikuleta maendeleo sababu mlichagua upinzani.

Upinzani gani ushirikishwe wakati unadai ni maendeleo ya vitu. Hivyo ilikuwa sahihi kuambia wapiga kura kuchagua maendeleo ya vitu au ya watu (kinadharia - hata wahusika wasiweze kufafanua)
 
Kwanza kabisa, niseme mimi si mtetezi wa Magufuli wala CCM. Ni mtetezi wa haki na mchambuzi wa siasa na mantiki.

Magufuli nishamsema sana, hivyo, ninachoandika hapa si kwa sababu ya kumtetea Magufuli...
With all due respect, the issue here is: He is not reliable. He promised 50m to every village, he promised a fair and free election, he promised and sworn to entirely uphold the constitution; but all in vain. It is very difficult through these examples, for a sober and normal mind to believe to all what he says.
 
Back
Top Bottom