Nasikia sauti ktk moyo wangu ina niambia kuna jambo lasiri sana linaendelea ktk siasa za Tanzania...
Jambo hili hata mimi sijuwi ila yatupasa kuliombea taifa kwa machoz na dam.
Mtikisiko ulio ikumba dodoma sasa unaenda kuwa mtikisiko mkubwa zaidi kwakuwa serikali inaongozwa kwa siri na wengi hufa na siri zao...
Basi tuliombee taifa.
Epuka kuongea au kumsuta mwenzako ukijuwa unaye msuta hujuwi kama vile wewe hakujuwi.
Nawaona wana kijani wanaongea sana nakudhani kuanguka kwa Ndugai ni fursa ila nataka niwaambie huu ndio mwanzo wa utungu....
Yapo mambo hatuyaoni ila sasa yataonekana.
Yapo mambo hatujuwi ila sasa yatajulikana.
Wakati haya yanaendelea mataifa yenye nguvu duniani yanafuwatilia kwa ukaribu kile kinaendelea ktk siasa za Tz.
Pray for Nation. Amen
Mwaka 2008 Tanzania ilishuhudia ikiandika historia ya waziri mkuu wake kushurutishwa bungeni kujiuzulu kwa kashfa mbalimbali. miaka kumi na tatu baadae mihili miwili katika nchi inasigana wazi wazi hadharani tena kwa jazba na viashiria vya vitisho dhidi ya upande mwingine ambao uliamua kunywea. Ombi la kusamehewa hadharani lilitolewa lakini upande wa pili ulikataa wazi wazi tena hasira zikijidhihirisha bayana.
Shinikizo likatoka upande wa mhilimi tendaji kwenda kwa mhimili jamii kuachia ngazi.
Mhimili jamii umeachia ngazi, kumbukumbu katika historia imeandikwa tayari kwamba mhimili mmoja katika nchi ya Tanzania ulishinikiza mhimili mwingine kuachia ngazi na kwa kuzingatia ulivyo na nguvu mhimili jamii ukatii na kuondoka ukabaki mhimili tendaji na mhimili haki kwa muda.
2022-2023 ni bayana mhimili uliojichimbia chini unaweza kung'oka kutoka kwenye shinikizo la jamii yenyewe.
Mhimili haki kimya, ukisusua katika utendaji wake na inawezekana una jambo lakini kwa kuwa ni watu wanaozingatia mfumo wa kisheria hawataki kuonekana wakikwaruzana na mhimili wowote lakini moyoni wana jambo zito sana hasa kwa kusukumiwa kuamua mambo tete na mtego wa kuaharibu mahusiano ya mihimili.
Kitakachojili na kwa kuwa ufalme ulipo ni mchanganyiko wa chuma na udongo na kwa kuwa jua limeruhusiwa na mwenyezi Mungu kumulika mwanga wake kwenye uso wa dunia kunahatari ya kupoteza............
Viongozi wanashauriwa waache kulipiziana visasi kwa mambo binafsi wanayopingana wenyewe
Mfano ajitokeze hadharani jaji mkuu ambaye ndiye mwenye dhamana ya mhimili kisha akasema kuna baadhi ya kesi hazina mashiko ya kisheria ila kwa matakwa ya mhimili tendaji wanalazimika kwenda nazo kwa shingo upande, je kesho itakuwa salama kwake?
NAKUBALIANA KATIBA IFANYIWE MABADILIKO ili iondoe mianya ya kuonea iwasio na nguvu za kidola.