Natabiri tena mabadiliko madogo Baraza la Mawaziri

Sawa mpendwa Nabii na mtume
 
Sasa mbona na wewe unatabiri? Janja janja tu kama Januari Makamba
 
Wewe hubahatishi siku zote 👍👍👍
 
Huna utabiri wowote ww muhuni. Hayo ni mambo obvious. Ni sawa na kutabiri kuwa mwaka huu watazaliwa watoto wengi wa kike na kiume.
 
Mabadiliko anayofanya Samia hayana faida yeyote kwetu mkuu,so ajiachie tu.Angemuondoa Makamba,Nauye,Mwigulu na Kinana tungeona kafanya la maana,ilivyo sasa ajinyamazie tu.
 
Mzee Wasi anataka kurudisha hadhi na heshima ya wateuliwa ili wawe ni wenye uwezo na kuaminika mbele ya umma. Utu uzima ni dawa. Nakuaminia kwa utabiri wako huu mkuu.
 
MKuu huenda ukalamba shavu jipw moyo, umesubiri sana...hakuna asiyependa vitu vizuri😂
Msimfanye aache kutoa mada zenye michango mchanganyiko (mixed). Kuna kipindi anatoa mada mzuri
 
Hakuna cha utabiri, huyu anachoweza ni kuteua na kutengua kila siku badala ya kuleta maendeleo
 
Mkuu umeelezea point moja kwa kuigawa mara tatu

Umenena kweli lakini
 
Mamlaka ya uteuzi inakosa umakini kwenye kuteua Watendaji au mawaziri aidha kwa kushauriwa vibaya na washauri wake au kwa kutozingatia ushauri wa wataalam.Kiongozi huwezi kujua kila kitu, ndiyo maana unakuwa na wasaidizi.
Kiongozi Mkuu Kama ana washauri wabovu,inabidi wajitafakari.,wanmchafua kiongozi Mkuu.
-Lakini Kama kiongozi Mkuu hafuati ushauri wa wasaidizi wake,inabidi abadilike, Urais ni taasisi
-Zamani washauri wa kiongozi Mkuu walikuwa wanaandaliwa vizuri kwa majukumu yao.
-Siku hizi Sina uhakika Kama wanaandaliwa au wanapeana kwa kujuana badala ya kufuata weledi wao.
 
Mkiongea ndo kwanza anaweka pamba masikioni
 
Huu hauna sifa wala vigezo vya kuitwa utabiri Kwa sababu:
1.Mabadiliko ya baraza la mawaziri ni kitu Cha lazima Kwa hiyo kitu ambacho Cha lazima kukifanyia utabiri ni kudanganya.

2. Pili utabiri wako hauna time frame, ulitakiwa udokeze Kwa ufupi kwamba utabiri huu utakuwa ndani ya mwezi wa 10 hivi ungeeleweka.

3. Umekosa hali ya kujiamini. Utabiri unatakiwa uwe na kujiamini ndani yake. Kwa mfano ukisema kutakuwa na mabadiliko na kweli utabiri useme hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…