Natafuta Audio Clip ya zaidi ya Dk 5 ambayo Rais Samia anazungumza Kiingereza

Natafuta Audio Clip ya zaidi ya Dk 5 ambayo Rais Samia anazungumza Kiingereza

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Nitafurahi sana nikipata audio Clip ambayo itazidi dk 5 Rais wetu Mpendwa akichana mistari kwa kiingereza katika mahojiano au maelezo flani sehemu yoyote. Iwe imenyooka haijaungwa ungwa.

Nitafurahi sana. Tuachane na haya madai ya watu kuwa yeye huwa mara nyingi anasoma tu. Tunataka kuwaonesha watu kuwa hata amewahi hojiwa kwa English au akahutubia watu wa English.

Mpaka sasa ni Maraisi wawili tu wamewahi kuongea na Wasomi vyuoni. Mwalimu Julius K. Nyerere na Benjamini Mkapa. Hawa nimewahi wasikiliza. Kwa kweli tunahitaji miaka mingi kupata Marais Smart kama hawa wanaojiamini.

Mkapa hadi Midahalo alikuwa anakubali. Baada ya yeye hakuna ambaye amewahi kukubali midaharo.
 
Samia hata maneno ya kawaida tu ya Kiingereza hajui kuyatamka vizuri.

Hata akiwa anasoma bado anashindwa kuyatamka.

Ni wa kawaida sana kwenye hiyo lugha.

Na hayuko vizuri kwenye kuongea.

Ukiona mtu anadai Samia yuko vizuri kwenye Kiingereza basi jua mtu huyo naye hiyo lugha inampiga chenga.
 
Acha kutupa kazi ngumu kiasi hicho,tutapata wapi hiyo audio sasa

Sio SAMIA tu hata rais ajae baada ya huyu hatutokaa tupate rais anaekichapa fluently

labda huyo rais aanze andaliwa tangu akiwa primary,ila kama n hawa wanaoanza andaliwa

wakishafika bungeni kwa juhudi zao binafsi hilo jambo kama nchi n sawa tu na Tanzania kushiriki World Cup.
 
Nitafurahi sana nikipata audio Clip ambayo itazidi dk 5 Rais wetu Mpendwa akichana mistari kwa kiingereza katika mahojiano au maelezo flani sehemu yoyote. Iwe imenyooka haijaungwa ungwa.

Nitafurahi sana. Tuachane na haya madai ya watu kuwa yeye huwa mara nyingi anasoma tu... Tunataka kuwaonesha watu kuwa hata amewahi hojiwa kwa English au akahutubia watu wa English.

Mpaka sasa ni Maraisi wawili tu wamewahi kuongea na Wasomi vyuoni. Mwalimu Julius K. Nyerere na Benjamini Mkapa. Hawa nimewahi wasikiliza. Kwa kweli tunahitaji miaka mingi kupata Marais Smart kama hawa wanaojiamini.

Mkapa hadi Midaharo alikuwa anakubali. Baada ya yeye hakuna ambaye amewahi kukubali midaharo.
Ningependa kusikia audio clip yako ukiongea kiingereza japo kwa dakika 4 tu mkuu
 
Samia hata maneno ya kawaida tu ya Kiingereza hajui kuyatamka vizuri.

Hata akiwa anasoma bado anashindwa kuyatamka.

Ni wa kawaida sana kwenye hiyo lugha.

Na hayuko vizuri kwenye kuongea.

Ukiona mtu anadai Samia yuko vizuri kwenye Kiingereza basi jua mtu huyo naye hiyo lugha inampiga chenga.
Unaweza mlinganisha na mwendazake???
 
Back
Top Bottom