Natafuta Audio Clip ya zaidi ya Dk 5 ambayo Rais Samia anazungumza Kiingereza

Yaan huna hata uwezo wa kujenga hoja.Kama uwezo wako wa kujenga hoja ni mdogo kiasi hiki,ni heri ukae kimya. Elewa hoja zangu kama ifuatavyo:. 1.Tafiti zinaonyesha ,nchi nyingi zilizoendelea zimetumia lugha zao shuleni .Mfano China,Urusi,Japan,Uingereza ,nk. 2.Ili tuendelee tunahitaji kutumia lugha yetu.Wizara ya elimu ibadilishe sylabus zote kutoka kiingereza ziwe kiswahili.Maneno ya technology yabadilishwe yawe ya kiswahili.Tutapata taabu kwa muda mfupi Lakin watu watasoma na kuelewa vizuri.Kwa Sasa wengi wanakariri tu.Hawaelewi vizuri,kwa kuwa wanajifunza kwa kukariri tu kiingereza.Wangejifinza kwa kiswshili wangeelewa vizuri Sana.China,Japan,Korea,India,wameendelea kwa kutumia lugha za kwao.Sisi tumekamatwa na ukoloni ,hata akili zetu hazifanyi kazi kwa ajili ya ujinga na upumbafu mwingi.Yaan unasifia mtu kuongea kiingereza?Na Utaona ,mpaka ujinga ulikolea tukapewa mpaka majina ya wakoloni.Peter,Samuel,John,Patrick.Ikinga mtupu.Hatutaki vya kwetu.Masatu,Ngunagwa.Ni ngumu Sana kuendelea kwa ajili ya kupenda vya watu.
 
.Maneno ya technology yabadilishwe yawe ya kiswahili.
Sasa tulinza munkari wako nami nitulize wangu tuelimishane.

Unashauri tuibadilishe maneno ya teknolojia yawe kwa kiswahili. Teknolojia ya nani? Huoni kwamba tutaendelea kukariri zaidi?

Hao wanaotumia lugha zao wamepiga hatua kiteknolojia na hivyo Wana teknolojia zao. Wanatengeneza vyao, wanaviita majina ya kwao na wanawafundisha watoto kwa lugha yao.
 
Ondoa upumbavu kichwani mwako, lugha ni zaidi ya utamaduni. Lugha ni nyenzo ya mawasiliano, ndio maana unaona Umoja wa Ulaya wanatumia Kingereza japo wote sio waingereza na Uingereza haipo EU.
Umesema kweli tupu,na umemaliza mjadala.Ni ujinga kupenda lugha isio yako.Lugha ndio utamaduni wako,utapendaje utamaduni usio wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sahihi
Ni kwamba elimu yetu tunafundishiwa kwa kutumia english na hivyo english imekuwa ni kipimo cha moja kwa moja cha kiwango cha elimu ya mtu kwa maana kama kawa huwezi kuzungumza vizuri kiingereza tafsiri yake hukuwa unaelewa masomo darasani.
 
Lugha yeyote ile maana yake ni mawasiliano baina ya wanadamu, kama mnaelewana kwenye hiyo lugha mnayoongea inatosha hivyo hivyo !! Lugha ya kiingereza sio maana yake kusoma sana, wapo wengi tu wanaongea kiingereza kizuri lakini hawana elimu yeyote kubwa,
 
Hivi ni Mungu alitupa akili hii watanzania au tumejitafutia wenyewe ya kufuatilia raisi kama anaongea kiingereza kizuri au la.
Inasikitisha sana.
 
Hata waafrika wa nchi zingine za Afrika hatuoni wakifanya ujinga kama huu, ni ajabu sana kuhukumu uelewa na elimu ya mtu kwa kuangalia uwezo wao wa kuongea kiingereza.

Ni aibu sana.
 
Ila mimi sioni kama ni sahihi kwa sababu unaweza ukashindwa kuongea na kuandika vizuri ila ukaweza kusoma na kusikia kiingereza na hivyo ukaweza kupata maarifa yeyote yaliyo kwenye lugha ya kiingereza.
 
"Nitafurahi sana nikipata audio Clip ambayo itazidi dk 5 Rais wetu Mpendwa akichana mistari kwa kiingereza"πŸ‘‡πŸ‘‡

 
Hapo shida iko wapi? Toa makosa uliyoyaona then nikusaidie.
Is it grammatically correct to say ;

Thanks for the chance = hapo katafsiri kiswahili kwenda kingereza moja kwa moja.

Alipaswa kusema Thank you for this opportunity.

Vile vile hakupaswa kusema ;

Iam really aprreciate being here.

Alitakiwa kusema = i am thankful being here.
 
Wewe ndio upo zama za mawe, yupo sahihi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…