Natafuta mchongo wa Medical Doctor (MD)

Natafuta mchongo wa Medical Doctor (MD)

Mkuu, nilikupa kazi unayoomba huku, kabla hata ya kuanza kazi yenyewe ukaingia mitini. Sasa umerudi kuomba kazi tena?

Ujue utaratibu wa hivi husababisha watu wenye shida serious wasisaidiwe kwa hofu kuwa hakuna userious. Usiombe kitu kama hauko serious na unachoomba maana unawaharibia na wenzako wenye uhitaji serious waonekane ndio wale wale tu na wapuuzwe.
Ndio graduates wa leo hawa, vyeti vikubwa..skills hakuna+professionalism sifuri.
 
Kumbuka Messi ni muajiriwa pia
Sio kweli, wale wanatumia kipaji, na ndo mana ubora ukipungua kwenye kipaj husika lazima muhusika apoteane...., Ni vitu viwili pekee vinatajirisha watu 1.BIASHARA
2. KIPAJI
 
Huyo utakuta alitaka kusoma udaktari, akafeli, kwasababu wanachukua waliofaulu sana, wanataka division one kali, ndomaana inamuuma ana hasira na kuonea wivu madaktari.

Mtu mwenye akili timamu hawezi akadharau kazi za watu kiasi hicho.
Mi nawajua mandezi kibao wenye division 3 leo eti ni madaktari, Tanzania takataka kweli.
 
We utakuwa ulitaka kusomea udaktari ukapata maksi ndogo, hicho unachofanya ni psychological defense
Wala, mi mastaa, nina division 1 kali sana ni vile tumejificha kwenye ma id haya, wewe ndio unaonekana unapenda sana udaktari na nina hakika wewe shuleni sio ata mzuri.
 
Wapo, ndio wana tu misdiagnose kila siku
Kwa guideline ya TCU kwa sasa huwez kuingia kutoka form 6 kwenda kusoma MD ukiwa na Div 3...zamani walikuwepo ndio ila sio kwa sasa unless upitie Diploma na Div 3 yako then uje uingie MD
 
Kwa guideline ya TCU kwa sasa huwez kuingia kutoka form 6 kwenda kusoma MD ukiwa na Div 3...zamani walikuwepo ndio ila sio kwa sasa unless upitie Diploma na Div 3 yako then uje uingie MD
Huyo hajui anazungumza nini achana naye, huwezi kusoma udaktari Tanzania una division 3
 
Wala, mi mastaa, nina division 1 kali sana ni vile tumejificha kwenye ma id haya, wewe ndio unaonekana unapenda sana udaktari na nina hakika wewe shuleni sio ata mzuri.
Toa huo uhakika kuwa shuleni siyo mzuri, unanifahamu? Kwanza una ushahidi gani kuwa nilisoma?

Hakuna kazi ya kuajiriwa yenye mshahara wa maana eti ukawa tajiri, kwahiyo haina haya ya kudharau taaluma za wengine, kila taaluma ina nafasi yake.

Ipo siku utachungulia kaburi, utamhitaji huyo huyo daktari unayemdharau.
 
Mi nawajua mandezi kibao wenye division 3 leo eti ni madaktari, Tanzania takataka kweli.
NACTE wanataka uwe na D4 ujiunge na kozi za afya ya physics,chemistry,biology na D ya somo lolote isipokuwa dini mtu anaweza akawa na four ya 30 akaenda kusomea udaktari na akawamzuri, utakuta waliopata one na two wanabaki kushangaa tu
 
NACTE wanataka uwe na D4 ya physics,chemistry,biology na D ya somo lolote isipokuwa dini mtu anaweza akawa na four ya 30 akaenda kusomea udaktari na akawamzuri, utakuta waliopata one na two wanabaki kushangaa tu
Tofautisha Daktari ( Bachelor of Doctor of Medicine) na Tabibu ( Clinical Officer- diploma) usichanganye mambo hapa. Tukiongelea Daktari tunaongelea mtu wa Degree , sio watu wa Nacte huko matabibu.
 
Tofautisha Daktari ( Bachelor of Doctor of Medicine) na Tabibu ( Clinical Officer- diploma) usichanganye mambo hapa. Tukiongelea Daktari tunaongelea mtu wa Degree , sio watu wa Nacte huko matabibu.
labda huelewi kwamba CO anawezakuja kuwa MD kwa vigezo nilivyo vitaja
 
Back
Top Bottom