Akili Unazo!
JF-Expert Member
- Feb 18, 2009
- 3,930
- 4,912
Asante kwa kuwa muelewa na kama umelewa ungeondoa vigezo vyako na kuweka tangazo lisilo na Vigezo kwa kuwa Mke Mwema hawezi jitambuwa yeye bali hutambuliwa na muhitaji Mwanaume. Kabla wadada hawajakengeuka na hii mitandao na Ushauri wa Akina Joyce Kiria ilikuwa Mwanamme akikupenda kwanza anakukutanisha na Mama yake au Shangazi yake au Mtu yeyote wa Makamu katika mazingira ambayo hayajaandaliwa ili kujua tabia ya huyo Mtarajiwa, iwe katika kuwaheshimu watu asiowajua, au jinsi anavyoongea, na baana ya yote mrejesho hutolewa kwa Muowaji kuwa pale hakuna kitu na kweli ilikuwa hivyoooo na ukienda kinyume huyo Muawaji atajuta milele..Haya
Siku hizi Mwanamke ndiye anayeweka vigezo tena kwenye mtandao wakati maisha yake ni ya kustaajabisha na wengine tokea wakiwa wadogo Mkanisani hawaendi lakini umri ukienda ndipo anapoanza kujipendekeza kwenda kumuona mchungaji ili amuombee aondokane na upweke..
Khee nani kakudanganya...
Pole