Habari zenu ndugu zangu?
Naomba msichoshwe na heading ya huu Uzi, najua Kuna nyuzi nyingi za namna hii zimekwisha kuandikwa humu. Nimejaribu kutafuta msaada kwenye nyuzi zilizopita Ila sijafanikiwa kupata msaada, ndiyo maana nimechukua maamuzi ya kuanzisha Uzi mpya.
Kama kichwa cha habari kinavyo someka hapo juu, Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 35, naishi kwenye hii mikoa ya nyanda za juu kusini.
Kulingana na changamoto ninazopitia kwenye maisha mpaka muda huu nahisi kupoteza tumaini kabisa kwenye aya maisha. Kila ninachofanya kinafeli. Kwa hali niliyonayo sasa sina kazi, Hela, nina ishi maisha ya kuungaunga na ya upweke, nahisi kutengwa na kukataliwa na kila mtu.
Nimekuwa nikiishi maisha ya namna hii toka nimeanza harakati za kujitegemea mwaka 2010, nimefanya vibarua mbalimbali sehemu tofauti tofauti kuanzia viwandani, site za ujenzi, biashara ndogo ndogo, uvuvi, nimelima sana mahindi na alizeti, Ila mpaka Sasa sijafanya chochote cha maana zaidi ya kupata pesa ya kula na kuisaidia familia yangu ambayo ni duni, hali ambayo imepelekea kukaa bila kuoa. Yote hii ni kutokana na hali yangu ya maisha kuwa duni. Natamani sana kuwa na familia lakini changamoto zimekuwa nyingi mpaka nahisi kuchanganyikiwa.
Mpaka nimeamua kuandika huku kwenye hili jukwaa ndugu zangu kweli nina shida. Naomba kama Kuna mtu ana connection ya mganga wa kweli ambaye anasaidia kutatua changamoto kama ninazo zipitia Mimi, basi naomba anisaidie namba zake au maelekezo namna ya kufika kwake.
Ndugu zangu mpaka naandika hivi nimekwisha kufikiria kwa kina, kwa sasa sina cha kupoteza zaidi ya kuchukua maamuzi haya ya kwenda kwa mtaalamu ili kama nina mikosi na mabalaa ambayo yananiandama basi nikapate kusaidiwa kuondokana nayo. Milango yangu ya mafanikio ikapate kufunguka na kunyooka kama ilivyo kwa wengine.
Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa yeyote atakae guswa na bandiko langu. Naomba msaada wa hali na mali ndugu zangu ili na Mimi nijikwamue kwenye hili lindi la ufukara linalo niandama.